Oyooooo,
Mimi ni mvulana miaka 29najishughulisha na kazi za hapa na pale zinazonipa kipato. Bila shaka unajua kupenda ni nini? Nimekua nikiona watu wakio tu kwa sababu ya umri kwenda, wengine wameoa alafu wanakuja baadae wanampenda mtu mwingne kitu ambacho sitaki kitokee kwangu.
Nimeshakua na wapenzi kadhaa lakini hamna ambae nishampenda nakua nao tu ili kunikidhia haja tena wengine ni wife material kweli kweli lakini nakua sijawapenda nawaacha. Nashindwa kuelewa yale mapenzi niliyokua nayafikiria wakati nikikua au yale ninayoyaona kwenye movie yapo kweli au vipi maana mimi sikutani hata wakunishika akili kidogo tu simuoni.
Naombeni ushauri kwenu