Miaka 50 ya uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 50 ya uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtitu, Jan 18, 2012.

 1. m

  mtitu Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  MIAKA50 YA UHURU: TULIKOTOKA, TULIPO NA TUNAKOKWENDA

  (KWA MAJADILIANO KATIKA STARTV: 03/12/2011)

  Prof. Mlambiti, M. E.


  Utangulizi

  Katika kujadili mada hii, nimeona niegemeekwa kujadili eneo moja la muhimu katika mchakato wa maendeleo ya nchi kiuchumi.Eneo hilo ni uongozi wa kitaifa wa nchi yetu kwa vile katika nchi uongozi ndiounaobeba jukumu la kuliweka Taifa aidha nafasi ya kupata maendeleo tarajia aula.

  Kwa ujumla, maendeleo ni matokeo yautumiaji fasaa wa mali ya asili ya nchi husika (watu na ardhi) ambao unaleta tija(uongezekaji wa kipato) au huduma inayohitajika na uma wa nchi. Utumiaji fasaawa mali asili ya nchi unategemea sana na Uongozi bora ambao hutunga sera na kuwekamanajimenti yakinifu ambazo kwa pamoja zinatuleta utumiaji fasaa wa mali asiliza nchi. Kwa hiyo UONGOZI BORA NA MANEJIMENTI YAKINIFU, ni msingi au nguzo yakuleta maendeleo endelevu katika nchi yeyote ile.

  Viegezomuhimu kwa mtu anayetaka Uwongozi wa Kitaifa katika nchi ni vifuatavyo.

  1. Ajue hali halisi ya nchi husika yaani ajue tatizo au kikwazo cha kimaendeleo ambacho nchi inakabiliwa
  2. Akisha jua tatizo au kikwazo kinacho kwamisha maendeleo ya nchi, aweke malengo au sera za kutatua au kuondoa kikwazo husika
  3 Kisha atengenezemikakati/programu maalum ya kuitekeleza ili kufanikisha malengo yaliyo pangwa
  4 Aweke mikakati yakufuatilia utekelezaji wa mipango husika na kuona inaendana na michanganuo ilikuhakiki kwamba melengo yaliyopangwa yanafikiwa kama ilivyotarajiwa au la kwa madhumuniya kuweza kurekebisha ikibidi.

  Madhumuniya mada hii

  Lengo kuu ya mada hii ni kujadili kwakifupi hali halisi ya uongozi wa Kitaifa tuliokuwa nao katika kipindi hiki chamiaka 50 ya uhuru wetu kwa kuzingatia viegezo nilivyoelezea hapo.

  Kama Taifa, nchi yetu imefanikiwa kuwa na awamunne za utawala tofauti wa viongozi wa kitaifa yaani awamu ya kwanza ya Baba waTiafa, awamu ya pili ya Mzee Mwinyi, awamu ya Tatu ya Mzee Mkapa na awamu yanne ya Rias Kikwete. Uchambuzi wa Tulikotokaunahusika na awamu tatu zilizopita na uchambuzi wa Tulipo inahusika na awamu yarais wa sasa.  Tulikotoka

  Awamuya kwanza ya Baba wa Taifa
  1. Mwl. Alijua tatizo lilowakabili wananchi na Taifa kiujumla. Ndiyo maana aliwataja maadui watatu wa maendeleo yaani UJINGA, MARADHI NA UMASIKINI
  2. Ili kukabiliana na matatizo haya aliamua kutengeneza sera ya Ujamaa na Kujitegemea na kufuatiwa na Tamko la kitaifa la AZIMIO LA ARUSHA (ARUSHA DECLARATION) ambalo liliweka misingi ya ujamaa wa Kiafrika
  3. Kisha alitengeneza mikakati au programu maalum za kuhakikisha malengo ya sera ya Taifa yanafikiwa: kama vile utaifishaji wa mali za watu binafsi na sera ya ujamaa vijijini (villagization scheme ya 1976)
  4. Aliweka mikakati ya kufuatilia utekelezaji ambao haukuwa makini wala wa karibu. Kama Rais Mwl. alijali zaidi usimamizi wa mambo ya kimataifa kuliko ya kitaifa. Kwa hiyo utekelezaji wa mikakati ya kitaifa ulifanywa na watu ambao hawakujua kiundani matatizo ya nchi na utekelezaji wa mikakati ulifanywa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi.

  Matokea yake ni kutopata maendeleo ya kiuchumi kama ilivyotegemewanasera ya ujamaa na kujitegemea haikufanikiwa.

  Awamu ya pili ya Mzee Mwinyi

  1. Mzee Mwinyi alifikiria tatizo lilokwamisha maendeleo ya taifa ni sera ya Taifa ya Ujamaa na Kujitegemea na jinsi ilivyotekelezwa.
  2. Ili kukabiliana na tatizo au kikwazo hicho aliamua kutokuendelea utekelezaji wa sera ya Ujamaa na kujitegemea kwa kutosema chochote juu yake na kutamka sera ya RUKSA kufanya unachweza ili mradi kinaleta maendeleo ya nchi.
  3. Sera ya kila kitu ni ruksa kukifanya iliimanisha kwamba hakuna mikakati maalum ya utekelezaji kwa vile hakuna mipango maalum ya kufuatilia. Ili kutatua tatizo la uajibikaji, aliamua kujipangia siku maalum za kutatua shida za wananchi kwa kukutana nao ana kwa ana. Sera hilo pamoja na uzuri wake ilibua tatizo la kiutawala kwani wachache aliweza kuwahudumia
  4. Kufuatia na kutokua na mwelekeo wa kitaifa wa kimaendeleo, mipango ya maendeleo yalitekelezwa kiholela bila ya kuwa na dira.

  Matokeo yake ni kua na hali ya walichonacho waendelee na wenginewajitegemee kwa kadri ya uwezo wao. Katika kipindi hiki Utaifa ukaanza kuyeyukana Ubinafsi ukaanza kuota mizizi

  Awamu ya tatu ya Mzee Mkapa

  1. Mzee Mkapa alifikiria tatizo lilokwamisha maendeleo ya taifa ni sera ya Taifa ya Ujamaa na Kujitegemea HASA sera ya uchumi kumilikwa na Uma kupitia mashirika yake.
  2. Ili kukabiliana na tatizo au kikwazo hicho aliamua kuwa na sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya taifa na kukubaliana na masharti ya kimataifa la fedha (IMF), kuruhusu uwekezaji katika kuchimba madini ya taifa na kutekeleza sera ya kupunguza wafanyakazi wa serikali (retrenchment) ili kupunguza matumizi ya serikali kama malipo ya mishahara.
  3. Kisha alitengeneza mikakati au programu maalum za kuhakikisha kwamba malengo ya sera ya ubinafsishaji wa mashirika ya uma imetekelezwa kwa haraka ilivyowezekana bila kutathmini faida au hasara ya sera hiyo. Kwa lugha nyingine kilichotekelezwa si ubinafsishaji (privatization) bali ni ugawanaji wa mali ya uma .
  4. Utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirka ya uma ulifuatiliwa kwa karibu sana na rais wa nchi na ulitekelezwa kwa ukamilfu sana kwa vile kazi ya kugawa ni rahisi kuliko kujenga.

  Matokeo ya sera hiyo ni mali nyingi za Taifa kumilikiwa nawawekezaji wa nje ya nchi kuliko wananchi kwa vile wananchi hawakuwezeshwakuchangia katika mchakato huo. Wenye uwezo wa kifedha na kisiasa walipatanafasi kunufaika na mali ya taifa na wananchi walio wengi kukosa haki yao. Katikakipindi hiki Utaifa ukayeyuka kabisa na sekta binafsi ikatambulika rasmi kama nisekta muhimu katika mchakato wa kuleta maendeleo ya kichumi katika taifa letu.

  Tulipo sasa

  Awamu yanne Rais Kikwete

  1. Rais Kikwete aliona kua nchi haina tatizo lilowakabili wananchi mbali ya kuhimiza uzalishaji zaidi ili kila mtu apate maisha boro kiujumla. Ndiyo maana alianzia na sera ya mabilioni ya Kikwete na kishapo ikifuatiwa na sera ya Kilimo kwanza.
  2. Ili kukabiliana na tatizo hilo aliamua kutengeneza programu ya maendeleo kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza alitekeleza sera ya Mabilioni ya Kikwete na awamu ya pili sera ya Kilimo Kwanza.
  3. Kisha alitengeneza mikakati au programu maalum za kuhakikisha malengo ya sera ya Taifa yanafikiwa. Kwa mabilioni ya Kikwete alishirikisha mabenki ya nchi kufikisha mitaji kwa wananchi Kuhusu sera ya Kilimo Kwanza, alihusisha makampuni na mashirika kuagiza vifaa vya kilimo na taasisi za kilimo zilishirikishwa kwa utafiti na utaalamu wa kilimo cha kisasa.
  4. Mkakati wa kufuatilia mabilioni ya Kikwete unaonekana unalalamikiwa na wengi kama unagawa wananchi katika upatakanaji wake. Mkakati wa kutekeleza Kilimo Kwanza ndio tu umeanza kwa hiyo sio rahisi kusema mkakati huo utaelekea wapi. Bali kwa umbali, mtu anaweza kusema kwamba tatizo litakalotokea katika utekelezaji wa miradi hiyo ya Rias Kikwete litakuwa ukosefu wa ufutiliaji wa karibu na uajibikaji kama inavyotakiwa.

  Matokea tarajia ni kwamba kama ufuatiliaji na uajibikajiusipozingatiwa ipasavyo, ufanisi utakosekana na tija haitapatikana na matarajioya kuleta maendeleo ya kiuchumi hayatafikiwa kama inavyotegemewa.  Tunakokwenda kama Taifa

  Ndiyo kamaTaifa tukubali kwamba “Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele” lakinitukumbuke kwamba kwa kawaida maendeleo ya kiuchumi hayana kikomo kwa sababumahitaji ya binadamu hayana kikomo pia. Kwa hiyo kama binadamu, kuridhika nahatua ya kimaendeleo uliochukua bila ya kujitathmini kama ulipofikia unastahilikuwepo au la ni sawa na kudumiza uwezo wako kama bianadamu. Kwa hiyo kama Taifasi vizuri kuridhika na hatua ya tuiofikia ya kimaendeleo ambayo bado iko chinisana kulinganisha na nchi tulizo kua nazo miaka hamsin iliyopita.Kwa sababuhiyo kuna umhimu mkubwa wa kuchunguza mchakato wetu wa kupata kiongozi wa Taifaambaye anakidhi viegezo nilivyovitaja hapo juu badala ya kupata viongozikufuatia itikadi ya chama chochote kile. Tukifanikiwa kufanya hivyo kunauwezokanomkubwa kuwa siku moja tunaweza kupata kiongozi atakeye tuletea maendeleotarajiwa. Inawezekana kwa kuwa WATU TUNAO, ARDHI TUNAYO NA SERA BORA TUNAZO.

   
Loading...