Miaka 50 ya uhuru bado TUNATAMBAA!!


Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
8,960
Likes
13,795
Points
280
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
8,960 13,795 280
Kama taifa tarehe 9/12/2011 tatutimiza miaka 50 ya Uhuru wa taifa letu. kwa bahati mbaya sana hata hiyo miaka 50 ni ya taifa ambalo haliko au halijulikani, kwani hii ni miaka ya taifa lililokuwa linaitwa Tanganyika, Tanganyika ambayo haipo kwenye Ramani ya dunia wala kwenye medani za kisiasa Ulimwenguni.

Kwa miaka hii 50 kama taifa tumedumaa badala ya kukua kwani kukua kwa taifa kuna vigezo vyake na kikubwa kuliko vyote ni utambulisho (Identity) wa taifa kwa jina na mipaka ya Kijiografia (Geographical Boundaries) pia kuna uhuru wa taifa (sovereignty) sasa hivi vyote bado kwa taifa hili tunalosema tunasheherekea "uhuru' wake havipo.

Utambulisho wa Tanganyika ni upi. Mipaka ya Tanganyika iko wapi hadi wapi na Tanganyika ni huru kama taifa yaani uhuru wa kuamua mambo yake kisiasa? Tanganyika imepakana na nchi nyingine inaitwa Zanzibar ambayo ina kila sifa ya kuitwa taifa. Cha ajabu ni kwamba wananchi wa nchi hiyo wanazo sifa(kupitia Muungano) za kuwa wananchi wa Tanganyika lakini wananchi wa Tanganyika hawana sifa za kuwa wananchi wa Zanzibar.

Mzanzibari anao uwezo wa kumiliki Ardhi Tanganyika, Kuchagua na kuchaguliwa kuwa Kiongozi, kuwa raia na kupata haki zote ambazo mtanganyika anapata. Lakini haki zote hizo mtanganyika hawezi kuzipata Zanzibar. Kwa miaka 50 tumeshindwa kabisa kutanzua mkwamo huu unayoifanya Tanganyika Kutokua.

Kama tunasheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, basi tuitambue!! Tunasheherekea uhuru wa nchi gani ambayo hatuitambui na wala haitambuliki na mataifa mengine duniani. Leo ukisema duniani kuna nchi inaitwa Tanganyika. utaeleweka kweli?
 
M

mharakati

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
1,275
Likes
55
Points
145
M

mharakati

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
1,275 55 145
Nafikiri umefika muda wa kuongelea utanganyika wetu, itakuaje katika muungano wazanzibari wawe wazanzibari na sisi watanganyika hatuna identity eti watanzania, Tanzania ni political entity na siyo watu bila ya kua na identity mtaipendaje nchi yenu ndiyo maana hata hawa viongozi wetu hawana uzalendo namna hii wallah!
 
mikatabafeki

mikatabafeki

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
12,827
Likes
2,112
Points
280
mikatabafeki

mikatabafeki

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
12,827 2,112 280
sual la ZANZIBAR NI NCHI AMA SIO NCHI wangekuepo wenyewe wangeliweka sawa
 

Forum statistics

Threads 1,237,957
Members 475,774
Posts 29,307,847