mwankuga
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 334
- 120
MIAKA 50,NA "NYERERE"MMOJA.
Jina la Dr.Harrison Mwakyembe linavuma kwa sasa,baada ya kufufua usafiri wa reli mjini Dar Es Salaam,na kufanya maamuzi mengine katika Mamlaka ya Bandari,yenye nia ya kutetea masilahi ya wanyonge.Kuna mwingine huyu Magufuli,naye anasifika kwa utendaji mzuri.Hawa wote ni mawaziri wa serikali ya CCM.
Hayo anayoyafanya Makyembe au hata Magufuli yanatoka wapi?Bila shaka ni kwa sababu ya utashi wao.Na hii ndio inanipa shida kuona kesho yetu.Leo tunashangilia kwa usafiri wa reli Dar es Salaam (ni jambo jema),lakini nini hatma ya reli ya Kati?
Haya anayoyafanya Mwakyembe yanatokana na nguvu yake binafsi kuliko serikali!Kesho Mwakyembe akitolewa hiyo wizara,mambo mengi yatarudi palepale!Kama unabisha,hebu niambieni sera ya usafiri wa reli uinasemaje?Mwongozo wa kitaifa kuhusu hayo mambo uko wapi?
Wakati Magufuli akifanya vizuri kwenye barabara enzi za Mkapa "mtoto wa Ulaya",aliyefuata akambadilisha na miradi mingi ya barabara ikasimama.Wakati tunashangilia usafiri wa reli na kuwasifu akina Mwakyembe tufikirie na mbele.
Katika taifa changa kimaendeleo kama la kwetu tunahitaji mfumo zaidi,kuliko mtu mmoja mmoja.Miaka 50 ya uhuru,tumefanikiwa kumjenga mtu mmoja,Nyerere tu!Tukamfanya yeye ni kila kitu.Hata alipoondoka madarakani na kurudi Butiama,bado alihitajika Dar Es Salaam kuamua baadhi ya mambo(Rejea Kitabu ya Uongozi na Hatma ya Tanzania) kwa sababu hatukujenga mfumo wa pamoja,ambao utawafanya watu wafikirie na kuamua.
Kwa namna hii,hata haya mambo ya reli Dar es Salaam (ambalo ni jambo jema) linawajenga zaidi akina Mwakyembe kuliko mfumo,kwani Mwakyembe akiondoka wizara hiyo,hatuna uhakika kama hilo litaendeleza.Maana kila mtu na lwake.
Ndipo najiuliza Dira ya Taifa nini nini?Nguzo au misingi ya Taifa letu ni nini?Taifa tunasimamia wapi?