Miaka 40 Serikali haijahamia Dodoma

Miaka 40 Serikali haijahamia Dodoma

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
dodoma+px.jpg


Kwa ufupi
*.Kukosekana kwa utashi wa kisiasakatika mpango mzima ndiyo hasa chanzo cha hali hiyo ambayo tayariimechukua sura ya kashfa.

Mwaka 1973, yaani miaka 40 iliyopita Serikali iliamua kuhamisha Makao Makuu kutoka Dar es Salaamkwenda Dodoma. Uamuzi huo ulipokewa na wananchi kwa furaha na nderemo, hasa baada ya kutajwasababu za uamuzi huo kwamba ni pamoja na kuhakikisha usalama wa nchi yetu.
Zama hizo zilishuhudia mitikisiko mikubwa katika Bara la Afrika, ambapo nchi za Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Namibia zilikuwa katika harakati za kuondoa ukoloni zikisaidiwa na Tanzania na Zambia. Pia, wakati huo Afrika ya Kusini ilikuwa bado ikiongozwa na utawala wa kidhalimu wa Makaburu.
Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa nchi zilizo mstari wa mbele wa mapambano ya kuzikomboa nchi hizo. Hivyo, kwa kusaidia harakati hizo kijeshi, Tanzania na Zambia zilichukuliwa na mabeberu kama maadui wao wakubwa. Zambia ilikuwa ikishambuliwa kijeshi na Makaburu mara kwa mara, huku Wareno wakifanikiwa kumuua kwa bomu mjini Dar es Salaam kiongozi wa Frelimo, Dk Edwardo Mondlane.
Hivyo, kwa kuzingatia ukweli kwamba Tanzania na Zambia zilikuwa makao makuu ya vyama vya wapigania uhuru wa nchi hizo na kwamba majeshi ya ukombozi namaelfu ya wakimbizi kutoka katika nchi hizo walihifadhiwa Tanzania na Zambia, usalama wa nchi hizo bila shaka ulikuwa mdogo. Hivyo, uamuzi wa kuhamisha Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma ulikuwa sahihi kabisa.
Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kwamba miaka 40 tangu uamuzi huo wa kihistoria uchukuliwe, hakuna lolote la maana lililofanyika. Mpango ulikuwa kwamba Serikali iwe imehamia Dodoma katika kipindi cha miaka 10, yaani ifikapo mwaka 1986. Lakini kwa sababu ambazo haziko wazi, Programu ya kuhamisha Makao Makuu haikutekelezwa kama ilivyotarajiwa, kwani hivi sasani taasisi na wizara chache sana ndizo zimehamia Dodoma na nyingi zimefanya hivyo kinadharia tu, siyo kwa vitendo.
Kukosekana kwa utashi wa kisiasa katika mpango mzima ndiyo hasa chanzo cha hali hiyo ambayo tayari imechukua sura ya kashfa. Badala ya kupata uthubutu na ujasiri wa kuwaeleza wananchi kwamba mpango wa kuhamia Dodoma hawautaki, hivyo kuelekeza mabilioni ya fedha za walipa kodi katika vipaumbele vingine, viongozihao wameendeleza ufujaji wa fedha za wananchi kwa kuwa na ofisi, magari, makazi na watumishi huko Dodoma na Dar es Salaam.
Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu (CDA), ambayo mwaka 1976 ndiyo iliyopewa jukumu la kuendeleza Makao Makuu ili Serikali iweze kuhamia, haina majibu kuhusu nini hasa kimesababisha mpango huo kukwama. Wizara saba ambazo ni Ikulu; Fedha; Mambo ya Nje; Katiba na Sheria; Nishati na Madini; Ulinzi; na Mambo ya Ndani zilipangiwa kuhamia Dodoma kati ya mwaka 1988 na 1993, lakini miaka 20 imepita bado zimejikita jijini Dar es Salaam.
Wizara nyingi bado zipo Dar es Salaam na majengo mengi ya Serikali na balozi za nje zilizo hapa nchini yanaendelea kujengwa. Hiyo ni ishara tosha kwamba mpango waSerikali kuhamia Dodoma haupo tena. Tumeshindwa kujifunza kwa nchi kama Nigeria, Ivory Coast, Malawi, Brazil na nyinginezo ambazo zilihamisha makao makuu ya Serikali katika muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa. Tofauti na viongozi wa nchi hizo, viongozi wetu wamekosa uzalendo na utashiwa kisiasa.

© 2013 MWANANCHI
 
Back
Top Bottom