::
Mapenzi ya siku hizi
Yana kila utelezi
Huniacha domo wazi
Nikitokwa na chozi
Najiuliza tangu juzi
Miaka 30 bila mpenzi
Vip,ntashinda huzuni?
::
Nipatapo mchumba
Akili yangu huyumba
Uhusiano hugomba
Yemsomi mi kayumba
Hunichoma ka mwiba
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Nilimpata mwingine
Pato likaleta mengine
Kapenda waleti nene
Nikaachiwa giza nene
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Nikasema sina bahati
Kaja wa penzi la dhati
Jambo moja kanishiti
Kakibamia haka taiti
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Natamani pata mtoto
Nitimize yangu ndoto
Nisiipite dunia ka mto
Moyo unawaka moto
Miaka 30 bila mpenzi
Je nitashinda huzuni?
::
Umri unaenda upesi
Uzee wanitia wasi
Pesa zanikimbia kasi
Naanza jenga utu hasi
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Mola nimemwomba
Mapambio nimeimba
Mafungo ka majumba
Kimya kila nilipoomba
Miaka 30 bila mpenzi
Vip ntashinda huzuni?
::
Nakata tamaa sasa
Dunia kwangu ni tasa
Sina alama ya kuacha
Nikiaga hii yetu dunia
Furaha inanitoweka
Miaka 30 bila mwenzi
Vip ntashinda huzuni?
=