Miaka 28 ya machungu ya ardhi Loliondo

Miaka 28 ya machungu ya ardhi Loliondo

UTANIPENDA

Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
31
Reaction score
12
MIGOGORO ya ardhi hapa nchini imekuwa tatizo kubwa kiasi cha kusababisha mifarakano hadi mapigano baina ya wananchi kwa wananchi au wananchi dhidi ya wawekezaji.

Ukiorodhesha migogoro mikubwa ya ardhi nchini, huwezi kuuacha uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.

Mara kadhaa wananchi wamekuwa wakipambana na wawekezaji mbalimbali waliowekeza katika eneo hilo zikiwamo kampuni kubwa za uwindaji na nyingine zilizojitwalia maeneo kinyume cha taratibu.

Hata hivyo, migogoro hiyo iliyodumu kwa takriban miaka 28 sasa tangu mwaka 1984, ni kati ya wafugaji wa kabila la Kimaasai na wawekezaji mbalimbali.

Pande hizo mbili zimefikia hatua ya Wanakijiji wa Soit-Sambu kumwandikia barua Mbunge wao, Kaika ole Telele, wakimtaka kuyafikisha malalamiko hayo sehemu husika.

Katika barua hiyo wananchi wameelezea kwa kina historia ya mgogoro huo na wawekezaji, madhara waliyoyapata wafugaji na misaada mbalimbali wanayopatiwa kutokwa kwa NGOs, ikiwamo ile ya kisheria.
Katika barua hiyo ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake, wananchi wamekuwa wakilalamikia kunyanyaswa, ikiwamo kupigwa na wawekezaji kiasi kwamba wanakaa katika ardhi yao kwa hofu katika kipindi cha maisha yao yote.

Barua hiyo ilielezea mgogoro wa ardhi ulioanza katika ardhi ya Sukenya mwaka 1984, baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kushinikiza kuchukuliwa kwa ardhi yao kwa zaidi ya ekari 12,600 na kupewa mwekezaji mmoja.

Wananchi hao walieleza malalamiko yao juu ya ardhi ya Sukenya iliyochukuliwa kwa njia isiyo halali na kusababisha unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu kupitia Kampuni ya utalii ya Thompson Safari na Kampuni ya uwindaji ya Ortello Business Corporation (OBC).

Katika mgogoro huo, Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira (LEAT ) kupitia mradi wao wa msaada wa kisheria unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Friends of the Earth International (FOEI), walifanya uchunguzi na kubaini adha waipatayo wananchi hao.

Katika tafiti mbalimbali mashirika hayo yalibaini mgogoro mkubwa ulianza kuibuka mwaka 2009 katika vijiji vinane vilivyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuvitaja kuwa ni pamoja na Ololosokwani, Oreipiri, Soitsambu, Olorien-Magaiduru, loosoito-Maaloni na Arash.

Utafiti wa LEAT umeeleza kwamba, mapambano baina ya mwekezaji wa OBC mwaka 2009 yalisababisha maafa ya watu wa kabila la Maasai ambapo zaidi ya maboma 200 yaliteketezwa kwa moto na watu zaidi ya 3,000 waliyakimbia makazi yao.

Adha nyingine ambazo zilitokana na mgogoro huo wa ardhi ni wananchi wa jamii hiyo kukosa chakula na mifugo 50,000 ilibaki bila kuwa na sehemu za malisho na wengine kufa.

Hata hivyo, madhara makubwa yalitokea kwa watoto pamoja na kina mama kutokana na kuhangaika kwa kukosa sehemu za makazi na huduma nyingine muhimu zikiwamo za afya.

Kwa upande wa LEAT, ilijitahidi kuwapa misaada mbalimbali ya kisheria wafugaji wa kabila hilo ikiwa ni pamoja na kuungana pamoja kuwapa elimu ya masuala ya ardhi wanakijiji, ikiwa ni pamoja na kujua sheria zake na taratibu zinazotakiwa kufuatwa na wawekezaji.

Hata hivyo walitumia muda huo katika kuendesha kampeni kuhakikisha kuwa sauti za wafugaji na malalamiko yao yanasikika kupitia vyombo mbalimbali vya habari ili kuweza kupata watetezi zaidi katika matatizo yao yanayowakabili.

Hivi karibuni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, alifanya ziara Loliondo na kuzungumzia mgogoro huo huku akiwataka kukaa pamoja kwenye meza ya mazungumzo ili kufikia suluhu kwa amani.
Alisema maadamu matatizo ya Loliondo yanahusu uhifadhi, hivyo ni sharti yatatuliwe, ingawa ni lazima utatuzi wake ufuate sheria pia busara itumike.

Akasisitiza kuwa suala la busara ni muhimu kwa kuwa kuna watu ambao wameishi kwenye baadhi ya maeneo yaliyokuwa na migogoro kwa zaidi ya miaka 40.

Pia akawaahidi kufanya kazi na mbunge wao kwa karibu ili kupata muafaka haraka iwezekanavyo.
Katika mkutano huo, wananchi walitaja kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kampuni ya uwindaji ya OBC kushindwa kuwapa mapato yao kama walivyokubaliana na kutaka yaongezwe.

Aidha, wananchi hao walilalamikia Kampuni nyingine ya Thompson Safaris, inayomiliki eneo lenye vyanzo vitatu vya maji, ambavyo ni muhimu kwa wananchi kuhodhiwa na wawekezaji hao bila wananchi kunufaika.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, wananchi waliopo kwenye eneo la mgogoro ni watu 6,275 na mifugo 38,787.

Hii inahusisha vitongoji vya Sukenya, Mondorosi, Enado-Oshoke, Irmung'i siruai, Masundu na Olepolosi.
Hata hivyo katika kipindi chote cha mgogoro, zimekuwapo taarifa mbalimbali za kupigwa kwa vijana wa Kimaasai na wengine kupelekwa mahakamani.

Miongoni mwa vijana waliowahi kuteswa na kufikishwa mahakamani ni pamoja na Olengoriais Munka na Kanana Ngai mwaka 2008.

Wengine waliokamatwa na kuteswa ni Kutiti Musa, Timan Olelongoi, Kiloki Ndekerei na Joshua Taruru aliyekamatwa na kupigwa na askari wa Thompson, ambapo kwa mujibu wa ripoti ya daktari, kijana huyo hasikii vizuri.

Kutokana na hali hiyo, kuna haja ya Waziri Kagasheki kuhakikisha migogoro hiyo inakwisha na jamii ya wafugaji wanaishi kwa amani kama ilivyo kwa wananchi wengine.

Tanzania Daima - Makala

[TD="bgcolor: #ffffff"]
[/TD]
 
Next time andika kwenye heading kwamba thread yako source ni Tanzania Daima ili tusijisumbue kuifungua thread yako.

Watu makini hatuna muda wa mchezo wa kusoma magazeti yaliyojikita kwenye propaganda.
 
hivi ortelo wana ondoka lini loliondo, maaana miongo miwili imeisha pita sasa, na nyumba upanga tunaona zikijengwa.
 
Nawahurumia watu wa Loliondo.Nasikitika kuwa hawana mtetezi mwenye nguvu kwa sasa. Nadhani kama zingekusanywa saini za wakazi wote wa huko na kwingineko na kuishitaki serikali kwenye mahakama kuu na kwa Mungu labda ingesaidia kuwaondolea dhuruma hii. Iweje kwenye nchi yao mgeni awe na haki kuliko wao? Thamani ya wanyama inawezaje kuwa kubwa kuliko ya watu? Mahatma Ghandhi aliwaongoza wahindi wenzake kuelekea kwenye machimbo ya kutengeneza chumvi kupinga sheria kandamizi ya kuwazuia kitengeneza.licha ya upinzani wa serikali kandamizi, hatimaye wamewezaleo hii kutengeneza hata vyombo vya anga za mbali. Yeye Ghandhi, aliongozwa na kanuni hizi kuu mbili 1. Ni wajibu wa kila raia mwema kuvunja sheria zote ambazo ni dhalimu. 2. Adui/Mtesi wako usimsaidie kukukandamiza kwa kukubaliana naye kwa namna yoyote itakayoendeleza uonevu wake dhidi yako.Saa ya ukombozi ni sasa.
 
Back
Top Bottom