Miaka 2 baada ya kifo cha Hayati Magufuli. Ni chuki au upendo?

toobiter

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
1,073
2,093
Ni karibu miaka miwili sasa tangu taifa lilipoondokewa na aliyekuwa kiongozi mkuu wa nchi, kama taifa tumeshuhudia mijadala ya kihisia na kimantiki kuhusiana na mambo mawili.

Kwanza ni kuhusu John Pombe Magufuli na pili ni kuhusu Raisi John Pombe Magufuli.

Kwa kuzingatia haki ya kutoa maoni tuliyonayo Watanzania wengi wamejaribu kutoa maoni yao kwa kiongozi huyo; wengine pongezi, wengine chambuzi, wengine kulia, wengine kejeli, wengine lawama na wengine hata kudhihaki.

Sitaki kuzungumzia maoni ya watu, maana ni haki yao na uhuru wao kumtathmini na kumuenzi kwa namna wanavyoona kiongozi huyo aliyetangulua mbele za haki.

Lakini kuna somo kubwa ambalo viongozi wote wajao wanapaswa kujifunza kuhusu namna ya kuwaongoza na kuwatawala watanzania kwa kuzingatia maoni wanayoyatoa kuhusu Magufuli na utawala wake.

Unapokuwa kiongozi wa ngazi ya taifa hasa eneo la uraisi kwa chochote unachokifanya,neno lolote unalotamka, msaada wowote unaotoa na uamuzi wowote unaoufanya hakikisha unajiuliza maswali haya mawili.
Je unajenga nchi au unajenga Taifa?

Kwenye suala la kujenga nchi, Magufuli amefanya mengi ya kukumbukwa na yasiyofutika. Mfano wa machache katika mengi ni Barabara, madaraja makubwa, umeme vijijini na mijini, SGR, maji ya ziwa victoria, zahanati na mahospitali, ujenzi wa ikulu na mji wa dodoma, Bwawa la umeme la nyerere na miundombinu yake nk

Kwenye KUJENGA TAIFA namuona Magufuli kwenye suala la covid 19 tu, hapa alisimama kama Rais wa wote na akatuunganisha wote katika wakati ule muhimu kama taifa, tulikunywa tangawizi, tukajifukiza, tukala malimao wachache wakaondoka na wengi saana wakapona ikilinganishwa na mataifa mengine.

Kwenye KUJENGA TAIFA alifeli katika yafuatayo;
1-kulitokeza uadui wa wazi kati ya matajiri na masikini.watu wa chini waliaminishwa kwamba mali/ukwasi wa matajiri ni kama haki yao iliyopotea na kila tukio baya lililowapata matajiri kiuchumi watu wa kipato cha chini walishangilia

2-Mahusiano butu kati ya kundi la waajiriwa hasa wa serikali na wasioajiriwa.jamii ilikuwa inasherekea kila tukio baya lililomgusa mtumishi wa serikali hasa zama za UTUMBUAJI.

Uhusiano mbaya kati ya subordinates na manajements.kulikuwa na mahusiano mabaya mno ya hofu na uwoga kati ya boss na mfanyakazi katika maeneo ya kazi.professionalism iliondoka maeneo ya kazi ila ikaja YES SIR na FEAR, taasisi,serikali,shirika na chochote kile kinaongozwa na vitu viwili tu. Its either LOYALITY or FEAR

Hongera Magufuli huko uliko umetuachia FURAHA, HUZUNI na CHUKI, hakika tutakukumbuka kwa meeengi uliyoyafanya bila kujali ni mema au mabaya kulingana na tafsiri ya mtu.

Wale wenye ndoto ya kuja kuwa viongozi ndani ya taifa hili kumbukeni kujenga TAIFA na NCHI kwa pamoja.
 
Mafisadi na wapenda rushwa ndio hasa wanafurahia kifo chake.
Wapenda maendeleo wataendelea kumkumbuka na kumuenzi
 
Alifeli kwenye fundamentals...

1.Freedom of speech
Hata hao wanaoanzisha nyuzi za kumsifia wamesahau alivyofungia redio na magazeti na JF hii hii ikapelekwa mahakamani...akijaribu kuidhibiti.....Leo wanakuja hapa hapa JF kutulazimisha tumuone shujaa ..

2.Uchumi...
Walioporwa hela waliporwa...kuzidishiwa Kodi,kufungiwa biashara bila kupewa haki ya kwenda mahakamani n.k.. Hadi watu wakaanza kuhifadhi fedha majumbani na kuogopa kufungua biashara...ikabaki umachinga Tu mabarabarani...

3. Demokrasia...
Huku hata sijui tusemeje ...uchaguzi mliona ulivyokuwa...

4.Haki za raia...
Ben Saanane,Roma,Tundu Lissu n.k...

5.kuheshimiana..
Waziri mkuu anaambiwa hadharani tutapiga shangazi zako....
Mawaziri wakubwa hata kiumri kina Kabudi wanaitwa wapumbavu hadharani...

Yako meengi Sana Kwa kweli...
 
Good analysis.. maskin wengi tz walikuwa wanafurahi sn mtu kutumbuliwaa as if yeye ata gain anything kumbee ni null...hii kitu Leo haipo wanaona hangaya hafai
 
Ni karibu miaka miwili sasa tangu taifa lilipoondokewa na aliyekuwa kiongozi mkuu wa nchi, kama taifa tumeshuhudia mijadala ya kihisia na kimantiki kuhusiana na mambo mawili.

Kwanza ni kuhusu John Pombe Magufuli na pili ni kuhusu Raisi John Pombe Magufuli.

Kwa kuzingatia haki ya kutoa maoni tuliyonayo Watanzania wengi wamejaribu kutoa maoni yao kwa kiongozi huyo; wengine pongezi, wengine chambuzi, wengine kulia, wengine kejeli, wengine lawama na wengine hata kudhihaki.

Sitaki kuzungumzia maoni ya watu, maana ni haki yao na uhuru wao kumtathmini na kumuenzi kwa namna wanavyoona kiongozi huyo aliyetangulua mbele za haki.

Lakini kuna somo kubwa ambalo viongozi wote wajao wanapaswa kujifunza kuhusu namna ya kuwaongoza na kuwatawala watanzania kwa kuzingatia maoni wanayoyatoa kuhusu Magufuli na utawala wake.

Unapokuwa kiongozi wa ngazi ya taifa hasa eneo la uraisi kwa chochote unachokifanya,neno lolote unalotamka, msaada wowote unaotoa na uamuzi wowote unaoufanya hakikisha unajiuliza maswali haya mawili.
Je unajenga nchi au unajenga Taifa?

Kwenye suala la kujenga nchi, Magufuli amefanya mengi ya kukumbukwa na yasiyofutika. Mfano wa machache katika mengi ni Barabara, madaraja makubwa, umeme vijijini na mijini, SGR, maji ya ziwa victoria, zahanati na mahospitali, ujenzi wa ikulu na mji wa dodoma, Bwawa la umeme la nyerere na miundombinu yake nk

Kwenye KUJENGA TAIFA namuona Magufuli kwenye suala la covid 19 tu, hapa alisimama kama Rais wa wote na akatuunganisha wote katika wakati ule muhimu kama taifa, tulikunywa tangawizi, tukajifukiza, tukala malimao wachache wakaondoka na wengi saana wakapona ikilinganishwa na mataifa mengine.

Kwenye KUJENGA TAIFA alifeli katika yafuatayo;
1-kulitokeza uadui wa wazi kati ya matajiri na masikini.watu wa chini waliaminishwa kwamba mali/ukwasi wa matajiri ni kama haki yao iliyopotea na kila tukio baya lililowapata matajiri kiuchumi watu wa kipato cha chini walishangilia

2-Mahusiano butu kati ya kundi la waajiriwa hasa wa serikali na wasioajiriwa.jamii ilikuwa inasherekea kila tukio baya lililomgusa mtumishi wa serikali hasa zama za UTUMBUAJI.

Uhusiano mbaya kati ya subordinates na manajements.kulikuwa na mahusiano mabaya mno ya hofu na uwoga kati ya boss na mfanyakazi katika maeneo ya kazi.professionalism iliondoka maeneo ya kazi ila ikaja YES SIR na FEAR, taasisi,serikali,shirika na chochote kile kinaongozwa na vitu viwili tu. Its either LOYALITY or FEAR

Hongera Magufuli huko uliko umetuachia FURAHA, HUZUNI na CHUKI, hakika tutakukumbuka kwa meeengi uliyoyafanya bila kujali ni mema au mabaya kulingana na tafsiri ya mtu.

Wale wenye ndoto ya kuja kuwa viongozi ndani ya taifa hili kumbukeni kujenga TAIFA na NCHI kwa pamoja.
Nchi iliharibiwa
 
Umeongea bila jazba wala bias zozote, ahsante
 
Back
Top Bottom