Miaka zaidi ya 18 sasa toka baba wa taifa atutoke naukumbuka sana mwaka huo 1999 wakati radio tanzania ilipotoa tangazo la kifo chako yalikua ni majonzi ya hali ya juu kwa watanzania wote na watu kipindi hicho walijawa na hofu kubwa uku wengine waliokuwa wazee wakiamini tutavamiwa tena na nchi kuingia kwenye vita kama mwaka 1978.
Wote ni mashahidi jinsi gani tulishuudia Tanzania yenye mshikamano wa hali ya juu kipindi kile kuanzia Wanajeshi,Police na hata wanasiasa tukamzika babu yetu kwa amani kabisa .
Rais Mkapa akihaidi kuendeleza falsafa yake ya kupambana na Umasikini,Ujinga na Maradhi lakini kilichofuata watanzania wote walikiona ikawa historia
ufisadi na kuuza nchi na ushenzi wote ukaasisiwa na Ben hakika ni majonzi kwa vizazi vijavyo..
Najiuliza tu maswali mengi sana yasiyo na majibu iliwezekana vipi kipindi cha nyerere police walikuwa hawana uwezo wa kusumbuana na RAIA wa nchi kamatakamata lakini kwa sasa imekuwa kawaida uonevu juu ya RAIA wa nchi hii?
Iliwezekana vipi nyerere Kuwapa elimu bure wanafunzi wote vyuo vikuu ambao sasa hivi ndio wanawanyima wezao mikopo ya kusoma vyuo vikuu? Pamoja na mapato kuongezeka?
Inakuwaje watu wanasoma na kumaliza uku nchi haina Sera ya kuwafaidi wasomi wake angalau kwa 25%ya waitimu wote wapo mtaani nyerere alitumia uchawi gani kuajiri hata darasa la saba huko nyuma?
Miaka 18 ya kifo cha nyerere watoto bado wanakaa chini wengine kutembea kiromita 10 kufuata shule kwenda kusoma wakati watawala wakipewa almasi ya dola 400 milioni huku wengine wakijenga uwanja wa ndege wa billion zaidi 50 kijijini kwao walipozaliwa..
Miaka zaidi ya 18 police wamekuwa adui wa wananchi maradufu kwa sababu ya uminyaji wa democracy na kupigwa Risasi kwa wapinzani wa serikali imekuwa kawaida na ukihoji unapewa kesi ya uchochezi....
Miaka 18 ya kifo chako babu watu wanatekwa wanateswa wengine kupotea ndani ya taifa lako baba kama livyotokea kwa Ben Saanane hakika ni majonzi makubwa sana.....
Miaka 18, ya kifo chako nchi imegawanyika kwa misingi ya kikabila na kivyama yaani wewe ukiwa na hoja ya kitaifa lazima ubatizwe majina na kila aina Mala gamba mala nyumbu ..
Miaka 18 watawala wanapanga kugeuza katiba kutoka kutawala miaka 5 mpaka miaka 7 nikakumbuka hotuba yako uliyosema kwa katiba tulivyoitengeneza hakuna Rais anaweza tawala miaka zaidi ya 10 lakini haya yanatokea sasa watawala wanajipanga kufanya uhaini juu ya wananchi wao."
Hakika tunakukumbuka sana baba yetu, babu yetu pumzika kwa amani popote ulipo naamini tutaendelea kupambana na kupaza sauti mpaka tupate haki za kweli na si unafiki wa sasa wa baadhi yetu kulialia kimoyomoyo..
R.I.P Baba wa taifa Mwalimu Nyerere..