Miaka 12 bila Mwl. Nyerere...........

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
Jana tumeadhimisha miaka 12 tangu kifo cha baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere. Kumefanyika sherehe kubwa pale Butiama zilizoambatana na kuwashwa kwa mwenge, pia kukawa na midahalo mbalimbali yote ikiwa na lengo la kutathmini na kurudia yale yote ambayo Mw. Nyerere aliyaamini.

Baada ya kuangalia sana yote hayo hii ndio tathmini yangu;

Mtazamo juu ya Mwl. Nyerere
Kwa mara ya kwanza mwaka huu nimeona watu wakiweza kutamka mapungufu ya mwalimu katika uongozi wake, kwa muono wangu hili ni jambo jema sana kama ni kweli lina lengo la kuweka kumbukumbu sawa na kutusaidia hasa sisi vijana kujifunza jambo kutokana na hiyo. Lakini kama ni kwasababu sasa watu wanataka kuhalalisha uozo wanaoufanya sasa kwa kusema hata mwalimu pia alikuwa anakosea naona ni mbinu ya kinafiki ambayo tunatakiwa tuepukane nayo.

Mtazamo wa Mwl. Nyerere juu ya viongozi bora
Katika hotuba yake ya uchaguzi wa mgombea wa uraisi wa CCM wa mwaka 1995 mwalimu aliwahi kusema maneno haya "Lazima tukubali kwamba ni kweli kiongozi wa nchi hii anaweza kutoka nje ya CCM, lakini mimi naamini kiongozi bora ni lazima atoke ndani ya CCM" lakini akaendelea kusema kwamba kiongozi huyo pamoja na kuwa anatoka ndani ya CCM lazima awe na sifa kuu nne,

  1. Apingane na rushwa kwa nguvu zake zote
  2. Ajue kuwa nchi hii inaundwa na wakulima na wafanyakazi ambao ni masikini hivyo ajue ni namna gani atawatoa kwenye umasikini
  3. Asiwe na Udini
  4. Asiwe mkabila
akamalizia kwa kusema kuwa sisi tunaomchagua mtu huyo tuwe tayari kusema huyu ndie kutoka ndani ya mioyo yetu na sio kwa kusitasita kwa mambo haya manne. Kwa sasa siamini kama CCM aliyokuwa anaisema mwalimu wakati ule ndiyo hii ya sasa, tuulizane tu ni nani kati yetu anayeweza kusimama leo akaulizwa kama kiongozi aliyemchagua ana sifa zote kama zilivyoelezwa na mwalimu wakati huo?

Viongozi na unafiki wa kumuenzi mwalimu
Imekuwa desturi sasa kwa viongozi kila 14 October kwenda Butiama na kujifanya wanamuenzi mwalimu. Tukiwa wakweli tutagundua kuwa kwa sasa hakuna kiongozi yoyote wa juu nchi hii anayemuongelea Mwalimu Nyerere kwa falsafa yake hata mmoja, kwanini? Sababu ni kwamba hakuna mtu anayefuata falsafa hiyo na kwasababu wanajua kuwa watanzania wengi bado wanaamini mwalimu ndiye alikuwa kiongozi bora na si bora kiongozi kama ilivyo sasa, hawathubutu kumpinga kwakuwa wanajua wataishia kupigwa mawe.

Tathmini yangu
Nchi yetu imekosa mwelekeo kwa kuwa tumekosa nahodha, sitaki kusema tunahitaji nahodha kutoka upinzani au CCM bali tunahitaji nahodha anayejua mahitaji yetu kwa sasa na kuendelea mbele. Sera ya Ubepari imeshindwa si tu Tanzania au Afrika pekee bali dunia nzima (mfano ni Ugiriki, Italia, Hispania na nchi nyingine za ulaya) tazama mtikisiko wa kiuchumi ulioipata Dunia ambao kimsingi uliletwa na sera hizi za kibepari, kama nchi hebu turudi na tuamue ni namna gani tunaenda mbele na sio kusubiri watu wengine watuamulie namna ya kuishi.

Mwalimu alipinga sana rushwa, kwa sasa sio tena rushwa ni wizi na kibaya hao wezi hawashughulikiwi kwasababu huenda wakawa wanakula wizi na wanaotakiwa kuwashughulikia au ni marafiki zao hivyo wanaoneana haya. Tumekuwa nchi ya walalamikaji, juzi nimemsikia jaji Warioba akisema kuwa tumekuwa taifa la walalamikaji, cha kuchekesha ni kwamba hata yeye pia alikuwa anawalalamikia hao wanaolalamika (kila mtu ni mlalamikaji)

Zamani tulikuwa tunatarajia majibu kutoka kwa viongozi na ndipo tunapommiss zaidi mwalimu. Leo hata raisi pia analalamika tena anawalalamikia watu wake wa kumsaidia kuwa hawafanyi kazi na anatulalamikia sisi sijui tumsaidieje! Mwisho sitaki mchukue muda mrefu kusoma haya, kama nchi tunahitaji kufanya review kama nchi na kuachana na habari za nani kasema nini na kamlaumu nani.......

Karibuni..........
 

BMT

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
586
222
tanzania bila baba wa taifa miaka 12 inaonyesha kuyumba angalau awam ya 3 kidgo wananchi maskin walipata ahuen ya maisha, lkni awam hii ya 4 maisha yamekuwa magumu kupta maelezo,na cjui nchi inakwenda wapi,
on behalf of poor tanzanians real we do remember mzee nyerere
 

ngwendu

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
1,965
173
mkuu madhaifu ya mwalimu yapo mengi tu. kwa kifupi hakuna mtanzania alieishi kipindi cha nyerere anayeweza kupaza sauti kuwa aliishi maisha bora kuliko kipindi cha marais watatu waliomfuata. Anayebisha hata humu jf aje na data.
Binafsi nikikumbuka jinsi tulivyokuwa tukipanga mistari kwenye maduka ya ushirika kununua kipande cha sababu na kipakti cha chumvi huwa sitaki hata kusikia.
baadhi ya madhaifu yake
1. mwl na ujamaa wake ulitufanya tuwe wavivu na masikini wa kutupwa kwani hakuna ambaye angejituma kufanya kazi zaidi kwa uwezo wake kwani wote tunatakiwa kuwa sawa kumbuka mashamba ya vijiji
2. alishindwa kusimamia elimu kwani mpaka anatoka madarakani hatukuwa na wataalamu wengi japokuwa wengi wanamsifu eti elimu ilikuwa bure. kwangu haina maana kama unafundisha watu 50 kati ya watu 30milioni. kumbuka kenya walipata uhuru mwaka mmoja baada yetu lakini leo hatuwafikii.
3. mwl kati anaondoka madarakani uchumi wetu ulikuwaje? jibu unalo kichani
4. Eti mwalimu alifuta ujinga kwa watu kujua kusoma na kuandika kwa zaidi ya 90%. Ndugu zangu hivi ukijua kusoma na kuandika ndo umefuta ujinga? kuna haja gani ya kuwa na form 4 hadi univarsities (au ndo maana hakuwekeza huko akijua watu wakijua kusoma na kuandika inatosha?) shule za msingi sizinatutosha? Nawakoloni siwalitufundisha baadhi yetu kusoma na kuandika ili tuwatumikie? kunatofauti gani na ya mwalimu? You PIPO think critically.
5. namengineyo mengi

mazuri yake
1. rasilimali zetu alizitunza na hili namsifu si sawa na haya many'ang'au yanayotutawala sasa hivi (nasema yanayotutawala na si kutuongoza kwani hayasikilizi maoni yetu)
2. Ticha alipambana na rushwa hili nampa 100%
3. alifanikiwa kujenga umoja wakitaifa japokuwa kuna baadhi ya jamii leo hii zina lalamika kuwa zilisahauliwa na utawala wake-na hili si la kupuuzia hata kidogo
4. alisaidia kuwakomboa wenzetu wakusini mwa jangwa la sahara kwa kutumia rasilimali zetu (japokuwa wao hawatujali-hii nashindwa hata niiweke wapi? kwenye madaifu au mazuri? Labda niwaachie swali moja tu, hivi kuna mmoja wetu anaweza kuacha watoto wake wakifa njaa nyumbani halafu akawapa jirani chakula?)

List i ndefu unaweza endeleza. kama nimekukera. leave me alone.
 

ngwendu

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
1,965
173
tanzania bila baba wa taifa miaka 12 inaonyesha kuyumba angalau awam ya 3 kidgo wananchi maskin walipata ahuen ya maisha, lkni awam hii ya 4 maisha yamekuwa magumu kupta maelezo,na cjui nchi inakwenda wapi,
on behalf of poor tanzanians real we do remember mzee nyerere
ndugu yangu wewe unaishi nchi ipi? wananchi wapi walipata ahueni awamu 3? Labda wafanyakazi kidogo kwani awamu ya 2 haikuwajali. lakini wananchi wakawaida tulikuwa na shida kupita kiasi mkuu. Nashauri uandike ukweli. weka ushabiki pembeni hautatusaidia.
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
Kuna kitu kinasemwa kwamba PRACTICE WHAT U BELIEVE hapa inasemekana mwalimu had to retire ili kuacha mtu mwingine ndo afanye transformation toka kwenye Ujamaa kwenda Ubepari tulimo sasa. This shows that he never agreed with Ubepari na pressure za IMF na WB
 

Kabembe

JF-Expert Member
Feb 11, 2009
2,551
1,733
Tanzania ya sasa baada ya Mwalimu imejaa Manaizesheni na Mabenzi,yaani ni ku-pretend and stealing from the poor!
 

Kabembe

JF-Expert Member
Feb 11, 2009
2,551
1,733
Tanzania ya sasa baada ya Mwalimu imejaa Manaizesheni na Mabenzi,yaani ni ku-pretend and stealing from the poor!
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,779
main.jpg

Asha Salum Kilungi (70) visibly moved at Mwalimu JK Nyerere commemorative symposium held at University of Dar es Salaam yesterday. She was overcome with emotion as she expressed her belated appreciation for the Father of the Nation`s intervention that she said helped her get back her plot earlier seized by a conman
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
main.jpg

Asha Salum Kilungi (70) visibly moved at Mwalimu JK Nyerere commemorative symposium held at University of Dar es Salaam yesterday. She was overcome with emotion as she expressed her belated appreciation for the Father of the Nation`s intervention that she said helped her get back her plot earlier seized by a conman

What i am sure of now the people she would have run to, would have been the same con men want to steal her plot
 

mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
185
Viongozi wetu ni wanafiki wanaimba kumuenzi na kusikiliza hotuba zake na kum nukuu sana maneno yake lakini wanamkejeli kwani nyuma ya pazia wanagonga glass za mvinyo kwa kuyakiuka yale ya Mwl
 

myhem

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
933
356
kikubwa ninachokumbuka ni kuwa pengo kati ya tajiri na maskini halikuwa kubwa kama ilivyo sasa.Angalia hata mishahara ya serilkalini sasa hivi na ulinganishe kati kima cha juu na cha chini kisha fuatilia enzi zake tofauti ya mishahara ilikuwaje?
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
Hivi kwa tathmini ya haraka, ni kiasi gani cha pesa kimetumika kwa ile siku moja pale Butiama? Je hiyo pesa ingetumika kufanya mambo mangapi ya maendeleo ya nchi yetu kuliko kujaza mafuta, kulipia hoteli na kuwapa posho wapuuzi ambao wanaenda Butiama kutalii na sio kufanya lolote la maana?
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,752
1,856
Viongozi wetu ni wanafiki wanaimba kumuenzi na kusikiliza hotuba zake na kum nukuu sana maneno yake lakini wanamkejeli kwani nyuma ya pazia wanagonga glass za mvinyo kwa kuyakiuka yale ya Mwl
Nimeipenda Avatar yako inaonyesha namna ulivyo mzalendo wa ukweli
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom