Miaka 10 ya Ugaidi Marekani, Septemba 11, 2001 - 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miaka 10 ya Ugaidi Marekani, Septemba 11, 2001 - 2011

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by wakuwaza, Aug 24, 2011.

 1. w

  wakuwaza JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Septemba 11, 2011 itatimia miaka 10 tangu yalipofanyika mashambulizi ya ugaidi huko Marekani. Lakini kabla tarehe ya maadhimisho hayo haijafika, nimesoma kitabu kinachoitwa HADAA: Unafiki Marekani, Ugaidi Duniani. Kitabu hicho kimeandikwa na William Shao. Yeye anadai kuwa tukio lote la kuanzia Septemba 11, 2001 hadi kuuawa kwa Osama bin Laden ni hadithi iliyotungwa kuihadaa dunia. Sikumwelewa mwandishi huyo wakati naanza kusoma kitabu chake, lakini nilipomaliza nikajikuta nimechanganyikiwa zaidi.

  Yeye anadai hakukuwa na magaidi katika ndege zile. Wala Osama hakuhusika. Ameandika kuwa Marekani haijawahi kumtafuta Osama wala haijamuua kama ilivyodai. Hoja alizotumia mwandishi huyo zinashawishi sana. Kama kitabu hicho kingekuwa kimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza labda kingeitia doa serikali ya Marekani. Dibaji ya kitabu hicho imeanza kwa kuwatahadharisha wasomaji. Nanukuu:

  "Katika kitabu hiki, ndugu msomaji, utasoma habari nyingi ambazo pengine hungependa kuzisikia wala kuzisoma, lakini zinatoa changamoto kubwa kwa akili zetu. Kama hujawahi kusikia habari zinazofanana na hizi utakazosoma katika kitabu hiki kuhusu yale yanayotukia duniani, huenda zikakushtua, kukutisha na kukushangaza. Ikiwa hauko tayari kukabiliana nazo, tafadhali kifunge kitabu hiki na ukitupe mbali nawe. Usijaribu kufungua ukurasa mwingine baada ya huu. Lakini ikiwa utavumilia na kukisoma hata ukurasa wa mwisho, huenda imani yako katika mambo mengi kuhusu tukio la Septemba 11, 2001 na ‘kuuawa’ kwa Osama bin Laden Mei 2, 2011 ikabadilika na kuwa tofauti na ilivyokuwa kabla hujakisoma. Kila sura moja ya kitabu hiki ni sawa na kipande kimoja cha picha nzima, lakini kikiwa chenyewe siyo picha nzima. Picha nzima utaiona baada ya kusoma sura zote hadi sentensi ya mwisho. Matukio ya ‘ugaidi’ kuanzia Septemba 11, 2001 Marekani iliposhambuliwa hadi Mei 2, 2011 ilipodaiwa kuwa Osama bin Laden aliuawa na Wamarekani akiwa Abbottabad, Pakistan, ni za kutungwa zaidi ili kuidanganya dunia badala ya kuiambia ukweli. Uongo umetawala mambo hayo kuliko ukweli ulivyotawala. Waliotajwa kuhusika na ugaidi huo hawakutajwa, na waliotajwa hawakuhusika."


  Kwa kweli nilikuwa naamini kila kilichosemwa kuhusu ugaidi huo, lakini sasa nadiriki kusema kuwa imani yangu imebadilika kabisa baada ya kusoma kitabu hicho. Kazi kwenu wanajamvi.
   
 2. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hicho kitabu kinaitwaje? Tujulishe tafadhali.
   
 3. w

  wakuwaza JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kitabu kinaitwa HADAA: UNAFIKI MAREKANI NA UGAIDI DUNIANI. Kimeandikwa na mwandishi William Shao. Nilikipata Tanzania Publishing House mtaa wa Samora maarufu kama TPH
   
Loading...