Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Muda huu kuna mhubiri wa Injili, Daudi Mashimo aka Komandoo wa Yesu, anaendelea na mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo akiwataka wanaojiita manabii nchini Tanzania waache mara moja kujiita hivyo kwa sababu unabii unatoka kwa Mungu na kwamba nabii wa kweli atakuja wakati utakapofika.
Amewapa siku 14 watubu, vinginevyo yuko tayari kutoa hadharani siri zao na nguvu wanazozitumia kwa sababu wanachofanya ni utapeli wa kiroho na kuwapotosha watu.
"Watanzania wengi wana hali ngumu kimaisha, sasa hawa matapeli wa kiroho wanatumia fursa hiyo kuwahadaa na kuwapotosha, nawataka waache mara moja vinginevyo baada ya siku 14 nitatoa siri zao na jinsi wanavyotumia nguvu za miujiza za 'Mngindo' ambazo ni za kichawi," anaeleza.