Mhonga achangia kituo cha afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhonga achangia kituo cha afya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Jan 20, 2010.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  KITUO cha Afya cha Mwamgongo kilichopo Kigoma Vijijini, kaskazini mwa Ziwa Tanganyika kimepatiwa umeme wa nguvu ya kujua ili kunusuru mazingira hatarishi yaliyopo katika kituo hicho.
  Kituo hicho ambacho kina wodi ya kujifungulia kina mama wajawazito, maabara na jokofu la kuhifadhia dawa hakijawahi kupata umeme tangu kilipoanzishwa miaka 14 iliyopita na hivyo kusababisha matatizo makubwa kwa wagonjwa.
  Hata hivyo, matatizo hayo hivi sasa yameondoka baada ya Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhonga Said Ruhwanya, kutoa msaada wa vifaa vya umeme wa jua vyenye thamani ya sh milioni 27.
  Akikabidhi misaada hiyo, Mhonga alisema alifikia uamuzi huo, baada ya kuguswa na yanayowakabili kina mama. Msaada huo utasaidia vijiji saba ambavyo ni Bugamba, Kagunga, Zashe, Kiziba, Mwamgongo, Mtanga na Kigalye.
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..atagombea ubunge mwaka huu?

  ..sioni huyu akishambuliwa kama ilivyokuwa kwa January Makamba.
   
Loading...