figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Iddi Mashaka, amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utunguaji wa helikopta namba 88HF na kusababisha kifo cha rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza.
Imeelezwa kuwa Mashaka, ambaye pia ni ofisa intelijensia wa hifadhi hiyo, anadaiwa kuwa kinara mkubwa wa ujangili katika hifadhi mbalimbali zilizoko Kanda ya Ziwa kwa kutoa ushirikiano kwa majangili pamoja na kuwaazimisha silaha za kufanyia uhalifu huo.
Hii ni aibu sana, wale tunaowaamini ndio wanaotuangusha. Nashauri sheria za hifadhi za taifa zifanyiwe masahihisho ili watu kama hawa wanyongwe na kufilisiwa.