MHHHH 🀭

Carasco Putin

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2022
Posts
14,355
Reaction score
40,409
Wewe sio wa kwanza. Kila mtu unayemuona amepiga hatua kwenye maisha yake kuna siku aliwahi kukata tamaa.

Kuna watu leo ukiwaona unaweza kudhani kuwa kila siku wao wanashinda tu, ukiwakaribia ndio utajua kuwa kuna wakati walitamani waishie njiani na wasiendelee mbele.

Chochote unachokipitia leo, Hata Kama kinakupa maumivu namna gani, usikubali kuhitimisha kuwa umefika mwisho na hakuna tumaini tena.

Kuna wengi wanatarajia utashindwa ila Mungu amejiandaa kukusaidia kushinda,

kuna wengi ambao wanatarajia kuwa ndio utakuwa mwisho wako, ila Mungu anajiandaa kukufungulia ukurasa mpya, usikate tamaa.

Kuna Watu wanapitia magumu Kama ya kwako leo, na watashinda, nawe jiunge nao kuwa mshindi.

Leo kuwa sehemu ya faraja kwa mtu Mmoja kwa kushare naye ujumbe huu, MUNGU atakubariki.
πŸ₯‡ 🧠 ✨
 
"Nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya kwa maana wewe upo pamoja nami.......

Gongo lako na fimbo yako vyanifariji....

Inspired Psalm_23
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…