mhhh! BAADA YA CUF ,SASA CHADEMA

Umenena point ya msingi sana.... Viongozi wetu wanatakiwa kuliona hilo mapema na kujifunza kutoka katika vyma hivyo vya NCCR na CUF, nafikiri kuna umuhimu wa kulipa kipaumbele na kuweka juhudi kubwa ili kuhakikisha hayatokei hayo. Hilo litawezekana kwa kuzingatia yafuatayo;
  1. Kuhakikisha tunachagua viongozi wanaokipenda chama na sio vyeo
  2. Kuhakikisha wanachama wapya wanaohamia kwenye chama kutoka vyama vingine hawapewi nafasi za juu za chama bila kutazamwa mienendo yao kwa muda mrefu.
  3. Kuwaepuka wanachama wapya wanaohamia kwa ajili ya kupata nafasi za uongozi kama ubunge na nyinginezo.
  4. Kuepuka makundi katika chama na kuhakikisha makundi yote yanatokomezwa mara yanapogundulika.
  5. etc

Tukizingatia hayo na mengine ya mengine, tutakiepusha chama chetu na migogoro mikubwa ambayo itasababisha mgawanyiko mkubwa utakaokipoteza chama chetu makini tunachokipenda.
 
Cdm ingefikisha vibuda viwili!
 
Ccm huvizia migogoro ndani ya vyama pinzani ili wavisambaratishe, mnaukumbuka ule mgogoro wa madiwani arusha?
 
Ukisifiwa na SHETANI ujue una matatizo.

CCM hawawezi kuiombea wala kuisemea vizuri CDM. That is expected.
 

katika post yako sijaona shimo lolote ulilolionyesha ili tusitumbukie zaidi ya utabiri,sadia na ueleze ni lipi hilo unaloliona linainyemelea gdm mbali na huo utabiri kuwa baada ya cuf ni cdm wakati kuna vyama vingine zaidi ya cdm lakini hujataka kuvitabiria.
 
Kiukweli CUF haitakufa,itabakia ktk ngome yake huko Pemba na Mji Mkongwe Unguja. Chama ambacho ambacho nasema kinaweza kufa ni CCM na zaidi kitakapo ondolewa madarakani. Wanachama wamefuata madaraka ya dola na utajiri kupitia tenda za serikali. Sababu nyingine ni uhasama,chuki na makundi yaliyopo CCM kufikia kutuhumiana kutaka kuuana! Hawa hawawezi bakia ktk chama kimoja kwa muda mrefu ujao.
 

Kwa ulicho bandika, eeh!
Basi CDM, Itashuhudia mazishi ya ccm!
Manake ndio yenye mtafaaruku ndani ya chama chao! au?
kwa taarifa tu, CDM itadumu kwa sababu, watu wameivaa Roho ya CDM! Haijalishi una chama au huna! Ukiivua hiyo Roho uko uchi! Na kama hujui migogoro mingi iliyo ndani ya ccm chanzo ni Roho ya CDM!
 
Unaandika utumbo lakini unajua bila heading kuweka neno CDM hakuna atakayeifungua thread yako

usitukane, jenga hoja. Utumbo ni nini. hapa ni majadiriano, sio kutukanana. Jenga hoja umbadilishe mwenzako. Sijapenda your way of putting arguments
 

hapana rafiki, ni kuwa huyu anatahadharisha CDM wawe makini haya yanayotokea vyama vingine yasije yakatokea. Unaangalia wenzetu wamekorofishwa na nini, nawe unachukua hatua za makusudi kuona kama kuna mianya ya hiyo cause unaizuia mapema. Kumbuka kuna wakati Zito na Slaa walikuwa katika "bad" terms, yakaisha. Nadhani waliangalia mwanya wakauziba. Huyu aliyepost ana nia njema.
 
alichosema mtoa maaada unapaswa kukitafakari sisi sote ni wana cdm lakini sio kwa maana ya kusifia kila kitu ambacho kimo ndani ya chama hata kama ni kibaya ikumbukwe kuwa bado kuna watu wanapenda ndani ya cdm kuona mgawanyiko kati ya mwkt na naibu katibu mkuu unakuwepo na kudumu kwa mda mrefu ili wao wapate nafasi ya kupika majungu kati ya mwkt (mbowe) na naibu katibu mkuu(zitto) hili pia ni tatizo tena wengi ni watumishi wa makao makuu ambao wana nafasi nzuri ya kushauri lakini hawafanyi hivyo
 
kiukweli hapa tanzania demokrasia itakuwa ya kweli kama tukibakiwa na vyama viwili imara.utitiri wa vyama nalo ni tatizo lingine
 
kiukweli hapa tanzania demokrasia itakuwa ya kweli kama tukibakiwa na vyama viwili imara.utitiri wa vyama nalo ni tatizo lingine

Vimeshabaki viwili tu mkuu baada ya CUF kuzikwa
 
Aisee hiyo ni cra p takatifu

Sio c rap, jamaa ana pointi. Suala la kujiuliza ni namna gani chadema wamejipanga kukwepa mitego ambayo nccr, tlp na sasa cuf wamenasa..
 
Baada ya CUF inafuata CCM,dalili zimeanza onekana
nakuunga mkono bratha akitaka kujua cdm ni imara yeye aangalie hotuba za mwenyekiti wa ccm anavyo lala mika mfano ipo mingi akiwa mwanza jk anasema kwa sasa pesa hazitoshi inabidi muanze kutafuta vyanzo vingine vya mapato ruzuku imepungua(cdm imeongeza wabunge)...tumewanulia land cruise lakini hamfiki kunakotakiwa(hawana pesa za diesel)mabano ni maneno yangu
 
Tatizo letu tunapenda kuhisi vitu ndo maana hatuelezi matatizo husika na kutoa mapendekezo. Fine cdm chaweza kufata kwa cuf kwa lipi labda;sera mbovu,uongozi mbovu,makundi ndani ya chama,ulafi wa madaraka..... Toa mifano na mapendekezo ili tuone hoja yako ina mashiko.
 
Hii biashara ya kujihami imeanza lini? Nape baada ya kutoa mada yake akajihami kweli. Wewe nawe hujiamini. Eti utatukanwa. Nani akutukane wewe *******? (lol?)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…