Mheshimiwa Yutong (MB) aongea na wazee wa JF

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,601
338
Muhuri wa Utengano wa JF
Idara ya Siri, Habari na Mwasiliano - Makao makuu
P.O. Box 2011
Da Lala Salama

Taarivya kwa byombo bya habari

Ifuatayo ni hotuba ya Mheshimiwa sana Yutong (MB)
Ndungu wazee wa JF niwapongeze kwa kuhudhuria wito wangu, pili niwapongeze mke wangu mama Preta Yutong kwa kuwa mvumilivu na msikivu, na bila kumsahau mkuu wa kambi ya upinzani JF bwana Rajeo pamoja na msemaji mkuu wake Faiza Foxy. Leo nitazungumzia mabo kadhaa ktk kufunga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012.

1. Hali ya sihasa injini
Ndugu wazee kama mnavyojua hali ya sihasa nchini sasa ni tete hasa kwa upinzani mkubwa ambao JF tunaupata. Tumefanikiwa kuzuia maandamano zaidi ya 100 yaliyokuwa yafanyike inji nzima. Aidha katika kipindi hiki pia tuliweza kuteua watu 1000 kushika nyazifa ktk idara za sirikali hii. Kati ya hao tuliweza kuteua machangudoa 50 kushika nafasi za ukuu wa wiulaya na makameruni 10 kuongoza taasisi nyeti za serikali. Hayo nimafanikio makubwa sana.

2. Uchumi
Ukusanyaji wa kodi umeweza kushuka kutoka bil 1000 hadi kufikia bil 200, aidha shilingi yetu imefanikiwa kushuka dhamani kutoka 1300 mpaka 1800 kwa dola moja, hayo ni mafanikio makubwa. Uwekezaji nchini umepanda. Kwani sasa tumekaribisha wawekezaji mpaka wa mitumba na gereji bubu. Magari mabovu yameongezeka sana.

3. Ilimu dunia
Elimu dunia imeshuka kiwango kwa asilimia 10, aidha mikopo kwa wanafunzi imepunguzwa kutoka 100% hadi 40% hayo ni mambo ya kujivunia sana. Shule na vyuo vingi vimezidi kuharibika kwa kukosa matengenezo kutokana na uhaba wa fedha kwani fedha.

4. Afya
Ukimwi umeongezeka kwa 30% kutokana na kuhamasisha watu kufanya ngono kwa wingi na kujenga magesti mengi sana. aisha kukabiliana na upungufu wa magesti serikali iliruhusu gesti bubu. Aidha pia sirikali ilitaka watu kuwekeza kwenye madanguro ili kuongeza kasi ya ongezeko la ukimwi. Kwa upande wa malaria serikali itaendelea kupambana na mbumbu badala ya kupambana na vyanzo vya mbu.

5. Starehe
Serikali itaendelea kuhamasisha watu kujenga mabaa/kumbi za musiki karibu na makazi ya wananchi ili kuongeza burudani zaidi. Aidha serikali inampango wa kujenga night klabu 10 ktk jiji la dar es salaam ili kuwawezesha machangudoa zaidi kufanya biashara maana mahitaji yamekuwa ni makubwa sana kwa sasa.

6. Usafiri
Serikali imeweza kuboresha usafiri kwa kuwa na wajenzi wengi wa bodi za mabasi ambazo hazina standard, hivyo kila kampuni imekuwa ikiunda basi design inayotaka yenyewe na hii imesababisha ajali nyingi sana. Daladala pia kila mtu na yake mwenye kosta haya, mwenye isuzu journey sawa, mwenye kipanya haya, mwenye mangi sawa, dcm sawa. Haya ni mafanikio makubwa sana.

Matarajio kwa mwaka 2012
Sirikali inafanya jitihada za kumrudisha theutamu ili watu waendelee kuburudika kwani utafiti uliofanywa umeonyesha kwamba theutamu ilikuwa inaangaliwa na watu wa marika yote vijana hadi wazee ktk maofisi na cafe zote nchini hasa dar.

asandenyi sana

Imesiniwa na katibu mkuu makao makuu JF
 
Naona Muheshi-mihogo (muhesi-miwa) umesahau mafanikio yafuatayo:-

1. Umefanikiwa kuua wananchi wako kwa makusudi katika ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe wa serikali yako hasa kitengo cha trafic pale wanapoona magari ni mabovu/wamejaza abiria kupita kiasi / basi zinaenda mwendo kasi, wao wanapokea rushwa na kuyaruuhusu yaendelee na safari kwani abiria waliopo humu sio ndugu zao.

Pia kung'ang'ania kwako kutunza mabomu yaliyo expire kumesaidiakupunguza kwa kuua watu zaidi ya 200 huku ukitangaza waliokufa ni 20 tu.

Ajali ya meli zanzibar imekusaidia kupunguza watu 2400, na ajali nyinginezo ambazo wewe unajivunia kama kutokuwa na miundombunu bora kulikosababishwa leo hii kulia kwa kupoteza mamia ya wa dar es salaam kwa mafuriko.

2. Muheshi-mihogo (mheshi-miwa), umesahau kujipongeza kwa muhishimiwa kuwa raisi mtalii wa kwanza duniani, kwani amefanikiwa kupanda mabembea, kupiga picha na wanamziki maarufu duniani e.g 50cents n.k na kuvunja rekodi ya kutembelea nchi zote duniani ktk kipindi cha miaka 6 tu

3. Muheshi-mihogo (mheshi-miwa), umesahau kujipongeza kwa kuanzisha shule za kata nyingi sana zinazotusaidia kuwafundishwa watoto jinsi ya kuuza pipi na ubuyu kwani hawasomi wanashinda wakifanya biashara hiyo.

Naomba kuwasilisha muheshi-mihogo )mheshi-miwa
 
Back
Top Bottom