GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Mheshimiwa Waziri Mkuu natambua upo salama kabisa na unaendelea na majukumu yako ya Kiutawala na juhudi zenu hakika kwa kipindi hiki kifupi tu chenu cha Uongozi hakika tunaziona japo changamoto za hapa na pale haziwezi kukosekana.
Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaishukuru Serikali kwa kuamua kutuletea aina hii ya usafiri ambayo mlidhani pengine itapunguza adha lakini badala yake tunaoutumia huu usafiri kila kukicha tumeona tu kilichofanyika ni kubadili tu jina kutoka DALADALA na kuitwa DALADALA za MWENDOKASI.
Mheshimiwa Waziri Mkuu nisaidie kuniulizia kwa UDART wenyewe haya maswali yangu yafuatayo:
Ukweli ni kwamba mpaka sasa sisi abiria hatujaona tofauti kati ya haya Mabasi yenu ya MWENDOKASI na usafiri wetu huu wa DALADALA sana sana labda tofauti ni kuwahi tu kufika unapoenda kitu ambacho hata huku katika usafiri wetu tuliouzoea linaweza kufanyika endapo askari wa barabarani wakiwa wameamka vizuri siku hiyo au zile traffic lights zikitumika.
Ila kama nyie kwenu neno MWENDOKASI ni zile rangi za mabasi, zile tai za madereva wao, ile milango kufunguliwa kwa mashine na madereva wao kutumia vipaza sauti basi mmefaulu ila generally huduma za UDART siyo zile ambazo wengi wetu tulikuwa tukizitegemea au zile ambazo kwa waliotembea kidogo nchi za Watu wameziona na niseme tu ukweli Mheshimiwa Waziri Mkuu hakuna kilichofanyika bali naona ni usanii usanii tupu umetawala na nakuomba lifanyie tena kazi hili suala la UDART ili hizi adha zisiwepo kabisa na nahisi pia kuna " kamchezo " UDART wanakafanya ila Wewe bado hujakagundua basi si vibaya ukatumia huu UZI wangu kama sehemu yako ya kuanzia na kama ikishindikana basi ni kheri huu usafiri mkauita tu MWENDOKASI NA KARAHA tutawaelewa zaidi.
Akhsante na naomba kuwasilisha.

- Kama mabasi yaliyoagizwa na yaliyopo kutoa huduma ni 300 kama tulivyohabarishwa sasa inakuwaje yanayotoa huduma jijini hayazidi hata 30?
- Kama wao ndiyo wanatoa huduma kwetu sasa iweje tena sisi abiria tunasumbuliwa na hadi kulazimishwa kwenda na chenji kamili pale madirishani ndipo upate tiketi yako je isingekuwa busara kwa wao UDART kufanya utaratibu na Benki Kuu ili wawape kila siku hizo chenji za Tsh 50 ambazo zinakuwa KERO kwetu sisi abiria?
- Kuna tofauti gani kati ya usafiri wetu huu wa DALADALA na huu wa UDART kama ukiingia ndani ya basi mnajazana hadi wengine wanakaa pembezoni kwenye kingo? Je hii ndiyo maana nzima ya huduma za mwendokasi?
- Kwanini utakuta mmekaa kabisa kituoni kwa mfano Morocco au Gerezani au Kivukoni au Kimara au Ubungo lakini Madereva wa haya mabasi huyaegesha kwa mbali kama vile wanatusikilizia na wakiona tu sasa abiria tumeshajazana katika hivyo Vituo tajwa na kila abiria ana mhemuko wa kupanda ndipo na wao huyawasha mabasi yao na kuyasogeza karibu ili tuanze kugombania kuingia ndani? Mheshimiwa Waziri Mkuu je huku kukimbizana na kugombania kuingia katika haya mabasi ndiyo maana nzima ya huduma ya mwendokasi?
- Kwanini wale WALINZI wao waliowaweka vituoni muda mwingi kama ni Wanaume utawakuta tu wameweka pembeni Virungu vyao huku wakijadili tena kwa kubishana mambo ya Simba na Yanga na kama ni Wanawake utawakuta kabisa wameegesha miguu yao katika vile vyuma au viti wanapiga soga tu za jana wamewachuna " mabuzi " wangapi na kazi kuwazungumzia akina Shilole na Wema huku abiria wengine wakipata taabu ya kujua mpangilio mzima wa usafiri na wakikosa msaada hadi sisi abiria wengine tuwasaidie kwa kuwaongoza?
- Mheshimwa Waziri Mkuu japo Mimi siyo " Mjuvi " wa masuala ya magari zaidi tu ya Baiskeli yangu hii ya Phoenix ila naomba hawa UDART wakujibu hivi haya mabasi ni kweli ni MAPYA? Nauliza tena waulize hao UDART hivi ni kweli haya mabasi yao ni MAPYA? Mheshimiwa hata kama sina utaalam wa magari ila ukiyasikia tu jinsi yanavyounguruma vibaya hutopata shida kuhisi kuwa pengine yote haya yametengenezwa Gereji za Kiwalani au Buguruni kwani yanakera na yanatupa shaka.
- Mheshimiwa Waziri Mkuu niulizie hao UDART kuwa ni kwanini Madereva wao hubadilishana kila baada ya Saa 8 wakati ruti zao ni fupi tu za Morocco - Gerezani, Morocco - Kivukoni, Morocco - Kimara, Kimara - Kivukoni, Kimara - Gerezani, Ubungo - Gerezani na Ubungo - Kivukoni halafu huku tena kuna mabasi yao mengi tunayaona yamepaki tu mule katika yard yao Jangwani. Hivi hawa Madereva wanaoingia mchana hawawezi wakapewa yale mabasi mengine yaliyomo mule ndani ili yaje yachukue abiria kwa uwingi wake na kusaidia kupunguza huu uhaba wa mabasi ambayo husababisha sasa sisi abiria kupambana kuyapanda hadi kupelekea wengine tunasukumana hadi kwa bahati mbaya unampiga Mtu kichwa katika purukushani na mkishapanda na kukaa mule ndani muda wote gari inatembea yule uliyempiga kichwa kwa bahati mbaya anakuangalia kwa hasira hadi unaiogopa hata safari yenyewe?