Mheshimiwa Rais katika DOWANS Tusidanganyane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Rais katika DOWANS Tusidanganyane

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kamanzi, Feb 7, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Heshima yako mheshimiwa Dr Dr Dr.

  Napenda kusemaulinitia moyo kidogo kwa kupata ujasiri wa kuzungumzia sakata la dowans. Hilo lastahili pongezi. Tatizo ni kwamba, umetumia siasa kujitetea.

  Ati umewaambia wanachama wako wa CCM kwamba hukulizungumzia kwasababu unapenda uhuru wa mahakama na kwamba watu wamekutusi kwa kudhani unahusika na DOWANS.

  Lakini Mheshimiwa Dr Dr Dr hivi nji lini umeanza kuheshimu uhuru wa mahakama? Hivi si wewe uliyewapa wakati mgumu mahakimu wakati wa kesi ya baba yako wa ndoa marehemu Ukiwaona Mzuzuri mpaka wakati wa kifo chake alikuwa mtu huru tu mitaani?

  Je, si wewe ambaye uliwahi kusema na nakunukuu, "yupo mtu anayegawa magari mekundu na anawaharibu mabinti, tunamjua na tutamshughulikia" na haukupita muda mzee wa kuusambaza Amatus Liumba aliwekwa ndani? Ama ulipata wapi uwezo wa kujua utamshughulikia wakati wewe sio hakimu? Japo simtetei Liumba kwa makosa mengine aliyofanya, lakini wewe uliona wapi mkuu wa personel (HR Director) akashitakiwa kwa kosa la kimahesabu? Halafu mbona hata ndugu wa Gavana Balali ambaye alikuwa ndie haswa muhusika mkuu wanakiri bado yupo hai?

  Hivi mheshimiwa Dr Dr Dr si wewe na serikali yako mlim-pressurize Chief Justice atupilie mbali uamuzi wa mahakama kuu ya kuruhusu mgombea binafsi katika uchaguzi wa mwaka jana?

  Eti mheshimiwa Dr Dr Dr, si wewe unayetajwa na mkurugenzi uliyemchagua mwenyewe Dr Hosea kuwa umempiga marufuku kuwafungulia mashtaka Mkapa na Sumaye kwa ufisadi wao? BAdo tu unasema unatunza uhuru wa mahakama?

  Hivi sio wewe mheshimiwa unayehusishwa moja kwa moja na kufungwa kwa Babu Sea na mwanae papii Kocha? Mheshimiwa Dr Dr Dr naona sasa unatuona WADANGANYIKA wote akili zetu hazina akili?

  Ushauri wangu ni kwamba badala ya kuukataa ukweli, waambie watanzania kuwa wewe, Rostam na Lowassa mwajua DOWANS ni yenu na sasa upepo wa Tunisia na Misri umekufanya upige breki kwenye hili.

  WADANGANYIKA ni wasahaulifu, ukiwaambia hivyo bado watakupenda vinginevyo unatuudhi sie wengine kwa kujifanya huijui DOWANS. Eti wamekutusi? Wewe ndio unatukana AKILI ZA WADANGANYIKA kwa kudhani unaweza kuwadanganya kila siku katika jambo lolote.
   
 2. m

  makongorosi Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia mambo yake mengi anayofanya Jk ni yale ya kujiona yeye mtoto wa mjini na kuiendesha nchi ki- mishen town ndiyo imetufikisha hapa kwenye Richmond/downs.
   
 3. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Mr. President wetu ni kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu, kuchukulia poa mambo wakati mambo yakiwa magumu. He has to change himself na serikali yake yote
   
Loading...