Mheshimiwa Lukuvi wizara yako inayo majipu ya muda mrefu, tumbua

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,611
Kipo kiwanja kimoja mbezi beach, ni cha mzee fulani mstaafu wa serikali ya awamu ya kwanza na ile ya pili.

Huyu mzee amehangaika hapo wizara ya ardhi tangu mwaka 1992 akijaribu kupata hati lakini anazungushwa kwa sababu kuna utapeli unaofanyika katika kufanya siku zipite, ili mwisho wa siku ashindwe kufuatilia na kiwanja kipewe mtu mwingine kwa sababu kipo sehemu nzuri karibu na barabara inayotokea kipita shoto cha maringo kuelekea njia panda ya white sands na Africana.

Kuna mtu mwingine ambaye ni hewa amepewa offer ya kiwanja hicho, hivyo mzee anashindwa kupewa hati eti mpaka rais aweze kuifuta offer aliyopewa huyo mtu hewa, ili ikibakia offer ya mzee ndipo aweze kupata uhalali wa kuomba hati.

Kinachokera sana ni kuona kuwa mzee huyu tangu 1992 amekuwa akikilipia kodi zote stahili na ushahidi wa risiti upo. Yaani kodi inapokelewa kwa mikono miwili lakini haki ya kuwa huru kutumia kile kinacholipiwa kodi, haipo!!.

Mzee kwa sasa ana zaidi ya miaka 82, imebidi vijana wake ndio wachukue mzigo wa "nenda rudi" isiyojulikana itaisha lini. Kila wanapoingia pale ardhi maafisa wanajibu kwamba suala la hicho kiwanja lipo juu ya uwezo wao na ni mpaka mheshimiwa rais atengue uhalali wa offer ya huyo mtu hewa. Vijana wakienda kutaka appointment na waziri, msaidizi wake anawarudisha ghorofa ya tatu kwenye ofisi maalum ya mambo ya revocation (utenguaji wa maamuzi ya awali).

Mheshimiwa William Lukuvi ulifanya kikao na wakazi wa kinondoni, mwaka jana, mwezi mmoja kabla ya uchaguzi, na ukachukua vielelezo vyote vya uhalali wa hicho kiwanja cha mbezi beach. Pia ulipelekewa ofisini kwako kopi za vielelezo hivyo na kuagiza ofisi ya kamishna ifanye kazi, lakini hakuna cha maana kinachofanyika.

Kwa heshima na taadhima mzee huyu anakuomba ulishughulikie suala hili ili nguvu aliyoitumia katika kuitumikia nchi hii akiwa mkufunzi mkuu wa vyuo vyote vya kilimo kuanzia miaka ya 60 mpaka miaka ya 90 mwanzoni, isipotee bure.

Mheshimiwa Lukuvi majipu unayo hapo hapo wizarani kwako, naamini upo uzembe wa makusudi ambao umechangia katika kushindwa kupatiwa suluhisho, kwenye hili suala la kiwanja cha mzee huyu.
 
Back
Top Bottom