Swahilian
JF-Expert Member
- Apr 28, 2009
- 591
- 66
Kwanza apewe heshima na utukufu Muumba wetu wa mbingu na ardhi, malaika na mitume na maandiko yao hali kadhalika sie wanadamu wafuatilizi.
Tulisubiri kipindi cha uchaguzi nacho kikaja kikatumika na baada chungu kikapika na Rais alikuja kupatikana, halafu wabunge na baadaye spika wa bunge, majaji, waziri mkuu na si punde baraza la mawaziri limetangazwa japo bado kutawazwa rasmi.
Kwa mtazamo wangu na tathmini yangu hafifu japo utendaji kazi wa baraza hilo jipya hatujaujua lakini nadhani ni kati ya mabaraza bora na Rais amejitahidi kupanga safu yenye mgawanyo mzuri wa kiumri, uzoefu na sifa.
Nimepata faraja hasa kutokana na uwepo wa sura mpya na za watu wachapakazi na hali kadhalika wale wazoefu waliobaki wanaonesha kufaa katika nafasi husika, nikipigia mfano uwepo wa Mh. J.P. Magufuli, Mh. S. Sitta.
Mh. S. Kawambwa, Mh. S.V. Nahodha na wengineo, nafkiri tunalo jipya la kutegemea kutoka kwao.
Mh. Kikwete amejaribu kutoa kazi kwa staili nzuri na nahisi ni vile wengi wetu tulipenda iwe..,. Yaani mupe huyu na huyo muruke.....
Itapendeza ikiwa malengo ya pamoja kama nchi yatatimizwa nao, na pale litokeapo tatizo wawe ni watu wa kulitafutia ufumbuzi wa haraka na wenye manufaa kwa nchi.
Tunawatakieni kazi njema na uadilifu katika nyadhifa hizo adhimu katika nchi.
Tumeaminishwa kwamba mnaweza na hivyo ni wajibu wenu kuthibitisha hilo.
''A luta continua''
Mungu Ibariki Tanzania....Mungu Ibariki Afrika.