Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, Mazingira, Mchungaji Natse

Aug 1, 2012
35
27

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WAKAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE MCH ISRAEL YOHANA NATSE (MB) AKIWASILISHABUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRAKWA MWAKA WA FEDHA 2015/2016

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9), ya Kanuni za Kudumu za BungeToleo la Mwaka 2013)



UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, Kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezeshakusimama mbele ya Bunge lako tukufu na kulihutubia Bunge pamoja na watanzania kwaujumla, Pili ninaishukuru Familia yangu kwa kunipa moyo na kunifanya niifanyekazi yangu ya Kibunge kwa ufanisi zaidi, Niwashukuru wananchi wote wa Jimbolangu la Karatu kwa kunipa ushirikiano mkubwa kwa kipindi chote cha miakamitano hadi sasa, Pia ninatoa pongezi zangu za dhati kwa Kiongozi wa KambiRasmi ya Upinzani Bungeni Mh Freeman A Mbowekwa kazi kubwa ambayo ameendelea kuifanya ndani na nje ya Bunge, watanzaniawanaona tumaini kubwa kutoka kwa upinzani, pia natoa pongezi kwa Viongozi wakuuwa vyama vinavyounda UKAWA, Wenyeviti na Makatibu Wakuu pamoja na sekretarietiya UKAWA, Kazi yao nzuri imeendelea kufuta machozi kwa watanzania wakiwa namatumaini ya kuuondoa utawala wa kifisadi wa CCM ifikapo October 2015 kwanimbadala wake ambao wamekuwa wakiomba kwa muda mrefu sasa umepatikana.Mheshimiwa Spika, Katika Ilani ya CCM ya Mwaka 2010 kifungu cha 34 kinachoainishamaswala ya Wanyamapori na Misitu, Ilani imeonesha Umuhimu wa wanyamapori namisitu unazidi kuongezeka siyo tu katika kuvutia watalii, bali pia katikakutunza mazingira. Katika kipindi chamiaka mitano ijayo (2010–2015), Serikali ya CCM itachukua hatuazifuatazo:- (a) Kuendelea kuelekeza nguvu zake katika kuhifadhi, kulinda,kuendeleza, kudumisha na kuvuna maliasili kwa manufaa ya Taifa letu, (b) Kuzipa serikali za mitaa nguvu zaidi na kuwawezesha wananchikumiliki na kunufaika na maliasili, (c) Kuongeza msukumo katika kuendeleza ufugaji wa nyuki kwa ajiliya kuzalisha asali na nta kibiashara, (d) Kuvutia wawekezaji katika kuanzisha viwanda vya kusindikaasali na nta, (e) Kuhimiza miji ianzishe bustani za ufugaji wa wanyamapori (zoos ) kwa maonyesho,(f) Kuweka utaratibu shirikishi wa upandaji wa miti, uvunaji naudhibiti wa moto. Ushirikishaji huoutakuwa wa sekta binafsi, NGOs na vijiji.


Mheshimiwa Spika
, Uharibifu wa mazingira ni tishio kwa maendeleo ya Taifa. Matumizi endelevu ya mazingira ni muhimu kwamaslahi ya kizazi cha sasa na kijacho,Ilani yao imeendelea kusema kuwa, Ili kuendeleza hifadhi ya mazingira, Serikali ya CCM itatekeleza yafuatayo:- (a) Kusimamia na kuendeleza mpango wa hifadhi ya mazingira katikamaeneo ya ardhi, bahari na ukanda wa pwani. (b) Kuendeleza kazi ya kuelimisha na kuhamasisha wananchi, ilikuimarisha utunzaji na hifadhi ya mazingira katika maeneo yao. (c) Kuendeleza kazi ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira katikamaeneo ya makazi, viwanda na mahoteli.

Mheshimiwa Spika
, Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali la Majukumu ya Wizara(Assignment of Ministerial Responsibilities Notice), la mwezi Januari, Mwaka 2011,majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais yameainishwa kama ifuatavyo:- Kuandaa nakusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Hifadhi ya Mazingira, Kufuatilia nakuratibu Shughuli za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(National Environment Management Council-NEMC). Aidha, kutatua changamotozinazohusiana na uharibifu wa Mazingira ili kuhakikisha matumizi endelevu yarasilimali na maliasili.

Mheshimiwa Spika, ukisoma katika Ilani ya CCM juu ya uhifadhi wa mazingira nchinina ukasoma pia katika mwongozo wa kiwizara katika majukumu ya ofisi ya Makamuwa Raisi Mazingira utaona kama upo mkakati wa kuhakikisha swala la kimazingiranchini linafanyiwa kazi kwa kuzingatia taaluma na weledi kuhakiki nchi inakuwasalama katika utunzaji wa mazingira na kuweza kuwezesha uchumi kukuaikizingatiwa kuwa yapo mahusiano kati ya mazingira na uchumi, mazingira naumaskini, lakini kiuhalisia utekelezaji wake umefanyika kwa kiwango kidogo mno.

Mheshimiwa Spika, Swala la uharibifu wa mazingira katika nchi zinazoendelea ni katiya sababu zinazofanya nchi hizo ziendelee kuwa maskini, UPO uhusiano mkubwakati ya mazingira na umaskini kwa maana kwamba, uharibifu wa mazingiraunachangia kuongezeka kwa umaskini na kwamba kadri hali ya umaskiniinavyoongezeka inasababisha uharibifu wa mazingira, kwa msingi huo umuhimu wakulinda na kuhifadhi mazingira nchini unachochewa zaidi na ukweli kwambamazingira ni mhimili wa sekta za uzalishaji kama vile kilimo, utalii, uvuvi namadini. Changamoto iliyopo ni kuhakikisha mazingira na maliasili za Tanzaniazinatumika katika njia endelevu kwa kuzingatia uwiano mzuri kati ya matumizi yamaliasili, hifadhi zake na uwezo wake wa kuendelea kutoa huduma, ili kusimamiamasuala ya hifadhi ya mazingira kwa ufanisi ni lazima kudhibiti shughuli za kibinadamuzinazoathiri mazingira, masuala ya kijamii na kiuchumi kama vile ongezeko lawatu, na shughuli za kiuchumi zinazoendana na matumizi yasiyo endelevu yamazingira zinazoweka shinikizo kubwa katika mazingira na kusababisha uharibifu.


UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2014/2015 NA MWELEKEO WA BAJETI2015/2016


Mheshimiwa Spika
, Katika taarifa ya waziri mbele ya kamati ya kudumu ya bunge yaArdhi Maliasili na Mazingira, imeonesha udhaifu katika utekelezaji wa Bajeti yamwaka 2014/2015, Kimsingi matokeo ya udhaifu yameonekana zaidi kwa athari zakimazingira ambazo zimeendelea kutokea nchini, lakini pia swala la fedha zamaendeleo katika uhifadhi wa mazingira bado halijawa kipaumbele kwa serikalihii ya sasa ya chama cha mapinduzi, na hili linajithibitisha kwa viwangoambavyo vinatengwa kwa miradi ya maendeleo, katika jumla ya shilingi Bilioni61.1 ambazo Bunge liliidhinisha ni kiasi cha jumla ya shilingi Bilioni 7.5 tuu ambazozilitengwa kwa miradi ya maendeleo katika Ofisi ya Makamu wa Raisi.

Mheshimiwa Spika
, Fedha zilizopokelewa na wizara kuanzia Tarehe 01 Julai, 2014hadi 31 Machi 2015 ilikua ni jumla ya shilingi Bilioni 36.3 fedha ambazo nitakribani nusu ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa mwaka mzima, huu ndio umekuwa utamaduni wa serikali hii yaCCM kudharau maazimio ya Bunge katika bajeti na kuonesha kutokuwajibika katikautekelezaji wa Bajeti kila mwaka. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshauri kwatakribani sasa miaka mitano mfululuzo juu ya nidhamu ya bajeti kwa serikalibila mafanikio yeyote. Kazi yetu kama UKAWA ni kusema kweli, Mwalimu Nyererekatika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE anasema ….'' Ukweli una tabia moja nzurisana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote nisawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa''…..mwisho wa kunukuu, hivyo basi jukumu letu ni kusema wazi pia kuwafahamishawatanzania iliyo kweli na kwa kuwa mwalimu anasema Ukweli haupendikupuuzwapuuzwa hata watanzania hawapendi kupuuzwapuuzwa na serikali yao, sasani wakati wa watanzania kufanya uamuzi sahihi kwa maslahi ya Taifa letu ifikapoOctoba 2015.

Mheshimiwa Spika
, Bajeti ya miradi ya maendeleo pekee ambayo iliidhinishwa naBunge ambayo imeainishwa katika kitabu cha Waziri cha taarifa kwa kamati yaBunge juu ya utekelezaji wa bajeti na makadirio ya bajeti ya mwaka 2015/2016,Fungu 31 Ofisi ya Makamu wa Rais Fedha za miradi ya maendeleo zilizotengwajumla ya shilingi Bilion 6.5 na fedha zilizokwisha tolewa kwa wizara hadikufikia mwezi machi 31,2015 ni jumla ya Shilingi Bilioni 2.2 sawa na asilimia33 ya bajeti nzima kwa mwaka, tafsiri ndogo ni kwamba hadi kufikia mwezi Machini asilimia 33 tuu ya fedha za Miradi ya maendeleo zilikuwa zimetolewa katikaofisi ya Rais. Tumejenga utamaduni wa kutotekeleza bajeti na mipango yetu kamaTaifa, na utamaduni huu umeasisiwa na chama cha mapinduzi kwa kuwa na ahadizisizo tekelezeka, pia kujenga utamaduni wa kuwalaghai wananchi kwa lugha tamuzisizo weza kutekelezwa na serikali.

Mheshimiwa Spika
, Utamaduni huu wa kutotekeleza ahadi na mipango ya serikalipasipo kuchukua hatua za kurekebisha,Taifa hili litaendelea kuwa maskinimilele, Mwandishi na Mchambuzi wa siasa na Profesa wa Uchumi Ndg Bryan Caplanwa Chuo Kikuu cha George Mason anasema, wanasiasa wengi hawatekelezi ahadi kwakuwa hakuna adhabu zinazochukuliwa kwa kushindwa kwao kutekeleza ahadi, lakinipia huwa hawaoni haja ya kutekeleza baada ya kushinda uchaguzi, Kimsingi anatoasuluhu kwa wapiga kura kuchukua hatua za kumwajibisha kiongozi wa aina hii, kwamujibu wa katiba yetu hakuna mahali ambapo wananchi wanayo haki ya kumwajibishakiongozi ambae hatimizi wajibu wake.

Mheshimiwa Spika
, Kimsingi Serikali hii haijawahi kufikia asilia mia zautekelezaji wa bajeti, inahitaji kupewa adhabu, tena adhabu kubwa hata yakutumikia kifungo cha maisha, ni wakati sasa watanzania kupima kati ya kupewaahadi hewa ambazo kamwe hazifikii utekelezaji wa kiwango hata cha asilimiaangalau hamsini, kwa nini sasa serikali isikiri mapungufu kiungwana na kutakakupumzika kwa hiari? Kwa nini watanzania sasa wasione haja ya kuwapumzisha kwania njema ya mustakabali wa taifa letu?

MABADILIKO YA TABIANCHI


Mheshimiwa Spika
, Kwa mara kadhaa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwaikiishauri serikali katika maswala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Tanzania ni moja ya nchi ambayo tunashuhudia matokeoya mabadilko ya tabia nchi, hususani uwepo wa ukame wa muda mrefu unaojirudiarudia ambao unaambatana na athari kubwa katika kilimo, usafirishaji, nishati,biashara na sekta mbalimbali za uchumi kwa jamii, Karibuni tumeona athari zamafuriko katika nchi yetu ambapo wananchi wamepoteza maisha yao, lakini baadhiya maeneo wananchi wamekosa maji kwa matumizi ya kila siku kutokana na ukame,ni mambo ya kimazingira yenye kuhitaji majibu ya kimazingira.

Mheshimiwa Spika,
Wakati wananchi wakipotezamaisha katika maafa ya kimafuriko ambazo ni athari za kimazingira, serikalibado ipo usingizini kwa kutokuwa na majibu ya kuliona tatizo la kimazingira nakuchukua hatua za kunusuru roho za watanzania maskini wanaopoteza maisha kilasiku kutokana na mafuriko, furaha ya serikali hii ya CCM ni kutenga bajeti kilamwaka za maafa na kuwadhulumu waathirika wa maafa yatokeapo bila kuwa nasuluhisho ambalo ni la kudumu kwa kupunguza au kuondoa kabisa athari za majangaya aina hii kutokea nchini, wakati yakitokea hayo kilimo katika maeneo husikakinadorora au kusimama kabisa, mifugo mingi na wanyama wa porini wanakufa kwakukosa chakula katika maeneo yenye ukamena kukosa na maji, na wakati mwingine kusombwa na mkondo wa maji yaliyofurika.

Mheshimiwa Spika
, upo usemi usemao ‘The devil lies in the details'yaani mzimu upo katika maandishi, ukisoma katika majibu ya serikali kwa kamatiya bunge. Serikali inasema, ….'' Kampuni ya DART (Dar Rapid Transport) ilipewahati ya Mazingira Tarehe 30/06/2009 yenye namba ya usajili EC/EIS/146 kwa ajili ya ujenzi wa kituo chamabasi yaendayo kasi eneo la Jangwani'' serikali imeendelea tena kusema '''….. DARTimetekeleza masharti mengi iliyopewa ikiwemo; kufanya ujenzi katika eneolinaloruhusiwa tu, kupanua miundombinu kuruhusu maji ya mvua kupita kwa urahisi,….Hoja hapa ni jehali iliyojitokeza hivi karibunihadi kupelekea kufungwa kwa barabara ya jangwani ndio utekelezaji wa mashartiwa kampuni ya DART kutoka kwa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira?Serikali iwaambie watanzania ukweli juu ya athari hizi za uzembe na kuwepo kwamiradi iliyotanguliza maslahi ya watu binafsi na sio watanzania ambao wanaambuliakupoteza maisha yao.

Mheshimiwa Spika,
mwaka 2010 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliitahadharishaserikali kwa kuonesha Baadhi ya viashiria vya uwepo wa mabadiliko ya tabianchikatika nchi yetu, ambavyo ni pamoja navifo vya mifugo vilivyokithiri kutokana na ukame kwa wakati huo, hasa maeneo yakaskazini mwa Tanzania kama vile Monduli na Longido wakati wastani wa mvua kwamwaka ukiwa umepungua kwa asilimia 25, Pia Utokeaji wa mafuriko unaosababishwana ongezeko la mvua zisizotabirika katika maeneo makame yasiyo na mimea nahivyo maji kutiririka kwa kasi zaidi na kusababisha madhara maeneoyanapoelekea, Pia Ongezeko la joto duniani linasababisha ongezeko hatari nautokeaji wa magonjwa mapya kwa mamilioni ya watu, hasa yale yanayoenezwa navimelea na bacteria kwa maeneo ambayo kwa asili hayakuwepo, Tafiti mbalimbalizilizohusu mwelekeo wa joto wa muda mrefu katika ziwa Viktoria,Tanganyika naNyasa zikionesha ongezeko la joto katikamaji ya kina kirefu kati ya nyuzi za sentigredi 0.2 mpaka 0.7 kuanzia mwanzonimwa miaka ya 1900( Taarifa za Serikaliya mwaka 2009).

Mheshimiwa Spika, Matokeo ya serikaliinayojiita sikivu ni haya yanayotokea sasa Kwa asili tulizoea watu kuhama aukuwa wakimbizi kutokana na mapigano ya vita, lakini kwa sasa wahamiaji wengiwanatokana na mabadiliko ya tabianchi na kwa lugha iliyozoeleka ni Wakimbizi waKimazingira "environmental refugees", Kimsingi hili limekuwa tatizo sana kwanikutokana na watu kuhama maeneo yao ya asili kwa ajili ya ukweli kwamba maeneohayo hayawezi tena kuwezesha kuishi kwao na hivyo inawalazimu kuhamia maeneomengine ili kuendelea na maisha yao jambo ambalo limetokea sana kwa wafugaji na wakulima naathari zake sasa ni mauaji kati ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeishauri sana serikali hii yaCCM kwa muda mrefu sasa, Kwa umri tuu inatosha kusema CCM sasa imekuwa mtumzima kama sio mzee, Waswahili wanasema…''Mbwa Mzee hafunzwi adabu''… Kimsingiwatanzania wameona kilichoitwa udhaifu wa Viongozi wa sasa, udhaifu wa CCM naUzembe wa Bunge katika kuiisimamia serikali, ikiwa leo ni mwaka wa mwisho waserikali hii ya CCM tutakuwa tukimpigia mbuzi gitaa au kumfunza mbwa mzeeadabu, Nitoe wito kwa watanzania, sasa tukatae vifo vya wananchi maskini katikamafuriko kwani hakuna hata kiongozi mmoja aliyekufa kwa mafuriko zaidi ya watumaskini tuu kufa, au kwa kuwa viongozi hawapati adha hii ndio maana hawaonihaja ya kutafuta suluhu ya majanga ya aina hii? Serikali hii imechoka sasa,haijui wajibu wake na wapi inawajibika, ni vema sasa tukafikiri kuwa naserikali inayowajibika kwa wananchi, inayoishi na kutambua wajibu wake kwaumma. October 25 ndio siku maalumu kwetu watanzania kubadilisha mfumo wauongozi wa nchi yetu na kuweka viongozi sahihi watakaoondoa kero za wananchi,na UKAWA ndio jawabu la watanzania.

UBOVU WA MIUNDOMBINU YAMAJI TAKA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Mheshimiwa Spika, Jiji la Dar es Salaam ni moja ya majiji machafu katika nchi zaAfrica Mashariki,miundombunu ya maji taka imekua mibovu katika maeneo mengi yajiji na hivyo kusababisha, kwanza harufu mbaya katika jiji la Dar es Salaamambayo ni hatari kwa afya ya binadamu, pili kusababisha maji kushindwa kusafiriwakati wa mvua na kusababisha mafuriko ambayo yamekua yakileta maafa katikajiji hususani katika maeneo ya mabondeni, wakati wananchi wakipata matatizo yakufikiwa na mafuriko katika maeneo ya mabondeni serikali bado imeshindwa kutoamisaada ya haraka kwa wahanga ikiwa ni wajibu wa serikali kuwasaidia wananchiwakipata matatizo, wakati yote haya yakitokea nchini, Serikali pamoja na kuonamadhara haya yakitokea na wananchi kuendelea kupata adha ya uchafu katikamaeneo yao pamoja na kusababisha magonjwa ya mlipuko, bado serikali hii ya CCMinaona ni pafyumu katika jiji na kubaki bila kuchukua hatua stahiki.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inawataka wakazi wa jiji la Dares Salaam, sasa si wakati wa kuomba omba msaada kwa Serikali kwani ni takribanimfululizo wa miaka kumi sasa ya Utawala wa Mh.Kikwete mambo haya yameshindwakupata suluhu ndani ya serikali yake, Hivyo ni ukweli kwamba mazingira bora yakiafya katika jiji la Dar es Salaam yatapatikana kwa kuwa na serikaliinayowajibika kwa wananchi na kutambua kero za wananchi waliowaweka madarakani- Jibu ni UKAWA ifikapo 25 Oct 2015.

UJENZI HOLELA MIJINI


Mheshimiwa Spika
, katika Bunge hili mara kadhaa tumehoji juu ya ujenzi holelanchini,Ni ukweli kwamba Miradi yote hapa nchini kabla ya kuanza utekelezajiwake ni lazima kwanza ufanyiwe tathmini (Environmental Impact Assessment-EIA)na kupata cheti cha kuuwezesha uendelee kama ulivyokuwa umepangwa, na tukasemakatika bunge hili lakini cha kushangazamiradi ambayo inamilikiwa na Serikali imekuwa haipati cheti cha Tathmini nahivyo imekuwa ikileta usumbufu mkubwa sana kwa wananchi au watumiaji na hivyo kuwa kero kwa Serikali yenyewe nakero kwa wananchi. Mheshimiwa Spika, katika nadharia hiyo, hivi karibuni katika jiji la Dar es Salaamyalipotokea mafuriko barabara ya jangwani ya mabasi yaendayo kasi ilijaa majina kufungwa, ukweli ni kwamba, Ofisi yaKampuni inayojenga miundombinu ya mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (Strabag)ilipewa Hati na Serikali ya kumiliki eneo hilo la Jangwani na hivyo tayariwamejenga ofisi zao za Kudumu. Mbali nakuhoji utolewaji wa hati kwa Kampuni hiyo,tunahoji Je tathmini ya mazingira ilifanyika?na kwamatokeo ya sasa hata kama tathmini ilifanyika ni kwa vipi au upo mkakati ganiwa kuondoa kero zinazojitokeza sasa kwa wananchi?Kitendo cha kujenga hapo nikurudisha maji kwa maeneo jirani na kuzidisha maafa. Aidha, kama Kampuni hiyoimepewa hati miliki ni kwanini waliokuwa wamejenga eneo hilo walihamishwa nakupelekwa nje ya mji? Yote haya yalihojiwa na serikali hii ya CCM ilitoa majibu mepesi na kujisifu kuwa ni serikalisikivu ilhali ikiendelea kufurahia mafuriko na maafa ya wananchi maskini.

UCHAFU KATIKA HALMASHAURI


Mheshimiwa Spika
, Katika swala la usafiwa mazingira kwa kudhibiti utupaji taka ovyo pamoja na halmashauri kusimamiaswala la usafi katika halmashauri zao, swala hili limeendelea kuwa ni tatizokatika halmashauri nyingi nchini kwa kushindwa kuweka miji safi wakati wote nakusimamia utupaji taka ovyo, Mkurugenzi wa halmashauri ndiye mwenye wajibu wakuhakikisha halmashauri yake inakuwa safi, kwa bahati mbaya sana swala la usafilimekuwa likifanywa kama kete ya kisiasa na wakurugenzi kutumika kufanya siasaza vyama, Katika halmashauri kadhaa nchini wananchi wameanza kuchangishwa fedhaza ushuru wa taka kwa maamuzi ya mkurugenzi ili kugombanisha wananchi na vyamavya upinzani vyenye mamlaka katika maeneo husika, Mfano katika Hamshauri ya Mjiwa Njombe kwa kuwa CHADEMA ilishinda kiti cha Diwani mwaka 2014 February, kablaya hapo Swala la usafi katika kata ya Njombe Mjini lilikuwa chini yaMkurugenzi, mara tuu baada ya ushindi wa CHADEMA swala hilo limekuwa likikwepwana Mkurugenzi na kutupiwa mzigo kwa Diwani wa kata ya Njombe Mjini swala ambalolimeufanya Mji wa Njombe kuwa mchafu tena mji wa Spika wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mkuu wa Mhimili wa Bunge, na Jimbo lake likiwa chafu kupindukia, Lakinipia hali ikaendelea kuwa mbaya mara tuu baada ya CCM kushindwa katika uchaguziwa serikali za mitaa mwezi Desemba 2014 na kuangushwa na CHADEMA,Kimsingi hukuni kutumika kwa watendaji wa serikali kisiasa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,inawataka watendaji wa serikali kuacha kutumika kisiasa na kufanya kazi zao zautendaji kwa kufuata sheria hususani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji waNjombe.

Mheshimiwa Spika
, Katika gazeti laMwananchi Mwezi Agosti 16, 2013 lilinukuuhabari ya Serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko yote ya plastiki ilikutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko hiyo kwenye mazingira,tamkohilo lilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisiya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa wakati huo Dk Terezya Huvisa alisema wametoa muda wa miezi mitano kuanzia mwezi huowa Agosti hadi Januari mwaka 2014 na itakapofika Februari Mosi wataanza msakorasmi kwa watakao endelea kuuza aina hiyo ya mifuko, wakati serikali ikichukuauamuzi huo bado iliendelea kuruhusu uwepo wa aina hiyo ya mifuko katika sokondani ya nchi, Kutokana na kukithiri kwauchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mifuko laini ya plastiki na serikalikushindwa hadi sasa kulishughulikia swala hili zaidi ya kufanya sanaa ya kudaihatua zinachukuliwa, Huu ni ushahidi tosha kuwa serikali ya CCM imechoka,serikali ambayo haiwezi kusimamia matamko yake yenyewe.

Mheshimiwa Spika
, Katika taarifa yautekelezaji wa mipango na bajeti kwa mwaka 2014/2015 inayoonesha maagizo yakamati ya bunge na utekelezaji wake, moja ya maagizo ni pamoja na kutekelezaagizo lake kusimamia kanuni ya kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki mapemaiwezekanavyo ili kuondoa tatizo sugu la uchafuzi wa mazingira ambao unatia aibunchi, na ukisoma katika majibu ya serikali inasema bado inaendelea kutoa elimukwa wadau juu ya umuhimu wa kutumia mifuko mbadala ambapo kanuni zimekuwepotangu mwaka 2006 hadi sasa ni takribani miaka kumi hakuna utekelezaji wowote wakuzuia utengenezwaji na uuzwaji wa aina hii ya mifuko ya plastiki, Huu niushuhuda mwingine wa kuchoka kwa serikali, Serikali ijifunze kutoka Rwanda Mjiwa Kigali hakuna kuingia na mfuko wa plastiki, ukifika uwanja wa ndege waKigali unaacha aina yote ya mifuko ya plastiki ndipo uupate kibali cha kuingiakatika mji huo, kama imezekana Rwanda kwa nini sisi tushindwe? Ndio manatunadharauliwa na wenzetu kwa kushindwa kufanya mambo madogo kwa manufaa yanchi yetu.

Mheshimiwa Spika
, ni vema sasawatanzania wakatambua ukweli wa serikali hii ya chama cha mapinduzi, serikaliiliyo na mipango mingi isiyo tekelezeka, mipango yenye mvuto kwa watanzania,hatuwezi kufikia malengo ya kufanya mazingira yetu kuwa masafi kwa kuwa namipango ambayo hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa katika kutekeleza kwa vitendona kuishi bali kwa kauli tuu katika maandishi, natoa wito kwa watanzania wote kutaka mazingira safi ifikapoOctober 2015 kwa kuing'oa CCM na UKAWA kuchukua Usukani wa Kuliongoza Taifahili ili tuweze kunufaika na rasilimali tulizonazo kwani hii ni nchi ya Asalina Maziwa.

UJENZI WA NYUMBA KATIKA KINGO ZA MITO NA FUKWE ZA BAHARI


Mheshimiwa Spika, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika mchango wake wahotuba ya Waziri Mkuu juu ya makadirio ya mapato na matumizi alizungumza juu yamasterplan ya mji wa Dar es Salaam, msigi wa hoja yake ni pamoja na kuwepo kwaathari za kimazingira pale mji unapokuwa na majengo yaliyojegwa kiholelea bilakuzingatia mipango na kuona athari zinazoweza kujitokeza kimazingira, KamaBunge na Kambi ya Upinzani tumekuwa tukishauri juu ya utoaji wa vibali vyaujenzi katika maeneo ya kingo za mito na fukwe za bahari kuwa si mwema kwamazingira, Ukisoma taarifa ya wizara kwa kamati juu ya utekelezaji wa maazimioya bunge na maagizo ya kamati, serikali inasema imeshindwa kubomoa nyumaNa.2019/2020 iliyopo Kawe kutokana na pingamizi lililopo mahakamani, Hoja hapasi kuingilia uhuru wa mahakama, siku zote tunasema serikali ya CCM ni dhaifu naukweli huu hauwezi kufutwa tuu kwa kusema si dhaifu au kwa kusema hii ni siasa,ukweli huu utabaki kuwa ukweli kwanza Nyumba hii imepewa Namba na serikali hiiya CCM kwa kutambua kuwa ni Nyumba halali, Pili serikali hii ya CCM ndio ilitoakibali cha Ujenzi wa Nyumba hii, Tatu serikali hii ya CCM ndio ilipima viwanjaeneo hilo la Nyumba na kuvitoa kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika
, TUJISAHIHISHE, Watanzania TUJISAHIHISHE, Mwalimu Aliwahi kusema''…. Hatulazimiki kuendelea na uongozi huu mbovu wa chama na serikali…..'' kwawakati huo tukiwa ndani ya mfumo wa chama kimoja, akitaka kufanyike mabadilikoya uongozi wa chama na serikali, mpaka leo chama hichohicho hakijabadilikakimfumo wala kiuongozi, sasa ni wakati wetu wa kuamua kutoendelea na uongozi huumbovu wa chama na serikali yake, yale ambayo tumekuwa tukishauri sasatukayafanyie kazi wenyewe kwa maslahi ya taifa letu. UKAWA Ndio Tumaini Letu.

UWEZESHWAJI WA IDARA YA MAZINGIRA NA BARAZA (NEMC)


Mheshimiwa Spika, Katika moja ya maagizo ya kamati ya bunge kwa serikali ni pamojana kuwezesha kifedha idara ya mazingira na baraza la mazingira ili liwezekufanya kazi kwa ufanisi ya uhifadhi wa mazingira, katika hoja mahususi yakamati, kamati ilitaka serikali kupitia wizara ya fedha ione umuhimu wa kuipatiaidara ya mazingira na baraza – NEMC Fungu la pekee ili kiasi cha fedhakinachotengwa kwa ajili ya idara ya Mazingira kijulikane wazi kwa kuwa fedhazinazoidhinishwa kwa ajili ya matumizi mengineyo kwa fungu 31 hujumuisha mgaowa kibajeti wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Katika majibu ya serikaliinasema swala hili lipo kwenye mchakato wa kuangalia uwezekano wa kufuataushauri huu wa kamati.

Mheshimiwa Spika, Majibu haya ya serikali kwa kawaida ya Bunge hili yamekuwayakitolewa na serikali hii ya CCM kwa maana ya utimizaji wa wajibu wa kujibumaswali na si kutoa suluhu ya matatizo katika utendaji, huu ndio mwaka wakukamilisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya miaka mitano, kwa ushauri wa miakamitano mfululizo hatutegemei jipya, na kama leo malaika atawashukia serikalihii ya CCM ikabadilika, basi wazingatie ushauri tuliokwisha utoa hapo nyuma nawatanzania wanaweza kuona uungwana wa serikali hii na kuwasamehe kwa uzembe wakutofanya hayo kwa miaka yote iliyopita.

Mheshimiwa Spika
, Uchimbaji wa madini endelevuni muhimu ili kulinda mazingira na kuleta maendeleo endelevu,ni muhimu kutambuana kutumia njia bora za utunzaji mazingira katika uchimbaji madini, Sekta ya madini hasa uchimbaji mkubwahapa Tanzania ni sekta inayokua kwa kasi na inayochangia kwa kiasi kikubwakatika uchumi wa nchi, Shughuli za uchimbaji madini husababisha uharibifu wamazingira, Baraza la Taifala Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limepewa mamlaka ya kusimamia shughuli zautunzaji wa mazingira nchini chini ya sheria No. 20 ya Utunzaji na Usimamizi waMazingira (EMA) ya mwaka 2004 Ibara ya 17 (1) na 25, Kumekuwa nauchafuzi wa mazingira katika migodi mbalimbali nchini kwa kutupa taka ovyo,kusambaza kemikali ambazo ni sumu kwa uhai wa viumbe hai na binadamu paleinaposambazwa katika vyanzo vya maji na ardhi, na ni dhahiri yakitokea katikamigodi ya Nyamongo, Bulyankhulu, Mererani, Geita Gold Mine michache kwakuitaja. Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ingependa kuwataka wananchi wanaoishipembezoni katika migodi ambao wamekuwa wakipata madhara kutokana na uchafuzi wamazingira, waone ni kipindi cha mpito kwao na hali hiyo itakoma mara tuu baadaya utawala huu kukoma mwezi Oktoba 2015. Tukiwa madarakani kama UKAWA tutalipameno Baraza la Mazingira Nchini ili kuweza kudhibiti swala la uchafuzi wamazingira katika migodi ili wananchi na viumbe visiendelee kuathirika na sumuna athari za kimazigira migodini.

SEKTANDOGO YA MISITU NA NYUKI

MheshimiwaSpika, Kwa mara kadhaa Kambi rasmi ya UpinzaniBungeni imeendelea kuishauri serikali juu ya uimarishaji wa sekta ndogo yamisitu na Nyuki, kwa mujibu wa kitabu cha ''Transforming the informal Sector,How to overcome the Challenges'' (ESAURP). Kinaainisha takwimu zaukubwa wa eneo la misitu Tanzania ikiwa ni hekta million 33.5 za misitu ambayoni sawa na asilimia 38% ya eneo la ardhi yote nchini,pia kinaainisha mchangomkubwa unaoweza tolewa na sekta ya misitu katika uchumi kwa kuirasimisha sektahiyo kuweza kuweka mazingira bora ya ajira kwa wananchi ikizingatiwa shughuliza misitu ni moja ya chanzo kikubwa cha kipato kwa wananchi wa maeneo yavijijini.

MheshimiwaSpika
, na kwa mujibu wa taarifa za TRAFFIC 2007zinaanisha kuwa ni asilimia 4 tu ya mazao ya misitu huvunwa kihalali naasilimia 96 huvunwa bila kupata vibali rasmi na serikali kukosa mapato kwauvunaji mkubwa unaofanywa kutokana na kutorasimisha biashara ya mazao ya misituna kuwa na utaratibu ulio rasmi wa kufuatailia uvunaji wa mazao haya ya misitu,Kambi rasmi ya Upinzanibungeni katika bunge hili tuliitaka serikali kuona umuhimu wa kuona asilimia kubwaya wananchi wanaotegemea bidhaa za misitu kuendesha maisha yao kiuchumi.

MheshimiwaSpika, katika hizo asilimia 96 ambazo huvunwabila ya kupata kibali, kuna miti ambayo inavunwa kwa ajili ya uchomaji wa mkaa,kwa mujibu wa tafiti zilizokwishafanyika, sekta ya mkaa huingiza zaidi ya dolamilioni mia sita na hamsini sawa na zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwakana kuajiri mamilioni ya watanzania hususani waishio vijijini. Ni wazi kuwasekta hii imeachwa bila mikakati na sheria unganifu. Tanzania tunapaswakujifunza kutoka Brazil ambayo inazalisha mkaa asilimia 11% na Tanzaniapekee inazalisha asilimia 3% ya mkaa wote unaozalishwa duniani. Sekta hiiikiwekewa mikakati mizuri ya makusudi itaweza kuzalisha mkaa kwa njia ya kisasahuku ikipunguza hewa ya ukaa na kuifanya sekta hii kuwa endelevu.


MheshimiwaSpika
, Brazil huzalisha asilimia 11% ya mkaawote unaozalishwa duniani. Kwenye miaka ya 1990 asilimia 60.3% ya uzalishaji wamkaa Brazil ulifanywa kutoka kwenye uvunwaji wa misitu ya asili baadaye mkakatiwa makusudi ulifanywa ili mkaa uzalishwe kutoka katika misitu ya kupandwa.Ingawa matumizi ya mkaa nchini Brazil ni kwa ajili ya viwanda vya kufua chuma.Jambo la msingi ni kwamba uvunaji wa mkaa kwa misitu asili ilipungua kwa asilimia82% kati ya mwaka 1989 hadi 1996. Makampuni makubwa yalipewa jukumu la kupandamiti, kuzalisha na kusambaza mkaa kwa ajili ya kuifanya iwe endelevu. Hapanchini upo uwezekano kabisa wa kuboresha ubora wa mkaa kwa kuwajengea uwezowazalishaji na kuifanya kuwa sekta rasmi huku tukiendelea kuboresha mazingirayetu. Hali hii ikiwezekana itasaidia sana katika kuboresha na kuhifadhi misitu nchini.Ikiwa sekta ya mkaaitafanywa kuwa endelevu ni dhahiri kuwa athari zitokanazo na mkaa kamavile uharibifu wa mazingira, hewa ya ukaa iharibuyo tabia nchi na gesi yaozone kupunguzwa kwa kiasi kikubwa. Kambi rasmi ya upinzaniiilishataka serikali kuanzisha mikakatiya makusudi ya kuweza kuifanya sekta ya mkaa iwe sekta rasmi na endelevu kwanini nishati tegemewa na asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania, Pia,mchango wake wa zaidi ya shilingi trilioni moja katika ukuaji wa pato la Taifani mkubwa ukilinganisha na mazao mengine yatokanayo na misitu hivyo haiwezikupuuzwa na kuachwa bila mkakati wowote.MheshimiwaSpika,Badala ya kuacha serikali iendeleekupoteza mapato kupitia watendaji katika halmashauri ambao wamekua wakitozafaini kwa bidhaa za misitu na mapato yake kutoingizwa katika mfuko wa serikali,na ukweli ni kwamba hata tusipo rasimisha mkaa utaendelea kutumika naitaendelea kuwa ni biashara ya wakubwa tu, na kama taifa misitu itaendelekakukatwa na mapato tutaendelea kuyakosa. Kwani ukweli ni kwamba hatuna chanzombadala cha nishati kwa watanzania wa kipato cha chini. Hivyo basi, ni wakatimuafaka kwa serikali kurasimisha biashara za misitu na kuwafanya wananchiwaendelee kufanya kwa utaratibu maalumu na kuweza kuipa serikali sehemu yamapato hayo.

MheshimiwaSpika
, iliwahi kusemwa hapa Bungeni na MchMsigwa Mbunge wa Iringa Mjini kuwa mwanamazingira mmoja duniani aliwahi kusemahivi, naomba kumnukuu Mh Msigwa tena kama alivyonukuu pia ,"To be poor and be without trees, is to be the most starved humanbeing in the world", Hakuishia hapo na akasema tena "To be poorand have trees, is to be completely rich in ways that money can never buy" mwishowa kunukuu. MheshimiwaSpika, tatizo la uharibifu wa misitu badolimeendelea kuwepo nchini na kuathiri juhudi za utunzaji wa misitu nchini,itakumbukwa mnamo tarehe 19 April 2013, ilizungumzwa ndani ya bunge hili kuwa magogoyamekuwa yakisafirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es Salaam katikamaswali kwa mawaziri huku tatizo la madawati kwa wanafunzi likiwa halijapatasuluhu?.


MheshimiwaSpika
, Kambi Rasmi ya Upinzani inaliangaliaswala hili kwa maono ya mbali zaidi, lipo tatizo kubwa la uhaba wa madawatinchini kwa watoto wetu mashuleni, na ufisadi mkubwa ukifanyika katika sekta yamisitu, jambo kubwa hapa ni kusimamia sera na taratibu rasmi wa serikali katikakulinda misitu nchini, itakumbukwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 4tu ya misitu yetu ambayo huvunwa kwa vibali halali na asilimia 96 ni kwa njiaisiyo halali, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama chawaandishi wa habari za mazingira (JET)- "Biashara haramu ya mazao yamisitu yaisumbua Serikali".

MheshimiwaSpika, tumekuwa tukishauri sana kuwa kutokanana ubadhirifu huo katika sekta ya misitu serikali inakosa mapato yatokanayo nauvunaji wa misitu, pia wananchi wa pembezoni mwa misitu wanashindwa kujikwamuakatika umaskini, kwa kurejea taarifa ya shirika la mazingira la TRAFFIC yamwaka 2007 ilitoa takwimu zilizoonesha hasara inayoipata serikali kwa mwakakutokana na biashara haramu ya misitu ikiwa ni shilingi bilioni 75, pamoja nakuonesha hasara hiyo ya mapato ya serikali pia ilieleza uhusikaji wa viongoziwa serikali katika ubadhirifu huo.

MheshimiwaSpika
,Mh.Waziri Mkuu, moja ya vipaumbele vyakena ofisi yake ni Ufugaji Nyuki hata sasa amekuwa maarufu kwa jina la ''Bwana Nyuki'', lakini bado sekta hii ipo nyuma ikilinganishwa na matamshi ya kuonesha kuwepo kwa juhudi kubwa katika kuiwezesha sekta hiikukua na kuwa na tija kwa uchumi wa nchi na jamii husika, swala la kipaumbelechochote cha serikali si kufanya kwa malengo ya kutangaza nia kwa wananchi kwamaslahi ya kisiasa, kuna haja ya serikali kuhakiki inatekeleza vipaumbele kwakuonesha utendaji halisi hasa kuifanya sekta ya nyuki kuwa na manufaa kwawananchi wanaoingia katika biashara hiyo, takwimu zinazotolewa na taarifa zaserikali juu ya kuiwezesha sekta ya ufugaji nyuki si za kuridhisha kutokana narasilimali nyuki tulionayo nchini.

MheshimiwaSpika, Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni inatoarai kwa wananachi sasa Kuchagua viongoziwakweli viongozi wenye uwezo wa kutekeleza ahadi kwa watanzania, hii ndioitakuwa dawa kwa matatizo yaliyodumu kwa zaidi ya miaka hamsini chini yautawala wa CCM kama tutaamua kwa pamoja kuweka madarakani vyama mbadala vyenyemaono mapya yaani UKAWA.

HITIMISHO.

MheshimiwaSpika
, Nimalize kwa kumshukuru MheshimiwaFreeman Aikael Mbowe(Mb), Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na MwenyekitiMwenza wa UKAWA, kwa kuniamini na kuniteua kuongoza Wizara hii kama WaziriKivuli Mazingira Ofisi ya Rais, Pia Wenyeviti wenza wa UKAWA Mh Prof. IbrahimuLipumba, Mh Emmanuel Makaidi, na Mh James Mbatia (Mb), kwa kazi kubwawanayoifanya ambayo imeshaanza kuzaa matunda kwa watanzania na hivyo ifikapo MweziOktoba 25, 2015 watakapo fanya uamuzi wa kweli kwani tayari wametambua UKAWAndio tumaini lao pekee. Mwenyezi Mungu Ibariki UKAWA, Mwenyezi Mungu Ibariki TANZANIA,Ameni.




___________________________________



Mch. Israel Y.Natse (Mb)

Msemaji Mkuu Kambi Rasmi yaUpinzani - Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, 2015
 
Back
Top Bottom