Koala
Member
- Aug 28, 2011
- 97
- 107
Mheshimiwa kwa naomba nikupe pole kwa kazi kubwa unayoifanya kutetea maslahi ya sisi wananchi wanyonge wa jimbo lako la Kibamba. Kwa kweli mkuu binafsi nakuunga mkono sana hasa katika suala la maji na kubomolewa kwa nyumba kuanzia pale stop over mpaka Kiluvya. Ila mkuu kuna kero moja kubwa sana ambayo umeisahau au unajaribu kuvaa miwani ya mbao na kuweka pamba masikioni.
Hii bara bara ya Mbezi kwa Msuguri inayokwenda mpaka Msingwa na kuunga Maramba mawili kwa kweli imekuwa kero kubwa. Hivi sasa bajaji wanatulipisha shilingi 1000, boda boda 2000. Sasa mkuu kwa maisha haya yalivyobana tutaweza kweli kumudu maisha? Mkuu naomba usikie kilio hiki. Najua Meya wa Ubungo uko karibu nae tunaomba umwambie aje angalau apitishe greda tu likwangue yale mashimo maana ni kero kubwa.
Naomba usikie kilio chetu, tumechoka.