Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Mheshimiwa huku kwetu jana na juzi tumetafakali sana hatimae tukakumbuka kuwa;
Wewe, kwa kauli yako tu umeifanya barabara ya ubungo kibangu inapitika tena kwa kiwango cha lami.
Wewe, kwa kauli yako tu umeifanya barabara ya moroko mwenge kupanuliwa.
Tena wewe kwa kauli yako tu umeifanya barabara ya airport Mwanza imejengwa kwa kiwango bora kabisa.
Na kadharika na kadharika!
Kwa sababu hiyo mheshimiwa; pamoja na kwamba tunatambua ukubwa wa nchi yetu,
Sisi wakazi wa Mwanagati Kitunda Ilala Dsm tuko chini ya miguu yako, tunakuomba,
Utujengee barabara ya lami pana toka banana kupitia Mwanagati kuunganisha na njia panda ya Buza.
Mhe Rais, kwanini iwe ni wewe?
Kwa sababu ya mateso makubwa ya usafiri tunayopitia hasa nyakati hizi za mvua, tumetafakari sana na kugundua kuwa; hayupo mtu mwingine anayeweza kutusaidia mapema kwa hili isipokuwa wewe.
Na kwa kuwa sisi tunaamini katika wepesi wako wa kushughurikia mambo; ndiyo maana tumeamua kuleta ombi letu kwako mhe rais wetu mpendwa.
Sisi tunaamini kwamba; kwa mamlaka yako, wewe ukiamua barabara hii ijengwe, itajengwa tu!
Mhe Rais, endapo utakubali barabara hii ijengwe, kando na kutusaidia sana sisi wakazi wa eneo hili pia itapunguza msongamano wa magari katika barabara ya Nyerere.
Ukikumbuka kuwa misafara yote ya waheshimiwa kutoka airport inachangia sana foleni mhe rais.
Hivyo mchepuko wa banana mpaka Mwanagati buza utakuwa ni Mbadala pekee pindi misafara hiyo inapochanganya.
Mungu akubariki na kukufanikisha katika kazi zako zote za ujenzi wa taifa.