Mhe.Rais Magufuli kwanza nikupongeze kwa kazi ngumu ya kuliongoza Taifa letu. Umeanza kazi yako ya Urais vizuri hasa katika kukusanya mapato ya serikali,kuthibiti matumizi ya hovyo ya serikali na kurejesha nidhamu katika utumishi wa Umma.
Pamoja na pongezi hizo kuna maeneo umeanza vibaya! Maeneo hayo ni kama ifuatavyo; Mosi, Sukari, suala la sukari ni suala nyeti na linamgusa kila mtu! Ni suala lenye utajiri mkubwa na ulaghai/ujanjaujanja mwingi! Nia yako ni nzuri katika kutaka kuidhibiti, ila approach yako si nzuri,maana approach za long term umezifanya kwa short term.
Huwezi kudhibiti uingizaji wa bidhaa bila kwanza kujenga uwezo mzuri wa uzalishaji wa ndani! Angalia sasa kwa muda mfupi umetusabishia hasara kubwa kupitia sukari! Kwa mfano kama ilikuwa tunywe sukari tani laki moja kwa bilioni 200 yaani tshs.2000 @kg,sasa tunakunywa tani laki moja kwa bilioni 300 yaani Tshs.3000@kg. Unaenda kutusababishia hasara ya bilioni 100 sisi Wananchi wako ndani ya muda mfupi sana!
Wataalam wako wa uchumi wako wapi na kwanini kama walikupa ushauri kwenye hili usiwatumbue? Pili,eneo la viwanda na biashara bado hueleweki vizuri! Waziri wa Viwanda na biashara ndugu Mwijage ni mzungumzaji sana lakini ukimsikiliza vizuri hamna kitu ni ngonjera tu! Sasa nakuuliza Mhe.Rais vipi mnataka kuirudisha serikali kwenye biashara 100%?,mmeshajiuliza kwa nini tulishindwa huko nyuma!?
Eti mnajivunia kuchukua 100% za General tyre! Mhe.Rais usipoenda kwa sera nzuri ya Serikali ya PPP hautofanikisha kamwe kujenga nchi ya "Magufuli ya Viwanda".Matatizo yetu sugu ni "Management & Technology"!
Tatu. Umesimamisha matumizi ya serikali badala ya kudhibiti! Mhe.Rais Magufuli hali ni ngumu sana mtaani,hakuna fedha mtaani! Wanasema eti Rais Magufuli anakusanya fedha anafungia Hazina kusubiri Budget yake!
Mimi nasema hapana! Achia fedha tumalizie Budget ya Kikwete! Kwani ilipitishwa na Bunge letu! Mwisho,umeanza kwa kujenga nidhamu ya woga na unafiki kwa watumishi na wataalam wetu! Kila mtu sasa anaogopa kutumbuliwa.
Hawakwambii ukweli sasa ni kurukaruka tu! Eti DC anasimama sasa hivi anasema sukari iuzwe kwa bei elekezi! Ni aibu hawajui hata kanuni ndogo za uchumi, demand & supply in relation to prices.Mhe.Rais Magufuli chukua hatua vinginevyo hata wanaofurahia kasi yako ya utumbuaji wa majipu watakugeuka muda si mrefu.