Mhe Rais JPM usiruhusu kosa hili lijirudie.

fbetwel

Member
May 27, 2013
36
19
Binafsi nampongeza rais kwa hatua anazochukua za haraka kutibu gonjwa la nchi hii. Anachofanya ni sawa na yale aliyofanya mwl Nyerere, kuondoa unyonyaji dhidi ya wanyonge.
Mwl alchukua hatua hizi pia,ikiwemo kuwafukuza fisi wa taifa hili.
Lkn ukiwa mchunga kondoo walozungukwa na fisi, ukawalinda kondoo wako pasipo kuweka kinga ya ulinzi pale uondokapo, wale fisi wakirudi na njaa mpya watakula hadi mifupa ya kondoo wako.
Mwl hakutuachia kinga ya katiba imara dhidi ya fisi aliowatumbua enz za utawala wake na hatimae baada ya kustaaf tu walionyesha dalili kwamba aliwapa njaa na wanaham ya kututafuna kwa hamu.
Kuna haja ya mhe. Rais, magufuli kubadili KATIBA kabla hajastaaf, hawa fisi akistaaf watarudi kwa kasi ya ajabu, asije rudia kosa alilolifanya mzee wetu mwl Nyerere.
Katiba tu ndio urithi bora kwa taifa hili.
 
Hill ni gumu mkuu.Na unapozungumzia Katiba bora 'ni lazima' arejee kwenye Rasimu ya pili ya Tume ya Katiba jambo ambalo kijani na njano hawataki kulisikia.Hapo JPM yuko mtegoni na hawezi kuthubutu.
 
Vyama vingi vilivyopo madarakani huogopa sana mambo ya katiba.sidhani kama hoja hii ikafanikiwa kwa wakati huu
 
CCM hawawez kukubali tubadishe katiba hivi nyinyi manaimani na magufuli abadilishe katiba mbona ccm bado ni ileile tusijidanganye hapa mpaka tukubali kupoteza maisha coz democrasia imefeli
 
Naona hii sio agenda ya mh.rais, agenda ni kutumbua majipu(very sad)

sasa, kutumbua majipu si ndo huko anakoongelea mtoa uzi hapo juu, kuwa anafanya vyema na aendelee kusawazsha kila baya,,,,,,,,,,au mi ndo sijaelewa?
 
Binafsi nampongeza rais kwa hatua anazochukua za haraka kutibu gonjwa la nchi hii. Anachofanya ni sawa na yale aliyofanya mwl Nyerere, kuondoa unyonyaji dhidi ya wanyonge.
Mwl alchukua hatua hizi pia,ikiwemo kuwafukuza fisi wa taifa hili.
Lkn ukiwa mchunga kondoo walozungukwa na fisi, ukawalinda kondoo wako pasipo kuweka kinga ya ulinzi pale uondokapo, wale fisi wakirudi na njaa mpya watakula hadi mifupa ya kondoo wako.
Mwl hakutuachia kinga ya katiba imara dhidi ya fisi aliowatumbua enz za utawala wake na hatimae baada ya kustaaf tu walionyesha dalili kwamba aliwapa njaa na wanaham ya kututafuna kwa hamu.
Kuna haja ya mhe. Rais, magufuli kubadili KATIBA kabla hajastaaf, hawa fisi akistaaf watarudi kwa kasi ya ajabu, asije rudia kosa alilolifanya mzee wetu mwl Nyerere.
Katiba tu ndio urithi bora kwa taifa hili.
...............................................................................................................................................................................kikwete alijalibu kutaka kuweka kinga ambayo ingelinda sana fisi wake ambao hawakutosheka na nyama walioipata na walikuwa tayali ata kula mifupa na ngozi yake kuiuza ughaibuni ili itengeneze suti ambazo wangezivaa wakati wakiendelea kuzifaid nyama zilizobaki,lakini alizidiwa na nguvu ya kondoo wachache ila walio na nguvu thabiti,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom