Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli azindua rasmi Ujenzi wa Gati Bandari ya Mtwara Leo!!

TPA

Member
Sep 28, 2016
49
71
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameweka rasmi jiwe la msingi kwenye Bandari ya Mtwara, kuashiria kuanza kwa Ujenzi wa Gati Jipya Na. 2 katika Bandari hiyo litakalokuwa na urefu wa mita 350!

Yafuatayo ni Matukio mbalimbali katika picha kuhusiana na uwekaji huo wa jiwe la msingi, uliofanyika leo katika Bandari ya Mtwara.

17155264_631226693750169_94696419874161548_n.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizindua rasmi jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Gati Na. 2 Bandari ya Mtwara leo.

16996317_631226757083496_7657104505827046719_n.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Wadau mbalimbali wakati hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara leo.

17098376_631226787083493_5071120862034006034_n.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akitoa maelezo kwa Mhe. Rais kuhusiana na mradi wa ujenzi wa Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara leo.

17155314_631226910416814_2675736078150988363_n.jpg

Mhe. Rais akishuhudia, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko na Mwakilishi kutoka Kampuni itakayojenga Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara wakitia saini makubaliano ya kuanza kwa ujenzi huo leo.

17021765_631227460416759_4888080480728306062_n.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko na Mwakilishi kutoka Kampuni itakayojenga Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara wakionesha hati za makubaliano mbele ya Wageni Waalikwa na Wadau Mbalimbali.

17155452_631227550416750_4626250920379452755_n.jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Francis Michael wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Gati Na. 2 Bandari ya Mtwara

17098209_631227613750077_3139845839201944352_n.jpg

Baadhi ya Wageni Waalikwa waliohudhuria tukio la utiaji saini na uwekeaji jiwe la msingi la ujenzi wa Gati Na. 2 katika Bandari ya Mtwara.

17155452_631227550416750_4626250920379452755_n.jpg

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, Prof. Ignas Rubaratuka na Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Francis Michael wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Gati Na. 2 Bandari ya Mtwara

17021780_631227937083378_4696262159128876659_n.jpg

Baadhi ya Watumishi wa TPA kutoka katika Bandari mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa ujenzi wa Gati Na. 2 leo.

17021699_631227977083374_2611347001798732503_n.jpg

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Dkt. Francis Michael (wanne kulia) akiwa na Wajumbe wengine wa Bodi hiyo kutoka kulia ni Bw. Aziz Kilonge, Bw. Jaffer Machano, Bi. Jayne Nyimbo, Dkt. Jabir Kuwe na Bw. Renatus Mkinga wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Gati Na. 2 Bandari ya Mtwara

17021657_631228083750030_902450201411590564_n.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (MB), akisoma hotuba yake wakati wa hafla hiyo.

17103573_631228343750004_8410657790505475724_n.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya TPA.
 
Nasikia Bandari ya Mtwara ina kina kirefu cha asili kwa nini TPA msitenge bajeti iwe kubwa kwa ajili ya kuhudumia nchi jirani kama kasakazini mwa Msumbiji,Malawi,Zambia, CONGO na nyenginezo?
 
Nasikia Bandari ya Mtwara ina kina kirefu cha asili kwa nini TPA msitenge bajeti iwe kubwa kwa ajili ya kuhudumia nchi jirani kama kasakazini mwa Msumbiji,Malawi,Zambia, CONGO na nyenginezo?
Selfishness ya wenye maamuzi ndo inaiweka TZ hapa ilipo.
 
Back
Top Bottom