Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni nakusalimu!
Naomba nikuulize jambo kuhusu msiba/kifo cha aliyekuwa Katibu wa Madereva Tanzania. Sote tunajua kuwa Marehemu huyu alikuwa mpigadebe mkubwa wa Dr. Magufuli na CCM kwa ujumla kwenye kampeni za uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. Alishiriki vyema na hata 'kuwasemea' madereva kwenye mkutano wa CCM pale katika Viwanja vya Jangwani.
Mara baada ya kifo chake, Mhe. Paul Makonda umejitokeza mitandaoni na hata kwenye televisheni ya EA TV ukisema kuwa umeviagiza vyombo vya usalama vya Wilaya ya Kinondoni kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha kifo cha Katibu huyo. Nilikuona jana kwenye kipindi cha EA TV (Kurasa) ukisema kuwa uchunguzi umeshaanza ukihusisha madaktari na hata watu wa usalama.
Sasa Mhe. Paul Makonda, kwanini ni kwa msiba huu tu? Kuna ujumbe gani unaotaka kuutuma kwa ndugu, jamaa, marafiki, madereva wenzake na watanzania kwa ujumla juu ya msiba huu? Mara ngapi umewahi kuagiza uchunguzi kwenye misiba ya viongozi wa taasisi za kijamii?