Ni Mara ya Pili kuja kimatembezi mkoani Arusha, mara ya kwanza nilifika mwaka 2001 na wakati huo nilifanikiwa kutembelea baadhi ya maeneo machache ya jimbo la Arumeru wakati tunafanya utafiti wa zao la kahawa.
Katika pitapita zangu katika jimbo la Arumeru naomba nikiri ipo kazi kubwa imefanywa na Nassary kama mbunge iukilinganisha na historia ya watangulizi wake.
Ni jimbo ambalo miundombinu ya barabara imejengwa hadi kijijini yaani barabara za kupanda vijiji vya mlimani kama Leguruki, Doombo, Nkwalua, akeri na kwenye hifadhi ya mlima Meru zinapitika kwa gari pamoja na ukubwa wa milima iliyopo pamoja na udongo tifutifu uliopo.
Nimetembele Miroroni sehemu zilizokuwa kame naona barabara zinapitika na maji yanapatika, nilipofika kijijini miroroni kwa mara ya kwanza palikuwa pakame na watu walikuwa wanatumia punda kwenda kutafuta maji kwa zaidi ya masaa kumi Leo kwa kiasi flani tatizo limepungu.
Tumepita Buguni kuelekea mirereni napo barabara ni nzuri japo hali ya Maji siyo nzuri, hii yote imenifanya nitambue uwezo wa kiutawala alionao Bw.Nasari pamoja na udogo alionao na pia kasikashi anazopata kutoka kwa watawala bado ameonyesha njia.
Uwepo wa Nasari Arumeru umewafanya wapinzani wake pia kupigana usiku na mchana kuleta maendeleo jimboni humu wakidhani wataweza kumwondoa madarakani kirahisi, mfano mzuri ni ujenzi wa kituo cha polisi Tengeru nasikia kilijengwa kwa nguvu ya maasimu wake kabla ya uchaguzi wa 2015 lakini maasimu hao waligonga mwamba.
Wameru wanajisifia ujasiri wao toka enzi za ukoloni wakimtolea mfano Marehemu Japhet Krilo anayeelezwa kuwa aliwahi kusafiri kwenda umoja wa mataifa kuomba Uhuru wa wana Meru lakini alikwama baada ya MHE.Mwalimu JK Nyerere kufika UN akiwa na hoja ya Uhuru wa Tanganyika ambayo Meru ipo ndani yake.
Nimefuatilia pia nguvu iliyopo Meru ya vijana na wazee kufanya kazi, Elimu ipo juu na katika kutembea kwangu sijaona nyumba ya Tembe bali zipo nyumba za mbao na nyumba za tofali zilizoezekwa kwa bati, hii ni tofauti na Mwaka 2001 na moja nilipofika humu na kukuta muamko wa Elimu upo chini sana na pia ujenzi wa nyumba zilizoezekwa kwa nyasi ukiwa umetapakaa maeneo mengi yakiwemo ya miroroni na Ching'ori.
Nimpongeze Nasari kwa kuwaleta wana Meru pamoja, kwa uvumilivu alionao hasa anapokumbana na nguvu ya dola pamoja na maasimu wake.
Kuhusu huduma ya Afya nimefanikiwa kuona maeneo mengi yakiwa na vituo vya afya ila Mhe.Nasari unapaswa kuangalia upya huduma zinazotolewa na wahudumu wa afya katika jimbo laki,tembelea vituo vya afya ikiwezekana weka mkakati wa kupata madawa ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu ya watoa huduma hapo utakuwa umefanya wanameru kunufaika na vituo vya afya ulivyojenga na vilivyojengwa na wananchi wako.
Yapo majimbo mengi nchini viongozi wamekaa miaka mingi lakini hakuna chochote unachoona wamekifanya, tembelea majimbo yote ya Dodoma ikiwemo Dodoma mjini ujionee umaskini ulivyo kisiri na hakuna huduma ya Maji wala afya iliyoimarika,majimbo ya Lindi, Mtwara, Tabora, Rukwa,Simiyu,Katavi,Geita,nk bado ule ukongwe wa wawatawala kukaa majimboni miaka 15 hadi 30 hauonekani ukibadilisha chochote.
Hivyo ni vyema kumpongeza huyu bwana mdogo kwa udhubutu wake wakuwaletea wananchi wake maendeleo.Nimpongeze kwa dhati ya moyo wangu kwa kuendeleza na kusimamia mapambano dhidi ya mabepari waliojimilikisha Ardhi Arumeru jambo ambao awali tuliaminishwa kuwa ni uvunjifu wa amani na kwamba mashamba hayo siyo Mali ya wameru ila kwa sasa watu wale wale waliokuwa wanampinga kuanzia bungeni hadi jimboni ndio wa kwanza kututangazia kuwa tumefanikiwa kuyarejesha Mashamba hayo kwa wananchi.Unatufundisha kutokukata tamaa katika kupigania haki hata kama utafungwa au kuteswa lakini ipo siku nafasi ya vita uliyopigana itaonekana.
NAVUTIWA SANA NA MAENDELEO YA ARUMERU HASA BAADA YA UTAWALA WA KIJANA HUYU, NINGEPENDA AWE MBUNGE WA JIMBO LANGU JAPO KWA AWAMU MOJA ILA NAAMINI HAITOWEZEKANA.