Mhe Mansoor alipochangia kwenye Kongamano la nafasi ya Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe Mansoor alipochangia kwenye Kongamano la nafasi ya Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Oct 8, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=3][/h]


  [​IMG]

  Mh Mansoor Yussuf Himid amewataka baadhi ya watu kutokuwa wepesi kwa kuwanyooshea vidole wenzao kwa sasa ni wakati wa kuzungumza kweli tena bila ya uwoga hasa katika mustakbali wa wazanzibar na nchi yao.

  Amesema wanaosimama na kusema hadharani kuwa mkiutaka msiutake muungano ndio huu huu kuwa wanakosea kwani hakuna mwenye haki ya kumlazimisha mtu juu ya anachokitaka mwenyewe.
  Iweje leo baadhi ya viongozi wawatishe wananchi juu ya mustakbali wa nchi yao

  Amewataka Wazanzibari kutokukubali kurudishwa walipotoka kwa sasa ni kwenda mbele na sio kurudi tena nyuma na amewaomba viongozi wenzake kuwa ni mabalozi juu ya hili kufikisha ujumbe kwa wengine wasiojua nini cha kufanya kwa sasa juu ya nchi yao ili waweze kuungana na wazanzibari wanaotaka kupumua na muungano huu.

  Pia amesema yeye haoni tatizo kwa mwananchi kutoa maoni yake anayoyataka juu ya muungano anaoutaka mwenyewe.

  Amewataka wananchi kutokuvunjika moyo na wajitokeze kwa wingi sana kutoa maoni yao wakati wa tume ya kukusanya maoni itakapopita waende kwa wingi sana kwenye mchakato wa kutoa maoni muda utakapofika ili waweze kuikomboa Zanzibar yao.

  Stori kwa hisani ya Hamed Mazrui via Face book
   
 2. Kitulo

  Kitulo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 2,225
  Likes Received: 2,357
  Trophy Points: 280
  Wazanzibar wengi hawautaki muungano hilo halina ubishi,vilevile ni wao wenyewe ndiyo wanaoweza kuuvunja muungano na kamwe wasitegemee watanganyika wawavunjie muungano ,sasa wafanye yafuatayo waungane wote bila kujali vyama vya siasa wamueleze rais Shein na viongozi wengine wakuu kwamba hawautaki muungano,kwa sababu kama rais Shein akiukataa muungano sidhani kama rais Kikwete ataulazimisha pia wasishiriki kwenye kutoa maoni ya katiba mpya kwa sababu hiyo ni katiba ya Taifa la Tanzania ambalo hawalitaki,wawashauri viongozi wao waliopo kwenye serikali ya muungano wajitoe na warudi Zanzibar akiwemo makamu wa rais,waache kuchukua vitambulisho vya NIDA (kwa sababu ni vya Tanzania),wabunge wao waache kushiriki bunge la muungano, ndugu zangu anzeni kufanya hayo kwani ndio mwanzo wa kujiondoa kwenye muungano.
   
Loading...