Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Leo ni siku ya 104 ya utendaji kazi wa rais wangu Magufuli (sina namna hata kama sikumchagua). Kazi kubwa aliyoifanya mpaka sasa ni kutumbua majipu tu, mzee kasitisha shughuli zingine zote yeye yuko busy na majipu.
Na watanzania wenzangu walio wengi wamefunga midomo, wanacheka kimoyomoyo rais wao anatumbua majipu. Hii kwao ni burudani tosha.
Na kwa namna nijuavyo mimi Tanzania yangu ina majipu mengi kwelikweli, yaani safari ya siku 104 ya rais wangu ya utumbuaji majipu bado haiwezi kubadilisha chochote na kwa kuwa rais wangu ana nia ya dhati ya kuhakikisha majipu yanatumbuliwa basi inaweza kuchukua zaidi ya miaka yake ya dhamana ya kuongoza aliyopewa ili kumaliza majipu hayo.
Watanzania wanaoishi katika nchi yangu wamesahau kabisa shida zao. Gharama ya sukari, mafuta, pembejeo za ujenzi na kilimo, si hoja tena mbele ya wapumbavu wenzangu wanaoishi katika nchi yangu.
Wako tayari sukari kununua kilo kwa sh 4000, chumvi sh 1000, kilo moja ya nyama sh 12000, mafuta ya taa lita sh 6000 maana rais wao kipenzi yuko busy na majipu. Sisemi haya kwamba ndivyo yalivyo ila nabashiri tu. Pia nalinganisha na uwezo wa kufikiri wa watanzania wenzangu.
Mtaani huko husemi kitu kuhusu rais wangu, utapigwa mawe. Asante rais wangu maana mtego wako umeweka pazuri utavua samaki wengi.
Hata usipofanya kitu nina hakika 2020 watakuchagua kwa kishindo. Watanzania wameridhishwa na kasi yako ya utumbuaji majipu.
By mbunge nje ya bunge (nawaza tu)