Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Wakati wahenga wakisema sheria ni msumeno, wataalamu wa sheria na falsafa ihusuyo haki waliweka bayana kwamba hakuna aliyeko juu ya sheria katika nchi inayoongozwa kwa sheria.
Katika kumbukumbu zangu napata kurejea baadhi ya hoja kuhusiana na baadhi ya makosa makubwa yaliyofanywa na Mhe. Mkapa enzi akiwa madarakani. Pia kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na wadadisi wa mambo ya kisiasa walieleza kwamba Mhe. Mkapa alimfuata nyumbani kwao Chato Mhe. Rais Magufuli kumsihi agombee kwa imani kwamba angemtunza tofauti na Mhe.Lowassa aliyeonekana kunuia kulipiza kisasi kwa kufumua mfumo na kuwawajibisha vigogo wote.
Vimeo vya Mhe. Mkapa vilivyotajwa ni:
Mkapa anahusishwa na umiliki wa mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kupitia kampuni yake ya ANBEN anayomiliki na mkewe, Anna ikiwa miongoni mwa makampuni matano yaliyoingia ubia na kampuni ya TanPower Resources Company Limited.
Mkapa, kupitia TanPower Resources Limited, anahusishwa na dhamana ya serikali ya kupata mkopo wa Sh. 17.7 bilioni kutoka CRDB Bank kwa ajili ya kuendeleza mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira.
Kwanza, inadaiwa kuwa Mkapa alimiliki kampuni akiwa bado rais (ANBEN 1998) wa nchi na hivyo atakuwa alitumia nafasi yake kujinufaisha binafsi na kampuni yake.
Pili, kwa kuwa alikuwa bado madarakani na kwa kuwa uamuzi wa kuuza Kiwira ulifanyika ndani ya Baraza la Mawaziri aliloliongoza, basi uamuzi huo ulikuwa wa upendeleo kwa kampuni yake.
Tatu, hata waziri aliyejenga hoja mbele ya baraza la mawaziri, Daniel Yona ametokea kuwa mshirika katika umilikaji wa mgodi huo, jambo ambalo haliendani na utawala bora.
Nne, mkataba wa kampuni ya Mkapa kuuza umeme kwa Tanesco ulifungwa Mkapa akiwa madarakani (Septemba 2005), jambo linaloonyesha upendeleo kwa kampuni yake na utovu wa utawala bora.
Miaka mitatu iliyopita serikali iliahidi kuurudisha mgodi wa makaa ya mawe mikononi mwa serikali jambo ambalo halijafanyika mpaka sasa licha ya kwamba vijana wengi wanahitaji ajira ukiacha mahitaji ya nishati ya umeme nyanda za juu kusini.
Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanajaribu kuongazia hatua atakazozichukua Mhe. Magufuli katika kuviondoa vimeo vya Mhe. Mkapa ikiwemo kupitia upya mikataba ya ubinafsishaji ili kuvirudisha mikononi mwa wananchi viwanda walivyopewa wawekezaji feki waliovigeuza magofu.
Swali linakuja, je muda bado au ndo tusamehe na kusahau kuhusu vimeo hivyo?