Mhe. Asumpta Nshama Nshunju Umetusaliti Wana Nkenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Asumpta Nshama Nshunju Umetusaliti Wana Nkenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by POLITIBURO, Apr 22, 2012.

 1. POLITIBURO

  POLITIBURO Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndg zangu wana JF na Wananchi wa Jimbo la Nkenge nawasalimu wote. Jimbo la Nkenge liko katika wilaya ya Missenyi, mkoa wa Kagera. Wilaya ya Missenyi ni changa na wananchi wa jimbo la Nkenge ni masikini hukikabilia na kipato duni, magonjwa ya mazao, maedeleo duni ya sekta ya elimu nk. Hali ya maendeleo iliyopo siyo zao la mbunge wa sasa au aliyepita! Kwa sasa mbunge wa Jimbo la Nkenge ni Asumpta Nshama Nshunju. Mhe huyu ni mbunge tangu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na aliupata ubunge baada ya DR Kamala kushindwa kuwajibika na kuwaletea maendeleo wana Nkenge pamoja na kushindwa kwa miaka 10 kutekeleza ahadi alizozitoa achilia mbali kuwatukana wapiga kura wake. Asumpta alitoa ahadi kedekede lakini kubwa zaidi ni kushirikiana na wananchi na kuwaletea maendeleo. Sasa ni wazi hakuna dalili ya utekelezaji wa lolote. Pia sisi wana Nkenge tunaamini maendeleo hayawezi kuja huku fedha na rasilimali za taifa zinaliwa na wachache ambao Mhe Asumpta haoneshi dalili au kuamka kupambana na mafisadi hao achilia mbali kushilikiana na wazalendo wanaoonekana kuchukizwa na ubadhilifu wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka yao. Mhe ameshindwa kuthubutu, amekosa hari ya kupambana wakati akiwa na silaha za kupambana na adui mafisadi. Kwa hilo sioni kama ana chembe ya jitihada za kuwaletea wananchi wa Nkenge maendeleo. Mimi naona ameamua mwenyewe kuuvua utu na uzalendo na amechagua kuwaunga mkono mafisadi. Kwa hiyo Mhe Asumpta ameamua kwa hiari yake kutokushirikiana na wapiga kura wake wanaishi kwenye umasikini uliotopea. Kwa kushindwa ama kusimamia au kushiriki kuunga mkono jambo hili la msingi ambalo siyo la kiitikadi naona ni usaliti kwa wana Nkenge na nchi yetu kwa ujumla. Mimi nawaomba wana Nkenge wote mlione hili, amkeni, jadilini hali inayoendelea jimboni. Kumbuka hizi sio zama za kusema heri enzi za fulani bali ni wakati muafaka wa kutafakari pamoja cha kufanya ili kunusuru jimbo letu na maendeleo. Naomba kutoa hoja!
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Ukichagua Mbunge wa CCM ujue ukejisaliti mwenyewe kabla hata haujasalitiwa na mbunge. Kama ameshindwa jambo dogo kabisa kama la kutia saini ya kukataa wizi wa mali ya umma wa wapambe wa Pinda unadhani ataweza kuandika proposal ya mradi wa maendeleo? Imekula kwenu mazima
   
 3. M

  Moony JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nshunju hawezi kusaini, mtu wa 'system'
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,185
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  yuko karibu na rostam, na kale kaunafiki kake ka kupiga magoti akiomba kura, Aondolewe na peoples powa huyu
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama unawakilishwa na huyu Asumpat Nshana basi nakupa pole. Mama mipasho imemjaa, na jazba nyingi. Na kila akipata nafasi ya kuongea zake ni kutoa hoja za kukandamiza CHADEMA. Tafuteni mgombea mwingine kwa 2015!
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mlimchagua wakati mnajua anaishi nje ya jimbo na mkoa wenu ili awasaidie nini?! Hata hivyo hakuna mbaya, simliongwa tshirt za njano/kijani,pilau na gongo nyie mkatoa kura?!
   
 7. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,185
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  sijawahi kumwona akiongea kwani mtoro bungeni, kweli yule hasara tupu, apigwe chini huyu 2015! Harakati zianzie kiziba hadi mtukula na minziro mpaka bubale watu waubiliwe ukombozi kwa nguvu ya umma jimbo likombolewe
   
Loading...