Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi asimamishwa kazi kwa kutoa malipo hewa

WENYELE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,426
1,431
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Frank Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani kulipa posho ya chakula kwa watu ambao si askari.



Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki anasimamishwa kazi kwa kufanya malipo ya kiasi cha sh. 305,820,000 kama posho ya chakula kwa watu ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.

Meja Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Kijeshi anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration allowance’ ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.

Meja Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo tangu leo tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma zinazomkabili.

Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa na Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi imebainika kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili kufanikisha malipo hayo hewa.
 
Napongeza juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kupambana na ufisadi kwa watumishi wa umma. Nataka niwajulishe kwamba hata hivyo yaliyofanywa na mhasibu huyo inaweza kuchukuliwa kama ni cha mtoto.

Wapo waliopiga mihela ile mbaya yake. Hebu angalia kisa hiki kilichopo Chuo cha Ufundi Arusha.

Kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2014/15 kiasi cha TZS 320,000,000/= fedha kwa ajili ya mafunzo viwandani zilitumika kama malipo hewa.

Mishahara ya wafanyakazi 25 walioajiriwa na Chuo Januari 2014 kiasi cha TZS 30,000,000/= zilitokomea zilitumika kama malipo hewa.

Kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2014/15 miradi hewa ya ujenzi chuoni ililipwa wastani wa TZS 400,000,000/= na hivyo kuwa malipo hewa.

Kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2014/15 yalilipwa malipo hewa kiasi cha TZS 250,000,000/= kwa ajili ya miradi ya ujenzi kupitia akaunti ya chuo inayojulikana kama ATC-PCB.

Ukarabati na upanuzi wa jengo la Utawala, unakadiriwa kulipa malipo hewa kiasi cha TZS 300, 000,000/=

Ujenzi wa jengo la madarasa lijulikanalo kama jengo la Ujenzi na Umwagiliaji linakadiriwa kulipa malipo hewa kiasi cha TZS 1,500,000,000/=. Kadhalika kutoka katika mradi huu, zaidi ya matofali 20,000 yalichukuliwa na Uongozi kwa matumizi binafsi.

Fedha ya msaada kiasi cha TZS 300,000,000/= kwa ajili ya kuendeleza shamba la Oljoro kwa kiasi kikubwa fedha hizi zilifanya kazi hewa na kupelekea kuwa malipo hewa.

Kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2015/16 kiasi cha wastani wa TZS 300,000,000/= fedha zinazokatwa kutoka mishahara ya wafanyakazi kwa ajili ya kodi ya nyumba fedha zilizodaiwa kutumika kwa ajili ya ukarabati wa nyumba. Fedha yote hiyo imegeuzwa kuwa malipo hewa.

Kwa wastani, zaidi ya TZS billioni 3.5 zimetumika kama malipo hewa katika kipindi cha kati ya mwaka 2011/12 mpaka 2015/16, Chuo cha Ufundi Arusha
 
We Mrangi kwani hiyo isue ya Lugumi ina ugumu gani??
Watu si wanaanzia mbali kwa kunyata, kwani ukimvizia swala unakurupuka??
Hizo sarakasi tu,ishu ya lugumi haitotokea kuguswa....maana Kuna Ike familiaa na mzee mziimaa ndani....na Yule ig....
Yule former shoe shiner boshen tu.....
Ishu ya lugumi lbda ukawa ingie madarakani ndy itamalizwa
 
Hizo sarakasi tu,ishu ya lugumi haitotokea kuguswa....maana Kuna Ike familiaa na mzee mziimaa ndani....na Yule ig....
Yule former shoe shiner boshen tu.....
Ishu ya lugumi lbda ukawa ingie madarakani ndy itamalizwa
KWELI INSHU YA LUGUMI HAITATOKEA KUGUSWA NI KAMA YA RICHMOND,LABDA UKAWA WAKINGIA MADARAKA WATAANZA NA RICHMOND
 
Back
Top Bottom