Mhasibu halmashauri ya Kwimba ni jipu la muda mrefu

Mhasibu halmashauri ya Kwimba ni jipu la muda mrefu

mandago shululu

Senior Member
Joined
Mar 24, 2013
Posts
125
Reaction score
37
Halmashauri ya Wilaya ya kwimba ni Wilaya kongwe kati ya Wilaya za Mkoa wa Mwanza,lakini cha kushangaza ni Wilaya ya Mwisho kimaendeleo kati ya Wilaya zilizo Mkoa wa Mwanza.

Tatizo kubwa lililopo ni aina ya wakuu wa Idara waliopo Kwimba kushilikiana na uongozi wa juu wa Wilaya.

Pamoja na kila Idara kuwa na Mapungufu lakini Idara ya fedha indio uti wa mgongo wa Halmashauri na ndio inayoyovuja kwa asilimia kubwa ikiongozwa na Mhasibu wa Halmashauri.

ikumbukwe kwamba Mhasibu aliyepo kwimba alikataliwa Halmashauri X na kuletwa Kwimba.Anafanya kazi kwa kiburi na kujinufaisha yeye mwenyewe.

Mpaka imefikia hatua ametenga watu wake ambao wanamkusanyia Pesa za ushuru na kumpelekea mfukoni.

Kwenye Idara yake ameshatenga Mhasibu X ambaye huwa anaongea na baadhi ya Wahe Madiwani kila kabla ya balaa kuwaweka sawa in any case of emergency, hela zinachotwa hapo hapo Halmashauri wanapigwa Madiwani.

Mpaka sasa Halmashauri ya kwimba kuna jumla ya vitabu 315 ya Mapato vimeshapotea lakini kwa taarifa za ndani imeswmekana kwamba vimechomwa moto ili kuficha baadhi ya ubadhirifu uliopo.

Kwa hali hiyo Widhara husika kama wanataka kujiridhisha na Bali hii wafike wafanye ukaguziili waone madudu yaliyopo.

Wakaguzi wa ndani ambao huwa wanakagua ni timu moja na majipu haya,huwa wanakuja kupigwa madini/noti tu wanatembea .

Kama ukaguzi makini utakuja,kuna watu kama saba ambao ni hatari sana kwa ustawi wa kwimba.

Kauri mbiu ya Mgufuri ni "HAPA KAZI TU" Kila tunapopiga kelele juu ya suala hili tunajibiwa hapa kazi tu kwa kuiba hela.

Juzi DT ameenda Hospital ya Wilaya kuomba Pesa kwa ajiri ya Malipo ya watu X ili,lakini baada ya kupewa zile pesa kilichotokea ni makubwa.

Haya ni machache,smart phone yangu inazima,Nitakuja na muendelezo wa Hoja nyingine kesho katika Idara ya Afya ambapo on-calls hazilipwi na Matokeo yake anakula kigogo mmoja ambaye ni X.

DT ASIMAMISHWE KAZI.Wengine watafata.

Katibu Chadema (W) Kwimba.
0782270412.Mwl Martin.
 
Mmbea grade one huyu. Watumishi huko kwimba muogopeni kama ukoma mtu huyu.
 
Sina neno, nipo busy na kukusanya michango ya kusaidia watu waliokumbwa na tetemeko.
 
halafu jua hapa ni JF hatuna x na y weka full majina usaidiwe vizuri ukificha ni sawa na case kutokuja tu hapa warahishishie wakubwa kazi na case iamuliwe fasta maana uchunguzi utakua umeufanya, sasa ukisema x na y hio inakua kazi ya ziada
 
Mtoa taarifa hana kosa,wewe unayaeanza kukosoa ndio unakosa na inaqwzekana ndio kundi hilohilo la majipu
 
Back
Top Bottom