Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,480
- 7,904
Mhariri wa gazeti Mwanahalisi, Jabir Idrissa amesema wataenda mahakamani kupinga kufungiwa miaka miwili kwa chombo chao wakidai hawajatendewa haki na serikali. Mwanahalisi lilifungiwa Rasmi jana na mkurugenzi wa habari, Dk. Hassan Abass likituhumiwa kwa kuandika habari za kichochezi mara kwa mara licha ya kupewa onyo.
Mhariri amesema kikatiba anayepima kama sheria imetekelezwa au imevunjwa ni mahakama, amejivuna kuwa hakuna aliyepeleka kesi mahakamani dhidi yao na akashinda.
Mhariri amesisitiza kuwa hawawezi kutunga habari kwani wananchi watang'amua na watakimbia na madai hayo yamemuumiza sana kwani inamaanisha anawalisha wananchi habari za kutunga kwa miaka 12 ya kuwa mhariri.
Amesema serikali inajidhihirisha isivyoweza kuvumilia yale ambayo hayapendezi kwao.