Mhariri Mwanahalisi: Serikali inajidhihirisha isivyoweza kuvumilia yale ambayo hayapendezi kwao, kutinga mahakamani

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,806

Mhariri wa gazeti Mwanahalisi, Jabir Idrissa amesema wataenda mahakamani kupinga kufungiwa miaka miwili kwa chombo chao wakidai hawajatendewa haki na serikali. Mwanahalisi lilifungiwa Rasmi jana na mkurugenzi wa habari, Dk. Hassan Abass likituhumiwa kwa kuandika habari za kichochezi mara kwa mara licha ya kupewa onyo.

Mhariri amesema kikatiba anayepima kama sheria imetekelezwa au imevunjwa ni mahakama, amejivuna kuwa hakuna aliyepeleka kesi mahakamani dhidi yao na akashinda.

Mhariri amesisitiza kuwa hawawezi kutunga habari kwani wananchi watang'amua na watakimbia na madai hayo yamemuumiza sana kwani inamaanisha anawalisha wananchi habari za kutunga kwa miaka 12 ya kuwa mhariri.

Amesema serikali inajidhihirisha isivyoweza kuvumilia yale ambayo hayapendezi kwao.
 
Ninachojiuliza ni kuwa KATIKA HILI KESI HII YA NYANI HAIPELEKWI KWA NGEDERE????????? (in north zone strategy's Voice)
Maana mahakama zetu huwa hazitutendei haki kabisa sisi U. K. A. W. A

naenda zangu Loliondo siyo Zimbabwee
 
Mahakama ni taasisi ya hovyo sana kwa wakati huu,

Kesi za CUF zimechukua miaka wakati kuna majaji hawanaga kazi,wanasoma magazeti

Hii taasisi ina maelekezo kutoka juu,hovyo kabisa
 
.
Acheni kuwa wanyonge. Yaani mnaonesha mmeshindwa kabla hata ya hiyo kesi kufunguliwa
 
Kushindwa haiwezekani,Bali mwanahalisi wamefungiwa miaka miwili,usishangae kesi ikachukua miaka miwili

Kesi za CUF,tena zenye hoja ndogo tu,je lipumba alijiuzuru au laaa,hizo zitachukua miaka mitano au mpaka zaidi ya 2020
 
Kama ni kesi ya kupinga kufungiwa hata ikichukua miaka kumi sawa tu. maana itaonesha kama kulikuwa na uhalali wa kufungiwa. Kukaa kimya baada ya kupewa adhabu ni mbadala wa kukubali makosa yako, hata kama ulikuwa na sababu ya kukaa kimya.
Kesi za CUF zina mlolongo mkubwa, hata kama unaona hoja zake ni ndogo lakini ili kuzijibu hizo hoja unahitajika mchakato mkubwa
 
Nahisi wafanyakazi wa Mwanahalisi inabidi wawe wana ajira nyingine pembeni.

Hii ikisimamishwa unarudi kwa nyingine.

Miaka miwili bila kipato ni kazi juu ya kazi.

Kama hii sheria haipo.
Wabunge wapitishe sheria ya kutaka serikali iwalipe mshahara wafanyakazi wa media ambayo itafungiwa.

Inaweza ikadiscourage huku kufungiana kila muda.
 
Huyo huyo Mlalamikaji huyo huyo msikilizaji kesi na huyo huyo mtoa hukumu kweli Tanzania mpya inakuja
 
Mhariri wa gazeti Mwanahalisi, Jabir Idrissa amesema wataenda mahakamani kupinga kufungiwa miaka miwili kwa chombo chao wakidai hawajatendewa haki na serikali. Mwanahalisi lilifungiwa Rasmi jana na mkurugenzi wa habari, Dk. Hassan Abass likituhumiwa kwa kuandika habari za kichochezi mara kwa mara licha ya kupewa onyo.

Mhariri amesema kikatiba anayepima kama sheria imetekelezwa au imevunjwa ni mahakama, amejivuna kuwa hakuna aliyepeleka kesi mahakamani dhidi yao na akashinda.

Mhariri amesisitiza kuwa hawawezi kutunga habari kwani wananchi watang'amua na watakimbia na madai hayo yamemuumiza sana kwani inamaanisha anawalisha wananchi habari za kutunga kwa miaka 12 ya kuwa mhariri.

Amesema serikali inajidhihirisha isivyoweza kuvumilia yale ambayo hayapendezi kwao.

Hii sheria ya kufungia magazeti siilisha futwa jamanii na sheria mpya au !!???
 
Hata hivyo mwanahalisi kufungiwa siyo habari tena wala siyo kiki kwa serikali, nilijua tu hata leo wakienda mahakamani mwanahalisi watashinda.

Back
Top Bottom