Mhariri Jambo Leo afariki dunia

Comments za hii thread sijawahi kuziona mahali pengine popote panapokuwa na taarifa ya msiba. Hii ni mara ya kwanza naona watu bila aibu wanamlaumu Marehemu na kusema wazi walikuwa wanamchukia. Kwa misingi hiyo, yawezekana pia kifo chake kina utata kutokana na wengi wenu kutoridhishwa na uandishi wake.
 
jambo Leo sijawahi hata kulishika hata kulisoma na inasemekena mmiliki na RizOne... Rest in Peace Mhariri
 
Mhariri Mkuu wa Gazeti la JAMBO LEO Willie Edward Afariki Dunia. Tone Multimedia company Limited tumepokea kwa masikitiko makubwa msiba huu, Tunawapa pole Familia ya marehemu,ndugu jamaa na Marafiki. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi.

Willy Edward alikuwepo mkoani Morogoro katika mafunzo ya siku moja ya Sensa pamoja na wanahabari wengine na kuwa inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu kwa muda mrefu .​

akithibitisha juu ya taarifa hiyo mhariri wa habari wa gazeti la Mtanzania Kulwa Karedia ambaye walikuwa wote na Willy mjini Morogoro amesema kuwa hadi majira ya saa 3 usiku walikuwa wote na baada ya hapo aliwaaga wanahabari wenzake kuwa anakwenda kulala .

556368_317271968358753_305451642_n.jpg
 
uchunguzi unaonesha kafa vipi jamani? maana ili gazeti ni la siasa za ubaguzi sana. Poleni wafiwa
 
uchunguzi unaonesha kafa vipi jamani? maana ili gazeti ni la siasa za ubaguzi sana. Poleni wafiwa


[h=1]MWILI WA MAREHEMU WILLY EDWARD UKITOLEWA MOCHWARI MOROGORO TAYARI KUSAFIRISHWA KWENDA DAR[/h]




Kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward

Ogunde, George Ongiri Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na ndugu, jamaa na waandishi wa habari, kubeba mwili wa mhariri huyo, aliyefariki dunia ghafla jana usiku eneo la Forest Hill, mjini Morogoro. Mwili huo ulikuwa unatolewa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha Mugumu kilichopo wilaya ya Serengeti, mkoani, Mara..



Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Azizi Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa Willy Edward



Baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mbunge wa Morogoro mjini, Azizi Abood, wakiwa na huzuni walipokuwa wakisubiri kutoa heshima za mwisho katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, muda mfiupi kabla ya mwili kusafishwa Dar es Salaam.



Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa

marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri​
Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde
 
R.i.p Mkuu.! Lakini jambo leo ningeshauri libadili mwelekeo.!
 
Kwa jinsi gazeti hili lilisivyopendwa sitangaa msiba huu hapa jukwaani usipewe kipaumbele kama kafa sijui mfungwa tena mhalifu wa kutisha!!!!

Siasa mbaya sana.

Rip Willy.

RIP Willy Edward!!! Sijawahi kununua hilo gazeti wala kulipenda ila nilipoona familia yako na picha yako TBC usiku huu nimeumizwa mtima. Mungu awatie nguvu wanafamilia.
 
KWA mara nyingine tasnia ya habari nchini imepata pigo la kuondokewa na Mhariri
Mkuu wa gazeti la kila siku la Jambo Leo, Willy Edward (38), aliyefariki ghafla
usiku wa kuamkia jana akiwa mjini Morogoro.Taarifa za kifo chake zilitolewa na mhariri mwenzake wa gazeti la Mtanzania,
Kulwa Karedia, ambaye alikuwa naye kabla ya kufikwa umauti, akisema kuwa alikuwa
ni mzima wa afya, na kwamba aliwaaga anakwenda kuwaona watoto wake ambapo alikaa
huko mpaka saa 6:30 usiku.

Alisema muda wa kurudi hotelini alikokuwa amefikia ulipofika, Willy alimwita
dereva wa pikipiki ili amchukue, lakini usafiri huo ulipofika hakuweza kuupanda
kwani alipotoka nje na kutembea kwa hatua chache alianguka.

Karedia aliongeza kuwa, ndugu zake walimkimbiza hospitalini na baada ya
vipimo vya daktari, ikabainika kuwa alikwishafariki dunia

HABARI ZAIDI ANGALIA TANZANIA DAIMA
 
Back
Top Bottom