Diplomatician
Member
- Aug 22, 2013
- 21
- 1
Mbali na Changamoto za hapa na Pale za Bidii ya Mh.Waziri Mkuu anazokabiliana nazo katika uhamasishaji wa Jamii ya Kitanzania kuhusu Ufugaji wa Nyuki,lakini kuna Baadhi ya Wananchi wameitika wito huo na kujitoa kinagaubaga kuchangamkia fursa hiyo yenye Mtaji mdogo katika baadhi ya Maeneo.
Sisi wanachi wako Mh.Waziri Mkuu kupitia mahala hapa Jamii Forum ambapo tunaamini kua Taarifa hii itakufikia kwa kua kuna Baadhi ya Wabunge,mawaziri na Wafanyakazi wengine katika Ngazi tofauti Serikalini ni Wadau wazuri wa JAMII FORUM, Jambo letu la Msingi ni kua, Sawa tumeitika wito wa Ufugaji wa Nyuki na sasa tuna kiasi cha kutosha cha asali LAKINI JE,SOKO la Kuuza Bidhaa hii TUYAPATE WAPI?
Mh. Waziri Mkuu tunatambua ya kua Mtu anapoamua kujihusisha katika Mazao ya Biashara ni Juu yake kuhakikisha anatafuta soko la Bidhaa zake hapa Kwetu Tanzania.
Lakini ombi latu kwako ni kwamba kama unavyotumia Nguvu nyingi kuhamasisha wananchi kujihusisha na Ufugaji wa nyuki vivo hivyo Tumia Nguvu kutuandalia Soko zuri ndani na Nje ya nchi,kwa kufanya hivyo utakua umeturahisishia sisi wananchi wa Kawaida ambao paka sasa hatujui wapi pa kuanzia ili kuuza Asali yetu ambayo tumekwisha ivuna na hatuna Wateja mpaka sasa.
Mh, Waziri Mkuu kama unavyodai kua serikali yako ni Sikivu hivyo naamini kua utakua Sikivu pia katika Suala hili.
Ukinyamaza kimya hatutachelea kujua kuwa Uhamasishaji wako ni wa kisiasa tu na si Wa dhamira ya Kweli kumkomboa Mwananchi wa kawaida.