Izz
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 750
- 322
Wanasiasa wana kauli yao moja upenda kuitumia pale wanapo puuzia Mambo, usema "Ni upepo tu huo, utapita". Lakini kwa hili la Mtwara, chonde chonde wekeni siasa kando na tulitafutie ufumbuzi utakao nufaisha pande zote mbili yaani serikali (mwekezaji) na Wananchi wa Mtwara.
Tusiogope kutoa maamuzi magumu kwa kuona aibu ya kukubali hoja za upinzani na kuchekwa kua mmeshindwa. Waswahili wanasema 'funika kombe mwanaharamu apite'
Mtwara kijeografia iko pembezoni na ni hatari kwa nchi ikiwa vurugu hizi zikiendelea kuwepo, kwani hatujui adui yeti ni nani na wao wanaweza kutumia mwanya huu wa vurugu kuotesha mizizi yao na kuhatarisha AMANI.
Ni wakati sasa wa Mh. Waziri Mkuu Pinda kufanya maamuzi magumu ya kizalendo ili kumaliza mgogoro huu kwa njia ambazo hazitaacha makovu kwa wana-Mtwara.