Mh. Tundu Lissu apewe ulinzi na Serikali ya CCM punde atakapomaliza matibabu nchini Ubelgiji

shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
8,106
3,967
Wana JF naandika hili katika bipartisan views/Maoni yasiyoegemea chamachochote. Ili mtu asije akaanza kuniita majina.

Tundu Lissu ni kiongozi mashuhuri wa upinzani na hilo halipingiki. Ombi langu ni kuwa itakuwa vizuri sana kwa serikali ya CCM kumpa ulinzi kama Kiongozi mashuhuri aliyeepuka kuuawa na watu WASIOJULIKANA.

Mpaka sasa waliofanya jaribio hilo hawajapatikana. Na hivyo ili kuzuia mission yao mbaya ambayo inaweza KULIPAKA taifa letu MATOPE katika jamii ya kimataifa ni vizuri TL akirudi apatiwe ULINZI wa kutosha. Both wa kutembea nao na nyumbani kwake kwa gharama zetu za walipa KODI.

Katika nchi zilizo na demokrasia viongozi mashuhuri wa upinzani HUPEWA ULINZI ili kuzuia serikali ISILAUMIWE kwa lolote.
Maana wale waliokuwa wakitaka kumuua Tundu Lissu are still at large/Hawajapatikana.Ni vizuri serikali ichukuwe UJASIRI huu wa tahadhari.

Hii haionyeshi kuwa ni kumpatia umaarufu bali ni kulinda heshima na jina la nchi yetu kama KISIWA cha AMANI.

Akiombwa na AKATAE ulinzi wa vyombo vya dola, basi serikali itakuwa IMEOSHA mikono YAKE.
Maana TL ni Mtanzania mwenzetu.
Utofauti wa kivyama hauna maana kuwa TUCHUKIANE.
Niko radhi kukosolewa.
Mwaonaje wana jamvi?
 
Kwa kuongezea tu katika hili.
UPENDO ni jambo kuu sana.
Mpende ADUI yako.
Na katika siasa hamna permanent adui bali permanent maslahi.
 
Apewe ulinzi na serikali.!? Unataka apewe walinzi au majambazi! ?Labda lukaku na barshite watoke madarakani ndio tuweze kufikiria hilo, ila kama bado wapo madarakani haiwezekani!
 
Kwa kuongezea tu katika hili.
UPENDO ni jambo kuu sana.
Mpende ADUI yako.
Na katika siasa hamna permanent adui bali permanent maslahi.
Mungu ndiye alieanza kuwapenda wanadamu, mungu wetu hana mpango ni chuki visasi utekaji kupoteza watu na mauji kwa kwenda mbele. Hapo upendo unaanzia wapi?
 
Wana JF naandika hili katika Bipartisan views/Maoni yasiyoegemea chamachochote. Ili mtu asije akaanza kuniita majina.

Tundu Lissu ni kuongozi mashuhuiri wa Upinzani na hulo halipingiki. Ombi langu ni kuwa itakuwa vizuri sana kwa serikali ya CCM kumpa ulinzi kama Kiongozi mashuhuri aliyeepuka kuuawa na watu WASIOJULIKANA.

Mpaka sasa waliofanya jaribio hilo hawajapatikana. Na hivyo ili kuzuia mission yao mbaya ambayo inaweza KULIPAKA taifa letu MATOPE katika jamii ya kimataifa ni vizuri TL akirudi apatiwe ULINZI wa kutosha. Both wa kutembea nao na nyumbani kwake kwa gharama zetu za walipa KODI.

Katika nchi zilizo na demokrasia viongozi mashuhuri wa upinzani HUPEWA ULINZI ili kuzuia serikali ISILAUMIWE kwa lolote.
Maana wale waliokuwa wakitaka kumuua Tundu Lissu are still at large/Hawajapatikana.Ni vizuri serikali ichukuwe UJASIRI huu wa tahadhari.

Hii haionyeshi kuwa ni kumpatia umaarufu bali ni kulinda heshima na jina la nchi yetu kama KISIWA cha AMANI.
Akiombwa AKATAE ulinzi wa vyombo vya dola, basi serikali itakuwa IMEOSHA mikono YAKE. Maana TL ni Mtanzania mwenzetu.Utofauti wa kivyama hauna maana kuwa TUCHUKIANE.
Niko radhi kukosolewa.
Mwaonaje wana jamvi?

Naunga mkono hoja, mchawi mpe mwanao akulelee...Good Idea
 
Nani alingoa zile kamera za kiona mbali masaa 24 ?
 
Mbona huzungumuzii zile kesi zake lukuki ambazo zinamsubiri mahakamani? Mbona huzungumzii yule dreva wake aliyekwamisha uchunguzi wa kuwanasa hao waliomshambulia kwa AK47, silaha ambayo haimilikiwi na majeshi yetu?
 
Hata wakimuua mtaifanya nini hiyo serikali ya CCM?

Ndugu nothing is permanent under the sun, so it is the fear, hivyo visasi vikitoka kifuani nakuja katika uhalisia wake amini amini ninakuambia utailaani hiyo siku ambayo ameuwa na utamlaani kila mtu aliyeshiriki kumua na hata unaweza kujilaani na wewe unayeshabikia kifo cha Tundu Lissu na wenzako wanashabikia kifo hicho na ndipo utagundua kuwa wote mnaoshabikia hamkujua mletendalo, utakaa uamini Tanzania utakayoishuhudia, itakuwa ni Tanzania nyingine kabisa ambayo hujawahi hata kuiwazia katika maisha yako na baada ya hapo utaelewa kuwa binadamu ni kiumbe hatari sana kuliko kiumbe chochote ambacho kimepata kuishi katika sayari hii.
 
Kwa kuongezea tu katika hili.
UPENDO ni jambo kuu sana.
Mpende ADUI yako.
Na katika siasa hamna permanent adui bali permanent maslahi.

..suala hili linachanganya sana.

..utakumbuka kwamba TL alishambuliwa ktk eneo la makazi ya viongozi.

..TL anaishi hapo kwasababu ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani na bunge la jamhuri limempatia nyumba ktk makazi hayo.

..eneo hilo, kwasababu ni makazi ya viongozi linalindwa 24/7.

..siku na saa ambayo TL alishambuliwa ulinzi haukuwepo!!

..JE, ktk mazingira hayo, ulinzi wa serekali ni wa kuaminika kiasi gani?
 
Tundu Lissu ni kuongozi mashuhuiri wa Upinzani na hulo halipingiki. Ombi langu ni kuwa itakuwa vizuri sana kwa serikali ya CCM kumpa ulinzi kama Kiongozi mashuhuri aliyeepuka kuuawa na watu WASIOJULIKANA.
Hapo sahihisha andika "Tundu Lissu alikuwa kuongozi mashuhuiri"...
 
..suala hili linachanganya sana.

..utakumbuka kwamba TL alishambuliwa ktk eneo la makazi ya viongozi.

..TL anaishi hapo kwasababu ni mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani na bunge la jamhuri limempatia nyumba ktk makazi hayo.

..eneo hilo, kwasababu ni makazi ya viongozi linalindwa 24/7.

..siku na saa ambayo TL alishambuliwa ulinzi haukuwepo!!

..JE, ktk mazingira hayo, ulinzi wa serekali ni wa kuaminika kiasi gani?
Unajua hapo atakuwa salama. Sababu ni kuwa wale walinzi atakaopewa WATAJUA wamepewa JUKUMU na hivyo yeyote yule hatadiriki wala kuthubutu kutuharibia jina la nchi kwa kumdhuru. Mh. Tundu Lussu.
 
Back
Top Bottom