Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,522
- 24,010
Miaka mingi iliyopita tulimsifu shujaa kibanga kwa kumpiga mkoloni aliyewaita waafrika Nyani,Mbwa na majina yote mabaya. Kibanga hakupendezwa na kauli hizo zenye kuutweza utu wa mwafrika tena nyumban kwa mwafrika kwa maneno yenye kashfa na dharau ya hali ya juu.
tunakumbuka siku ile bwana yule mzungu alipoenda kukagua mashamba na kukuta kuwa hakukuwa na mazao ya kutosha kutokana na ukosefu wa Mvua. Bwana huyo Mkoloni alianza kuporomosha matusi na kana kwamba haitoshi alitaka hata kumtandika bakora Kibanga kitu ambacho kilimkwaza sana Kibanga na kuamua kumpiga hasa mkoloni mpaka alipokuja kuomba radhi aachiwe.
Miaka mingi imepita Kibanga amegundua kuwa yale aliyokuwa akisemwa na mkoloni yule yalikuwa ni kweli. waafrika ni kama nyani,kima.mbwa n.k. wamekosa utu, wanauana wenyewe kwa wenyewe kama vile ambavyo mbwa hupigana mpaka kuuana. wamekuwa hawajali utu wanagombania madaraka na kutaka kuendelea kukaa madarakani. katika Umri huu wa uzee Kibanga amekumbuka maneno ya yule mkoloni kuwa ninyi waafrika ni wavivu, hamfanyi kazi. amekumbuka baada ya kuangalia namna ambavyo ardhi ya afrika haitumiki vizuri. rasilimali za afrika zinakuja kunyonywa na wageni.
tumeona namna ambavyo waafrika wameuana na wanauana kwa sababu ya dini,kabila,koo na rangi. tumeona namna ambavyo waafrikaw wanang'ang'ania madaraka na wapo tayari hata kuua ili waendelee kubaki madarakani. Tumeyaona ya Syria, Egypt, Burundi, Zanzibar, Kenya miaka ile, ZImbabwe na hata Afrika kusini weusi walipowaua wenzao kwa sababu ya Ajira.
Kibanga katika uzee wake huu akiwa amechoka sana ameamua kumuomba radhi mkoloni yule kwa kitendo alichofanya miaka ile kumpiga kwa kutetea waafrika wenzie. Kibanga huyu ambaye ameachwa muda huu amejilalia kwenye kibanda chake cha mbavu za Mbwa amepata nafasi hiyo aliyokuwa akiiihitaji leo hii baada ya Mkoloni yule kuwa anafungua visiwa vya maji ambayo amevichimba kama msaada baada ya Kijiji anachoishi Kibanga kukosa maji kwa miaka mingi sana hata baada ya Uhuru. Ni mkoloni yule yule aliyepigwa na Kibanga amekuja sasa kuwasaidia wana kijiji cha Kibanga. Kibanga huku akitokwa na machozi ameinama akitaka kumshika miguu mkoloni yule kumtaka radhi. Mkoloni amekataa jambo hilo akisema pia naye hakufanya jambo jema miaka ile kutamka maneno yale "mbele za watu" baada ya kumaliza kufungua mradi huo alikaa na kuongea na kibanga mamabo mawili matatu wakikumbushana habari za nyuma. na Mkoloni akauliza kama walishajenga Reli nyingine ukiacha ile waliyojenga wao. Kibanga kwa aibu aliinamisha kichwa na kujibu "bado tupo kwenye mchakato"
Mkoloni yule alisikitika na kusema wakati mwingne alikuwa anawaza kama wangekuja angalau kurekebisha mambo flan nchini halafu waondoke wawaachie tena mambo yakiwa salama. Akaulizia hata vile viwanda walivyokuwa navyo vichache miaka ile. miradi ya umeme n.k na Mkoloni yule alishangaa kuwa mbona akiwa huko kwao anawaona akina Jumbe wanaenda sana nchini kwake mkoloni wakiwa na mapesa mengi? na misafara mikubwa sana?
Baadaye yule mzungu aliondoka kuelekea kwenye kijiji kingine kuendeleza miradi ya kuwasaidia wananchi. Kibanga alirudi chumbani kwake akajilaza kitandani na kutafakari miaka ile ilivyokuwa na sasa hali ilivyo. akatokwa na machozi kwa uchungu mkubwa uliomjia rohoni kama mtu aliyekatwa na kisu kisicho na makali . akanyanyua mikono yake na kuipeleka kifuani akiugumia maumivu. akafumba macho akalala usingizi wa miele. maskini peke yake akiwa amezungukwa na kiza huku mbu na nzi wakimng'ong'a. angalau alipumzika kutokana na adha za nchi yake.