Mh Rais wasamehe wenye vyeti feki

Mandakakawa

Senior Member
Mar 29, 2017
113
56
Nianze kwa kumpongeza rais wetu Dr. John Pombe Magufuli kwa kuunda tume ya kubaini kilichokuwa kinaendelea kuhusu madini yetu hongera sana, ila upande wa pili naomba nimkumbushe zoezi la vyeti sio halali limeisha?

Naomba nichukue nafasi hii kumuomba Rais awasamehe hawa wote waliokumbwa na hili balaa kwani naamini wengi hawakufanya kwa nia mbaya ni kweli kudanganya kwenye elimu ni kosa lakini haliwezi kufikia wale tuliowaamini wasomi wa kweli lakini ndio waliokuwa wanashirikiana na na wageni kuliibia taifa hawa ndio watu kudili nao kisawasawa na sio madini tu angalia na maliasili, gas na tender kubwa kubwa za nchi.

Naomba Mh. Rais ni kweli hawa wa vyeti feki wamekosa wasamehe naamini kabisa watalitumikia taifa kwa weledi na uaminifu ila mfumo ulekebishwe kudhibiti haya yasijitokee tena.
 
Unataka msamaha gani zaidi ya kutoshitakiwa kwa kuwakilisha nyaraka bandia kwenye ofisi za umma!?
 
Si walishasamehewa wakaambiwa waende nyumbani kwa 'Amani ya Bwana'? Kwani kuna mtu alifungwa?

Msamaa unatakiwa hapa ni kuwarudisha kazini kwani huku mtaani wa nashindwa pa kuanzia na kikubwa ni kuanza mapambano na hawa wahujumu uchumi waliopo na waliopita ila Mh raisi chondechonde wasamehe na warudishe kazini
 
Mbona alishawasamehe kwa kuwapa wiki mbili pia za kujiondoa wenyewe!!!

Tafuteni tu kazi zingine hata kulima. Mtafurahia kuondolewa mkijopanga.

Kwa sasa sahau juu ya kurudishwa mlipokuwa.
 
naona watu wanajibu kishabiki tu ila hawa watu ni watu ambao wana misongo mikubwa sana ya mawazo walichofanyiwa ni haki lakini humanity iangaliwe makosa yalishafanyika zamani basi wafocus kuzuia tatizo lisitokee tena.
ona huyu kajinyonga
TMPDOODLE1495728578980.jpg
 
Akiwasamehee hao basi awasamehe wale wote aliowatumbua, na wafungwa wote walioko magerezani ili tuanze upya.

Nianze kwa kumpongeza raisi wetu Dr. John Pombe Magufuli kwa kuunda tume ya kubaini kilichokuwa kinaendelea kuhusu madini yetu hongera sana, ila upande wa pili naomba nimkumbushe zoezi la vyeti sio halali limeisha?

Naomba nichukue nafasi hii kumuomba Rais awasamehe hawa wote waliokumbwa na hili balaa kwani naamini wengi hawakufanya kwa nia mbaya ni kweli kudanganya kwenye elimu ni kosa lakini haliwezi kufikia wale tuliowaamini wasomi wa kweli lakini ndio waliokuwa wanashirikiana na na wageni kuliibia taifa hawa ndio watu kudili nao kisawasawa na sio madini tu angalia na maliasili, gas na tender kubwa kubwa za nchi.

Naomba Mh. Rais ni kweli hawa wa vyeti feki wamekosa wasamehe naamini kabisa watalitumikia taifa kwa weledi na uaminifu ila mfumo ulekebishwe kudhibiti haya yasijitokee tena.
 
naona watu wanajibu kishabiki tu ila hawa watu ni watu ambao wana misongo mikubwa sana ya mawazo walichofanyiwa ni haki lakini humanity iangaliwe makosa yalishafanyika zamani basi wafocus kuzuia tatizo lisitokee tena.
ona huyu kajinyonga
View attachment 514386
Wakati wanachonga vyeti walikuwa hawajui kuwa ni makosa?
 
Unaomba awasamehe kwa kuwa ni wengi?
Je, uliwahi kuwaombea msamaha wale waliofukuzwa na kuhukumiwa jela miezi ya nyuma ambapo ilikuwa kwa mmoja mmoja?
Kama swali la pili huna majibu kwalo toka hapa kabla sijakutukana.
 
Back
Top Bottom