Mh Rais vunja bodi ya Utalii Tanzania

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Wana jamvi

Kutokana na majibu ya kuwa na mkakati wa kutangaza utalii ambayo mikakati hiyo inatoka mdomoni bila utekelezaji kwa kipindi kirefu sasa, Aidha, mikakati hiyo imekua bubu na kufanya Wakenya kuwahi kutekeleza kwa miaka sasa, katika kutangaza vivutio vyetu katika kila tukio kubwa mfano sherehe za krismass, mwaka mpya na sherehe za kitaifa na kimataifa, kutumia wanamichezo, kutumia bidhaa zetu ni wazi kabisa bodi hii imeishiwa mbinu au watumishi wamekosa sifa stahiki hivyo kutotekeleza au kuwa na sera na mbinu mbovu za kukuza utalii, kibaya zaidi watumishi wake wengi hawafahamu vivutio vyote ama wanafahamu kupitia luninga sio kwa kuona au hawana Key attractions inventory.
Vyema basi bodi ya utalii isukwe upya na wataalamu watoke Tanapa, Ngorongoro, Makumbusho ya Taifa na Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori ( TAWA) kwani hao wote wanajua kwa wingi wao vivutio vyote, kwani juhudi zote za kuja kwa wageni bado zimechangiwa na mamlaka nilizotaja, bodi ya utalii hawajui hata ("Slogans") kauli mbiu katika kila Hifadhi na mamlaka ya hifadhi Ngorongoro
 
Wewe unategemea nin kama katibu mkuu wa wizara ni mwanajeshiii, hapo jiandaeni kuona mapambano ya ujangiri tuu na sio kukuza utalii......,
 
Hapo inabidi kwanza katibu mkuu awe mjuzi wa mambo ya wildlife management na tourism ndio mambo yanaweza kwenda vizurii.... Mwambie muheshimiwa aanze kuweka watu wenye taaluma zao na waliofanikiwa kwenye sehemu husikaa na wasiwe academicians.... Academicians waachwe waendelee kutufundishia vijana wetuu ili tupate watendaji walio kwiva
 
Back
Top Bottom