tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,017
- 1,940
Mh SSH ifikapo Tarehe mosi May 2021 watumishi woote wa umma wanatamani kusikia mambo mawili tuu yaani Kuongeza mishahara pamoja na kuwapandisha Madaraja.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba ni miaka karibia tano/ sita watumishi wamepuuzwa na serikali iliyokuwa ya Mh Hayati Magufuli japo maisha yanapanda kwa kasi sana.
Jambo hili limekuwa chungu sana na lenye maumivu yasiyo elezeka kwa kila mtumishi wa umma. Rais Magufuli alifanya mengi mazuri kwa Taifa hili lakini yoote hayakuwa na maana kwa watumishi wa umma, hakuna mtumishi wa umma yeyote ambaye aliyafurahia mema ya Hayati Magufuli kwa sababu tu ya uminyifu wa haki zao.
Mengine ambayo unaweza kugusia na yakachochea hisia za watumishi na kukuona wewe ndiye Joshua wa kwenye Biblia aliye mrithi Musa ni pamoja na:
3. Kufungulia uhamisho kwa awatumishi haswa walimu.
4. Kupunguza kodi kwa watumishi wa umma.
5. Kuingilia kati suala la makato ya bodi ya mikopo yaani ikiwezekana irudishwe ile 8%.
6. Kuangalia upya suala la kikotoo.
7. Fao la kujitoa kazini.
8. Kuondoa mdudu aitwaye Retention fee kwa wanufaika wa bodi ya mikopo.
9. Bima ya Afya kwa mtumishi asipangiwe aina ya wategemezi bali aweke mtu yeyote anayemtaka.
10. Kuondoa vyama nyonyaji kwa watumishi wa umma kama CWT, TALUGWA, TUGHE nk
11.
12..
Haya niongezeeni wana JF...
Hakika mama ukiyasemea haya haswa hayo mawili ya juu basi hata ukiteremka jukwaani ukakwea pipa kurudi Dar salaam tayari Mhuri wa moto wa jina lako utagongwa kwenye viunga vya moyo ya watumishi na utakumbukwa vizazi na vizazi. Pia kama utakuwa na mpango wa kusalia madarakani baada ya miaka 4= hii basi utakuwa umepata turufu yenye nguvu kubwa