Mh.Rais, Leo ni siku yetu wa baba.

sirjohn

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
778
1,000
MH. JOHN POMBE MAGUFULI, LEO NI SIKU YETU WA BABA.

Mh. Rais, pole sana kwa kazi ya kututumikia watanzania kama mfanya kazi namba 1, tambua haya ni mapenzi toka kwa Mungu, tambua siyo kwamba wewe ni zaidi ya watanzania wote zaidi ya milioni 50 ila ni kwa neema tu zake mwenyezi Mungu, kamwe hatutaacha kukuombea, tunaamini Mungu yuko pamoja nasi. Sina sababu ya kuandika mengi sana hasa uliyoyafanya kwa muda mfupi , unayoyafanya na unayo panga kuyafanya, neno letu ni moja tu kwako, watanzania chapa kazi.

Pamoja na sisi kukuamini na kukukabidhi katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uisimamie na kuilinda bado unatakiwa kutambua kuwa una jukumu kubwa sana la kuwa baba wa taifa (watu wanakufananisha na mwalimu Nyerere, hii ni heshima kubwa sana, usikubali kamwe kuiharibu! hakuna mtanzania hata mmoja aliyewahi kufananishwa na Mwalimu Nyerere kwa utendaji wake), mwalimu alikuwa msikivu, mvumilivu, mnyenyekevu, mchapa kazi na aliwapenda sana watanzania ( kifo cha mwalimu kililiza wengi, waliokuwa mahospitalini, magerezani, mashuleni, nk)! Una kazi ya kuwathibitishia haya watanzania kuwa una haki ya kufananishwa na mwalimu!

Pamoja na kwamba tumekukabidhi nchi ili utuongoze kwa kupitia kiti cha urais ,bado unawajibu wa kutambua mamlaka ya Rais ni mamla ya wananchi kwa mjibu wa katiba yetu, una wajibu mkubwa sana kwa watanzania wote bila kujali dini zao, elimu zao, kabila zao na itikadi za vyama vyetu (hili ndilo linalotusumbua kwa sasa watanzania, mwalimu alisema tuna kazi za kupambana na ujinga, maradhi na umasikini lakini kwa sasa tuna kazi ya kubwa ya kupambana na ubaguzi wa itikadi wa kivyama) na hili limekuwa na changamoto nzito kwenu tuliowapatia dhamana ya kutuongoza.

Mh. Rais yapo mambo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine umeyatenda bila kujali sisi tutasema nini hilo linakubalika kwa misingi ya manufaa kwa nchi yetu na watanzania kwa ujumla, hakika tunakuamini sana amiri Jeshi wetu mkuu .

Sikupenda kuandika chochote toka umeingia Ikulu maana sijaona zito ambalo ni chukizo kwetu sisi wanao, wewe ni baba mzuri wa familia! Pamoja na hayo yote mazuri binafsi sitakuwa nimejitendea haki au kukutendea haki wewe au watanzania kwa ujumla kama sitalisema hili la moyoni kwangu! mh Rais, ni wakati sasa wa kuacha kusema kuwa mkubwa hakosei, na bahati nzuri hili umeanza kulisimamia wewe mwenye (walikosea kwenye makinikia na sasa unarekebisha ). Kama unavyoomba na kututaka tukuombee hivyo hivyo na sisi tunakuomba utusikilize hata kama mawazo yetu hayana maana lakini yasikilize.

Mh Rais kuna huyu ndg yetu Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda, pamoja na mambo mengi ya hapa na pale aliyoyatenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma sikuona sababu ya kumsema kwako, nilitamani kumpa muda, nilitambua yeye ni binadamu na binadamu anakosea, ila hakosei kila siku! hizi ni ofisi za umma, ofisi za watanzania ambazo zina heshima zake, zina utaratibu wake na zina kaliwa na watu wanaotambua misingi ya utawala, haki za binadadamu, utu wa mtu na heshima ya kuwa binadamu! ( mwalimu alisema tuhuma tu inatakiwa kumuweka pembeni mtumishi wa umma! Usipuuze minongono ya watu) Isiwe tu kwa sababu ya HAPA KAZI TU basi tuamue kutumia nafasi zetu kuwafanya watumishi wa umma sehemu ya kujifunzia kufoka. Mh Makonda alianza kidogo kidogo kuwadhihaki wafanya kazi wa umma na jamii ilipiga kelele lakini zile kelele alikuwa anapigiwa kiziwi na kwa bahati mbaya na wewe ulisimama upande wa Makonda na kuacha kusikiliza watanzania wengi waliokasirishwa na huyu RC (mtoto umleavyo ndivyo akuavyo! ), wakati mwingine huwa naamini kuwa Makonda ni BASHITE na hii ni kwa matendo yake! Ukimgusa tu utasikia vita ya madawa ya kulevya.. kwa nini hajifunzi, kwa nini asitafute njia nzuri ya kutaka kusimamia ofisi yake vyema bila kuacha makovu kwa watu wengine?

Sitaki kuyataja mengi ya Makonda mfano lile la uvamizi wa kituo cha redio, natapenda nisimamie hili la maafsa elimu Mkoa wa Dar es salaam! Mh Rais itafute ile video, kwa hali ya kawaida ukiisikiliza utachukulia poa tu lakini maneno na maelekezo ya huyu RC kwa wale maafsa elimu ni dhihaka na dharau kwako mh Rais! Makonda anakuvua nguo, ule ni ujumbe kuwa baadhi ya wateule wako wana mapungufu makubwa sana ya kiuongozi, hii dhihaka na jeuri kwa watumishi wenzake anaitoa wapi!

Mh Rais, wafanyakazi wana njia za kuwarekebisha na kuongeza ufanisi kazini, sijawahi sikia njia za kumrekebisha mfanyakazi afanye kazi kwa bidii, weledi na ufanisi ni kumtisha na kumkejeli! sijawahi sikia wala kusoma kokote pale kuwa ili wafanyakazi wafanye kazi kwa uadilifu, weledi na ufanisi njia sahihi ni kuwatisha, kuwatukana na kuwadhalilisha!

Kuna njia za kuwamotivate wafanyakazi, wafanyakazi wanahitaji kupewa motivation (mshahara mzuri, mazingira mazuri ya kazi, wanahitaji faraja, upendo, kuthaminiwa na kutambulika, wafanyakazi wanahitaji social motivation, social recognize (wafahamike katika jamii kwa kazi wanazozifanya), wafanyakazi wanahitaji zawadi, wanahitaji kupewa cheti kwa kazi wanazofanya, wanahitaji muda wa kupumzika na siyo kukesha kazini , wanahitaji mahusiano mazuri na mwajiri wao , wafanya kazi wanafurahi sana pale wanapotambua mwajiri wao ana waamini (Makonda kila siku anawatukana na kuwambia nusu ni vihio )!, utumishi wa umma hasa Dar es Salaam imekuwa sehemu ya mateso na dhihaka! Hivi mh Rais na watanzania wenzangu hivi mnajua kwa nini kila siku Makonda anatafuta kujipenyeza katika magazeti na media na mbalimbali? Makonda huwa anatafuta motivation hasa (social motivation & recognize, anataka kutambulika).

Sina nia mbaya na huyu RC wala sihitaji atumbuliwe ila namshauri atambue hizi ni ofisi za umma, yeye ni kijana bado yuko kwenye game Zaidi ya dk 90, atambue utu wa mtu na atambue pia watu kama yeye na style ya uongozi wao huwa wanaitumikia jamii kwa muda mfupi sana! Bado una nafasi ya kurekebisha na bado utendaji wako ukaonekana.

Ni mimi Mwanakiji wa kijijini.
 
le madame

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
477
500

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom