Mh. Rais Kwa hali hii watu wabaya watapitia humo humo.

Kkimondoa

JF-Expert Member
May 31, 2014
4,453
4,933
Naziona dalili mbaya kwenye taifa letu tena ya hatari hadi nimeanza kuiogopa matukio haya yanayo tokea sasa yana ashiria hatari kubwa huko tuendako ,watu wabaya nao watatumia mwanya huo huo kukamilisha matakwa yao , majibu mepesi ya serikali kwenye matukio makubwa na ambayo hayakuwahi kutokea tanzania yana ashiria kuwakaribisha watu wabaya kutekeleza mambo yao na kuiuzia serikali tuhuma

Majibu yaliyo tolewa kwa MIILI SABA RUVU ,kupotea kwa BENI SAA NANE na KUTOLEWA BASTOLA HADHARANI NAPE (MB),KUINGIA NA SILAHA OFISI ZA CLOUDS na sasa hili la huyo mwana mziki ROMA yatakuwa chambo kwa watu wabaya kukamilisha yao. Kama hata watu maarufu tena wenye heshima kubwa wanafanyiwa hayo hadharani mchana kweupe ni vipi kwa wale wasio maarufu na wasio julikana kabisa?? Huenda wamesha potea kwa maelfu .

Serikali yetu tunaomba mbadilishe namna ya ku deal na matatizo , njia na mbinu mnazo tumia sasa nadhan zinalitia taifa kwenye hatari endapo haya yataendelea kuchukuliwa kirahisi rahihisi , hata ndani ya ndoa kama mke na mume wakiwa na ugomvi na ugomvi wao ukawa wazi na usipo suluhishwa vyema basi ndipo hapo wabaya wanapo anza kutumia mwanya huo kukamilisha malengo yao.

Naiona Tanzania si sehemu salama tena ,tanzania imebadilishwa ,tanzania inaogopesha, tanzania si ya amani tena kwa sasa.

Mifumo ya kuifanya tanzania kuwa kama Rwanda haitwezekana maana hakukuwa na maandalizi yeyote ya kuifanya iwe kama Rwanda tangia uhuru wake

Haitawezekana bali itazidi kuharibika na kuzidi kushuka kiuchumi kila uchwao pesa kubwa inayo tegemewa na serikali inatoka mikononi mwa wananchi kwa maana serikali bado haijajijenga kiuchumi kuweza kujiendesha bila mchango wa wananchi,maisha ya wananchi kila siku ndiyo yanayo ilisha serikali na misaada toka kwa wahisani,

Nadhan haitawezekana kuwa kama uganda maana hatukuandaliwa kuwa hivyo tangu uhuru wake hiyo tanzania si ya hulka hiyo na ikilazimishwa nchi itazid kuporomoka na kuharibika kila uchwao na kuharibu taswira yake kwa mataifa mengine.

Humphrey .P. Kasekwa
Kasekwahump@gmail.com
Simu Na 0754****23
 
Back
Top Bottom