Mh. Rais, haya majipu bila kuwa na katiba mpya, ukiondoka yatajirudia

mdesi

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
1,366
2,202
Mtukufu rais, umeonesha nia njema kwa nchi yetu, kwa mawazo na vitendo. Umeleta heshima na udhamini wa majukumu anaypewa mtu, dhana ya mazoea hakika imeanza kuondoka kwa kasi miongoni mwetu.

Haya yote hayatakuwa na msingi endapo hayatawekwa kwenye katiba. Inamaana uking'olewa kwenye kura za maoni kipindi cha pili atakayekurithi ataweza endesha inchi kwa jinsi atakavyo ona na hata kuturudisha tulikotoka.

Utatumbua mijipu afu baadae inarejea tena inakuwa sugu. Tiba ya moja kwa moja ni katiba, vinginevyo hamna maana.

Tulijionea wa bunge wabunge la katiba walivyochezea mapendekezo ya katiba tulioitaka,kwa fedha nyingi ya wavuja jasho.

Naomba turudishiwe katiba yetu tuliyoipendekeza isipokuwa sura moja tu inayohusu muungano; hicho ni kipengere pekee unachoweza kifanyia kazi upya. Lakini mengine yote yarudi kama tulivyo yapendekeza. Sina mengi ni hayo tu Ndugu Rais.
 
Mtukufu rais, umeonesha nia njema kwailenchi yetu, kwa mawazo na vitendo. Umeleta heshima na udhamini wa majukumu anaypewa mtu, dhana ya mazoea hakika imeanza kuondoka kwa kasi miongoni mwetu. Haya yote hayatakuwa na msingi endapo hayatawekwa kwenye katiba. Inamaana uking'olewa kwenye kura za maoni kipindi cha pili atakayekurithi ataweza endesha inchi kwa jinsi atakavyo ona na hata kuturudisha tulikotoka. Utatumbua mijipu afu baadae inarejea tena inakuwa sugu. Tiba ya moja kwa moja ni katiba, vinginevyo hamna maana....
Tulijionea wa bunge wabunge la katiba walivyochezea mapendekezo ya katiba tulioitaka,kwa fedha nyingi ya wavuja jasho.

Naomba turudishiwe katiba yetu tuliyoipendekeza isipokuwa sura moja tu inayohusu muungano; hicho ni kipengere pekee unachoweza kifanyia kazi upya. Lakini mengine yote yarudi kama tulivyo yapendekeza. Sina mengi ni hayo tu Ndugu Raisi....
Na kwa sababu wanaccm walio wengi sasa hivi bado wanamgwaya magufuli, Rais anaweza kutumia nafasi hiyo kuirudisha ulingoni katiba ya Warioba na akiamua itapita. Waifanyie marekebisho kwenye baadhi ya sehemu kwa mfano namna wabunge wanavyoweza kupatikana, utaratibu wa 50-50 kati ya wanaume na wanawake haufai. Kila mtu aingie bungeni kwa juhudi zake, hakuna upendeleo wa mwanamke wala mwanamme. Lakini pia suala la Muungano na idadi ya serikali, mapendekezo ya awali ya Warioba yatatuvuluga, yapitiwe upya. Mambo mengine yawe kama wananchi walivyopendekeza kwenye rasmu ya Warioba.
 
Hata ije katiba ipi kuna watakaoona haifai.

Katiba pekee si suluhisho, suluhisho ni kuuwa wala na wapokea rushwa. Bila kusahau wezi wa mali ya nchi.
 
Nchi iongozwe kwa mujibu wa katiba, katiba ya warioba iongezewe iboreshwe otherwise iachwe hivyo hivyo, fullstopp
 
Katiba ya Warioba ifanyiwe marekebisho kidogo kwenye sura na muundo wa Muungano....isiwe serikali 3...iwe mbili kwa Moja! tu na waingize Takukuru na wapewe meno!
 
Back
Top Bottom