Kila mwenye akili timamu analijua hilo, kwamba kwa mujibu wa Katiba yetu, Raisi atatawala mwisho miaka 10. Juhudi anazofanya Raisi wetu za kupiga vita wizi ubathirifu uzembe na uhujumu uchumi,ni za kupongezwa na kila mtakia mema Nchi hii.
Wasi wasi wangu ni je? Baada ya miaka yake kuisha, iwe mitano au 10, na tukamchagua mwingine mwenye dira tofauti itakuwaje?. Siasa hazitabiriki. Hata wakati tunamchagua Mzee Mkapa, hakuna Ambaye alijua malengo yake ya mfukoni. Lakini baada ya kuanza tu uongozi akaamua kuuza kila kitu kizuri kilichoanzishwa na Baba wa taifa. Tena akauza bila hofu kabla hata ya mwalimu kuaga dunia.
Mimi Roho iliniuma sana. Lakini cha ajabu Juzi tu yeye mwenyewe Mkapa alisikika ktk vyombo vya habari akijutia uamuzi wake ule. Ambao mpaka Leo umefanya Watanzania wengi kuathirika sana kimaisha.
Ushauri wangu kwa Raisi Magufuli. Ni muhimu sana tena iwe mapema kabisa ufanyike mchakato wa katiba mpya.tena iwe ni ya wananchi wote. Asiruhusu kuingingiliwa kisiasa kabisa. Lengo letu wote Kama nchi Liwe ni kuweka dira ya MAENDELEO ya miaka 100 ya nchi yetu. Na iweke wazi kuwa. Chama chochote cha siasa kikikamata dola, pamoja na nyongeza ya sera za vyama vya siasa lakini dira kuu iwe ni KATIBA YA WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Na hii imesaidia sana Manchi ya wenzetu wanaoona mbali. Vinginevyo basi itakuwa Rais wetu pamoja na juhudi zake zote lakini Anatwanga maji ktk kinu