Mh rais, hawa ndio CCM walioua na wanaoua ushirika nchini

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,098
8,727
Mh rais natumai Jumapili ya leo utakuwa umepumzika na unaendelea na maandalizi ya kufanya kazi juma la kesho.

Nikuandikiae ujumbe ni mtanzania niliyepata fursa ya kufanya kazi na wakulima wa mkoa wa Morogoro kupitia kwenye vyama vyao vya ushirika kwa kutoa huduma ya kukusanya madeni ambayo kwa jinsi nilivyokusanya nilipewa mikopo ambayo vyama vya ushirika vinadaiwa kutoka kwenye mabenk mbalimbali. Pili walinipa madeni ambayo ni amana na akiba za wanachama.

Nilianzia katika saccos iliyoitwa Mkasu. Chama hiki kilishafunga milango, hakukuwa na mtu ofisi. Chama hiki kilikuwa na mikopo zaidi ya milioni 800 kutoka benk ya TIB na pesa zao zaid ya 1bil. Chanzo cha kifo cha chama hiki ni siasa. Wanasiasa waliingia hapo wakakopa na kukopeshana mikopo hewa, sasa wote wamekimbia ila wengi wao ni wazito sasa.

Nilikaa wiki moja na kukusanya 25m sasa chama kimefufuka na kimeanza upya.

Chama cha pili ni Udzungwa hapa ndo nimekuta wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi wametafuna zaidi ya 4b, mmojawapo akiwa mzee Mohamedi kamanda wa vijana mkoa wa Morogoro. Pia yupo Kifyoga, Katibu Mwenezi wa sasa CCM wilaya ya Kilombero, pia yupo Meya Mstaafu Ndugu Mguruta, Meya wa sasa (CCM), yupo mjumbe wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero CCM, Ndugu Msavira.

Chama hiki kilianzishwa na wakulima wa miwa. Viongozi hawa na wengine ambao walikuwa makada wa CCM walijipa majukumu mazito wakakopa mikopo CRDB na TIB zaidi ya 2bil. Kilichoniumiza Mh. rais ni watu hawa niliowataja kukataa kulipa madeni yao na kukimbilia mahakamani.

Kwakweli Mh. rais nilikuta chama hakina hata sent tano, nimekusanya milioni 90 ndani ya wiki moja na waliobakia viongozi wa chama waliopita wakiongozwa na Mguruta wamekimbilia mahakamani na mahakama bado inawakingia kifua.

Sasa nmeingia Turiani saccos, naomba ulinzi wako niwafunge CCM wenzako.

Naomba kuwasilisha.

Ni mimi Sifileo.
 
Watakuua hao ni wauaji Magufuli mwenyewe ile tuhuma ya kugawa million kumi kumi inamtafuna hakuna msafi sisiemu awe makufuli awe makomeo hakuna msafi kamwee
 
Back
Top Bottom